Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba iliyopifunga Yanga 2019

IKIWA zimepita mechi saba wakishindwa kufua dafu mbele ya Yanga, wekundu wa Msimbazi (Simba), watakuwa wakijaribu bahati yao, kwa mara nyingine tena, Aprili 16 kuona kama wanaweza kurudia kile ambacho walifanya kwa mara ya mwisho msimu wa 2018/19.

Ndio! Mara ya mwisho kwa Simba kuifunga Yanga kwenye Ligi ilikuwa msimu huo na bao lao alifunga Meddie Kagere aliyekuwa amejiunga na timu hiyo akitokea  kwa miamba ya soka la Kenya, Gor Mahia.

Ndani ya michezo saba iliyopita, Simba imetoka sare mara tano na kupoteza mara mbili, yote waliyofungwa ni kwa bao 1-0.
Tangu Februari 16, 2019 ,  Simba  imebakia na wachezaji watano walioanza kikosi cha kwanza, kilichoifunga Yanga (2018/19)  kwenye  Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Wanajangwani akibakia beki Abdallah Shaibu 'Ninja'
Nje na hao watano, kuna  Mzamiru Yassin ambaye alikaa benchi na sasa ni panga pangua kikosi cha kwanza na kiwango chake kwa sasa kipo juu.

Dabi hiyo ambayo itazikutanisha timu hizo kila moja ikiwa kwenye kiwango bora kwenye mashindano yote, huku mashabiki wa timu hizo wakiendelea kutambiana.
Ikumbukwe  wiki chache zilizopita Simba ilitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga nao wakifanya yao upande wa Shirikisho, wote wawili pia wametinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kama ASFC, pia wameshinda mechi zao za mwisho kabla hazijakutana Aprili 16 .

Yanga imetoka kushinda na Kagera Sugar mabao 5-0 Uwanja wa Azam Complex na Simba dhidi ya Ihefu mabao 2-0 (Highland Estates), hivyo timu hizo zina morali ya kutosha.
Inawezekanana ukawa unajiuliza wako wapi nyota ambao walicheza dabi ya msimu wa mwisho kwa Simba kuifunga Yanga, hii ni orodha kamili.


KIKOSI CHA SIMBA SC vs YANGA SC
Aishi Manula (Simba), Zana Coulibaly(Africa Sports),Mohamed Hussein (Simba),Juuko Murshid (Vipers),Pascal Wawa (SBS), James Kotei (Mtibwa),Jonas Mkude(Simba, anaanzia benchi),Clatous Chama (Simba),John Bocco (Simba),Meddie Kagere (SBS) na Emmanuel Okwi(Erbil SC).
Akiba walikuwepo Deo Munishi 'Dida' (Namungo),Nicholas Gyan (SBS),Yusuph Mlipili (Prisons), Mzamiru Yassin (Simba),Hassan Dilunga (Hana timu), Haruna Niyonzima ( Al-Taawon SC) na Rashid Juma (Ihefu).
Kati ya mastaa hao waliobakia Simba, wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha kwanza ni Manula, Chama ambaye anaongoza kwa asisti 14, Mzamiru, Tshabalala, huku Bocco wakati mwingine anakaa benchi.


KIKOSI CHA YANGA
Ramadhani Kabwili (Rayons Sports), Paul Godfrey (SBS),Gadiel Michael(Simba), Andrew Vicent Dante (KMC),Kelvin Yondani (Geita Gold), Abdalah Shaibu (Yanga),Feisal Salum (Nje ya timu), Papy Tshishimbi  (Ihefu), Heritier Makambo (Congo), Amis Tambwe (SBS) na Ibrahim Ajibu (SBS).
Wa akiba walikuwa ni Klaus Kindoki (Congo),Juma Abdul (SBS),Mohamed Issa Banka (Polisi Tz), Juma Makapu (Ihefu), Mrisho Ngassa (Ana kituo cha soka), Haruna Moshi (Kastafu) na Matheo Anthony (KMC).


WALICHOZUNGUMZA BAADHI YAO
Kipa Dida ambaye anacheza Namungo kwa sasa, licha ya kukaa benchi katika mchezo huo anasema "Mechi za dabi hazizoeleki ndio maana zina maumivu makali kwa timu inayopigwa na furaha kwa inayoshinda, natarajia mchezo wa Aprili 16 utakuwa mgumu."
Kwa upande wa beki wa KMC, Dante anasema "Timu inayokuwa vizuri kwa siku hiyo ndio itakayowapa raha mashabiki wake, mfano hiyo mechi ambayo Simba ilitufunga 2019 ilituumiza sana wachezaji mwisho wa siku ndio matokeo hatukuwa na namna nyingine."