Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa Akrama:Nilitoa kadi Simba kimakosa

Muktasari:

  • Ingawa katika kumbukumbu zake anasema kilichomsukuma kuingia kwenye uamuzi ni majeraha ya goti wakati akicheza timu za madaraja ya chini kama mwanasoka.

MIONGONI mwa marefa walioingia kwenye historia za kuchezesha dabi za Simba na Yanga nchini ni Mathew Akrama.

Ingawa katika kumbukumbu zake anasema kilichomsukuma kuingia kwenye uamuzi ni majeraha ya goti wakati akicheza timu za madaraja ya chini kama mwanasoka.

"Nilianza kuchezesha mechi za Ligi Kuu 2006 nikiwa kama refa wa msaidizi na baada kustaafu  mwamuzi Issarow Chacha mwaka 2007 nikashauriwa nibadilishe nafasi hiyo ili niwe refa wa kati na ndiye aliyenikabidhi filimbi na kunibariki," anasema mwamuzi huyo mstaafu na kuongeza:

"Mwaka 2008 nikaanza kuchezesha kama mwamuzi wa kati mchezo wangu wa kwanza niliuona  mgumu ni dhidi ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kipindi hicho Mecky Maxime alikuwa nahodha, wale watu ni ndugu nje ya uwanjani ila siyo dakika 90."

"Mwaka 2012 kati ya Yanga na Simba nilipomwonyesha kadi ya njano mchezaji wa Simba Haruna Moshi badala ya nyekundu baada ya kumchezea vibaya wa Yanga,"anasema Akrama.

"Ilikuwa mechi yangu ya kwanza ya dabi  kama mwamuzi wa kati, presha ilikuwa kubwa, ingawa baada ya hapo viongozi wa timu hizo waliona unyoofu wa maamuzi yangu na wao ni shuhuda wa hilo,"anasema.

Katika kumbukumbu za maktaba ya Mwanaspoti, mechi hiyo ya dabi ya Ligi Kuu iliisha kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa(Sasa kwa Mkapa).

Katika mchezo huo ulioanza Saa 1:02 usiku, Akrama alimtoa kwa kadi nyekundu winga Simon Msuva wa Yanga dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu beki wa Simba, Juma Nyosso.

Siku hiyo, Simba walitangulia kwa bao la kiungo Amri Kiemba dakika ya pili, kabla ya mshambuliaji Said Bahanuzi kuisawazishia Yanga dakika ya 63 baada ya beki Paul Ngalema kuunawa mpira kwenye boksi.

Akrama alimuonyesha kadi ya njano Boban kwa rafu hii lakini Akrama alilaumiwa kwa kumuonyesha kadi ya njano badala ya nyekundu kiungo wa Simba, Boban licha ya kumchezea rafu mbaya beki wa Yanga, Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul.

Na pia alilaumiwa kuwa kutomchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.


USHIRIKINA VYUMBANI

Anasema kuna baadhi ya wachezaji wamejengwa katika mitazamo ya kishirikina, badala ya kuzingatia miiko ya soka na kufanya   mazoezi kwa bidii ambayo yakiwaweka fiti wanakuwa na uwezo wa kucheza kwa kiwango cha juu.

"Ilikuwa inanishangaza sana ukiingia kukagua vyumba vyao vya kubadilishia nguo unakuwa wanafanya vitu hivyo wazi wazi bila kujali na wanakuwa wanajisifu kama vile ni vitu vizuri, kiukweli kama hayo mambo yapo hadi sasa wanapaswa kubadilika na kuona fursa zilizopo katika soka ambazo zitawatoa kimaisha," anasema na kuongeza:

"Nilichokuwa nakifanya kabla ya kuingia uwanjani nasali ili kama zipo nguvu za giza ziweze kuondoka na kila mtu atoke akiwa salama kuna wakati nilikuwa nawashirikisha na watumishi wa Mungu, ndiyo maana sikuwa na hofu hata nikiona wanafanya shiriki."


UCHUNGAJI WAKE

Baada ya kustaafu kuchezesha Ligi Kuu mwaka 2017 akapata muda mwingi wa kuhubiri na kufanya shughuli zake zingine.

"Niliokoka mwaka 2003 hata wakati nafanya kazi ya uamuzi nilisimama na Mungu, ndiyo maana sikuwahi kuyumbishwa," anasema.

"Nimekuwa shuhuda mzuri kwa wanamichezo kuwaambia katika kazi zao ushirikina hauwezi kuwasaidia zaidi ya uharinifu na wakajikuta wanapotea katika ramani ya michezo na kupoteza pesa zao kwa waganga."

Jambo analoliomba kwa  mamlaka za soka nchini, wawape thamani waamuzi waliopo viwanjani na waliostaafu, kutokana na majukumu makubwa wanayoyafanya ambayo nyuma yake wanakumbana na changamoto kubwa.

KUHUSU LIGI,WAAMUZI

Anasema anawaona baadhi yao wanapata nafasi ya kuchezesha mechi za kimataifa, hivyo ameipongeza TFF kwa hilo, kuhusu Ligi Kuu imetoa timu zinazofanya vizuri kimataifa akiitaja kama ni hatua nzuri inayoonyesha ukomavu na kukua kwa ligi hiyo.

"Kwa hilo niwapongeze viongozi wa TFF chini ya Wallace Karia kuhakikisha soka linakuwa siku hadi siku, wadhamini kuongezeka hilo ni jambo zuri," anasema Akrama ambaye kazi ya uamuzi aliianza mwaka 2000 akapanda kuchezesha Daraja la Kwanza 2005, kisha Ligi Kuu 2006.


KUMBE BABA YAKE MSANII!

"Ilikuwa  ngumu kushawishika kuigiza na baba yangu kwa sababu tuliishi maeneo tofauti mimi Mwanza yeye Dar, ila kati ya kazi zake ambazo nilikuwa nazipenda sana ni Ua Jekundu na Kabuli la Safia," anasema.

Nini kimekuvutia kwenye makala hii; tuandikie; +255658-376 417