Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PUMZI YA MOTO: Maajabu ya tatu fainali Z'bar Heroes

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Hiyo ilikuwa ni fainali ya tatu ya Zanzibar Heroes katika historia tangu timu hiyo kuanzishwa 1947.

LEO, timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' itacheza fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Burkina Faso katika kusherehekea miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hiyo inakuwa ni fainali ya tatu ya Zanzibar Heroes katika historia tangu timu hiyo kuanzishwa 1947.

Na bahati nzuri zaidi ni kwamba fainali hizo zote  zimekuja baada ya Mapinduzi ya 1964.


HISTORIA YA ZANZIBAR HEROES

Februari 1926, nchi nne za Afrika Mashariki zilizokuwa makoloni ya Uingereza; Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar zilikutana mjini Nairobi, Kenya kujadili namna ya kuanzisha mashindano ya pamoja ya soka.

Hii ilifuatia ushawishi wa mabepari wawili ndugu, Lever Brothers kutoka familia ya Lever ambao mwaka mmoja uliopita, 1925 walinunua haki za kampuni moja ya Uingereza ya Gossage iliyokuwa na viwanda vya sabuni nchini Uingereza na kuwa na tawi lake Kenya.

Lakini, hata hivyo, Tanganyika na Zanzibar zikajitoa kwenye mashindano na kuwaacha Uganda na Kenya wacheze wenyewe. Mashindano hayo yakaanza 1926 kwa jina la Kombe la Gossage.

Baada ya kujitenga kwa muda mrefu hatimaye Zanzibar ikajiunga na Gossage Cup 1947. Huo ndiyo mwaka ambao timu ya taifa ya Zanzibar inahesabiwa kuanza rasmi.

Zanzibar ilijiunga na Gossage Cup miaka miwili baada ya Tanganyika nao kuwa walishajiunga 1945. Hata hivyo Zanzibar haikuwa ikifanya vizuri kwenye mashindano hayo hadi 1959 ilipomaliza katika nafasi ya pili.

Tofauti na miaka mingine, mwaka huo mashindano yaliendeshwa kwa mtindo wa kuhesabu alama hivyo hakukuwa na fainali.

Miaka mingine huko nyuma na hata huko mbele, mashindano hayo yaliendeshwa kwa mtindo wa mtoano na bingwa kupatikana kwa mchezo wa fainali.

Mwaka 1966 Kombe la Gossage lilibadilishwa jina na kuwa kombe la Palmeras Challenge bila Zanzibar kufika fainali. Liliitwa hivyo kuanzia 1967 hadi 1971 bila Zanzibar kufika fainali.

Kuanzia 1972 mashindano hayo yakaitwa Palmeras CECAFA Championship. Zanzibar iliendelea kuwa wasindikizaji kwenye mashindano hayo hata yalipobadilishwa tena jina 1974 na kuwa Cecafa Senior Challenge Cup.


FAINALI YA KWANZA 1995

Baada ya miaka mingi ya kusubiri hatimaye 1995 Zanzibar ilifika fainali ya kwanza ya Cecafa Senior Challenge Cup, mashindano yaliyofanyika Uganda.

Hiyo ilikuwa fainali ya kwanza katika historia ya soka la Zanzibar katika mashindano yote iliyoshiriki.

Fainali hiyo ilikuja miaka 31 baada ya Mapinduzi ya Januari 1964.

Ilivyokuwa - mashindano ya 1995 yalifanyika Uganda huku wenyeji wakipewa nafasi ya kuwa na timu mbili, Uganda A na Uganda B. Tanzania Bara ilishiriki mashindano hayo kama mabingwa watetezi baada ya kushinda ubingwa mwaka mmoja uliopita nchini Kenya.

Kulikuwa na viwanja viwili, Nakivubo wa Kampala na Bugembe wa Jinja. Jumla ya timu nane zilishiriki na kugawanywa kwenye makundi mawili.

Kundi A ambalo Zanzibar ilikuwepo pia lilikuwa na wenyeji Uganda A, Kenya na Rwanda lilibaki Kampala kwenye uwanja wa Nakivubo. Na kundi B ambalo lilikuwa Jinja liliundwa na Tanzania Bara, Ethiopia, Uganda B na Somalia.


MATOKEO YA ZANZIBAR KUNDI A

Kenya 2-0 Zanzibar

27/11/1995

Zanzibar 2-1 Rwanda

29/11/1995

Uganda A 0-1 Zanzibar

4/12/1995


NB: Mechi hiyo ilivunjika dakika ya 85 baada ya mashabiki wa Uganda kurusha mawe uwanjani huku Zanzibar ikiongoza 1-0. Zanzibar wakahesabiwa washindi.  

Ushindi huo ukawafanya Zanzibar wafuzu nusu fainali na kupangwa kukutana na Ethiopia, Desemba 7, 1995 hukohuko Bugemba, Jinja. Zanzibar wakashinda 1-0 na kutinga fainali.

Fainali hiyo ikawakutanisha na wenyeji wengine,  Uganda B Desemba 9, 1995 dimbani Nakivubo mjini Kampala. Zanzibar ikashinda bao 1-0 kwa bao la Victor John Bambo na kuwa mabingwa.

Kikosi cha Zanzibar kilichoshinda Cecafa Senior Challenge Cup 1995 kilijumuisha: Shekha Khamis (nahodha), Abdulrahman Mussa, Sabri Ramadhan 'China'

Victor John Bambo, Nassor Salum 'Chollo', Seif Khalfan, Issa Gazza, Nasib Salum, Shaaban Ramadhan, Riffat Said, Said Mohamed 'Makapu', Juma Sheikha, Hassan Ramadhan Wembe,   Salum Ali, Mbegu Mohamed, Uzia Abdallah, Simai Haji, Mohamed Shaaban 'Kachumbari' na Mbarouk Suleiman.


FAINALI YA PILI 2017

Miaka 22 baada ya fainali ya kwanza 1995, Zanzibar ikacheza tena fainali ya pili 2017. Hiyo ilikuwa fainali ya Kombe la Cecafa kama ile ya 1995 - safari hii mashindano yalifanyika Kenya katika miji ya Kakamega na Machakos.

Zanzibar ilikuwa kundi A pamoja na Tanzania Bara ambayo safari hii ilitumia jina la Kilimnjaro Stars, Kenya, Libya na Rwanda.

Zanzibar 3-1 Rwanda

5/12/2017

Tanzania 1-2 Zanzibar

7/12/2017

Kenya 0-0 Zanzibar

9/12/2017

Libya 1-0 Zanzibar

11/12/2017

Nusu fainali

Uganda 1-2 Zanzibar

15/12/2017

Fainali

Kenya 2-2 Zanzibar [penati 3-2]

17/12/2017

Kikosi kilichofika fainali kilikuwa na makipa

Ahmed Ali 'Salula' (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman 'Wawesha' (JKU); mabeki Abdallah Haji 'Ninja' (Yanga), Moh'd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed 'Sangula' (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh 'Machupa' (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame 'Luiz' (Mlandege), Issa Haidar 'Mwalala' (JKU), Abdulla Kheir 'Sebo' (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

Viongo walikuwa ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma 'Zimbwe' (Chipukizi), Mohd Issa 'Banka' (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman 'Pwina' (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Ali Yahya (Academy Spain), Hamad Mshamata (Chuoni) na Suleiman Kassim Selembe (Majimaji).

Washambuliaji walikuwa Kassim Suleiman (Prisons),

Matteo Anthony (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ)

Khamis Mussa 'Rais' (Jang'ombe Boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto),


FAINALI YA TATU 2025

Mwaka huu ikiwa ni miaka 30 baada ya ile fainali ya kwanza kabisa, Zanzibar wanaingia tena fainali. Lakini safari hii ni katika mashindano mengine,  Kombe la Mapinduzi.

Mashindano hayo ambayo asili yake ni klabu  yamefanyika katika mfumo wa kushirikisha timu za taifa mwaka huu na wenyeji kutinga fainali. Baadhi ya wachezaji waliokuwepo 2017 na safari hii pia wapo ni kama Feisal Salum.