Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Odegaard Injini ya Arsenal yenye shida hii

Muktasari:

  • Katika mchezo huo wenyeji Tottenham walipoteza mchezo huo kwenye uwanja wao wa kisasa kwa kufungwa bao 1-0.

JUMAPILI jioni iliyopita katika Ligi Kuu England (EPL), Kaskazini mwa Jiji la London kulikuwa dabi kali ya wapinzani wa jadi kati ya Tottenham Hotspur na Arsenal.

Katika mchezo huo wenyeji Tottenham walipoteza mchezo huo kwenye uwanja wao wa kisasa kwa kufungwa bao 1-0.

Mchezo huo ni moja ya mechi kali zinazotazamwa na mamilioni ya wapenda soka duniani kutokana na historia ya mechi kuwa na upinzani mkali katika dakika zote.

Mchezo huo ulimalizika kwa Arsenal kupata bao la ushindi dakika ya 64 kupitia kwa beki wa kati, GabrieI Magalhàes  mara baada ya kumalizia vyema kwa kichwa mpira wa kona kutoka kwa Bukayo Saka.

Arsenal ilicheza bila injini yake ambaye ni kiungo mshambuliaji, Martin Odegaard aliyekosekana kwa sababu ya kuwa na majeraha ambayo aliyapata wiki mbili zilizopita katika mchezo wa kimataifa.

Injini hiyo ambayo iliibeba Arsenal katika msimu uliopita nafasi ya eneo lake alikuwepo Thomas Partey, Jorginho na Kai Havertz ambaye alilambwa kadi nyekundu.

Odegaard ni injini ambayo eneo la katikati analimudu vyema akiweza kuchezesha timu vizuri, kusaidia mashambulizi na kufunga mabao ambayo hatimaye Arsenal yaliibeba na kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita.

Nahodha huyo wa Arsenal na timu ya Taifa ya Norway alipata majeraha ya kifundo cha mguu wa kushoto Jumatatu, wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Australia.

Majeraha hayo yalikuwa makali kiasi cha kusababisha kushindwa kuendelea na mchezo na kutolewa ndani ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine.

Wakati akirejea jijini London, Odegaard mwenye umri wa mkaka 25 alionekana akitembea kwa usaidizi wa vifaa tiba magongo maalumu vya kutembelea jambo lililoashiria kuwa  lilikuwa kubwa.

Kutumia kifaa tiba hicho ni ishara kuwa alipata majeraha mabaya ya kifundo cha mguu ambayo huwa hayatabiriki kupona kwake kutokana na eneo hilo kubeba shinikizo kubwa la mwili.

Vilevile ni eneo ambalo limesheheni tishu laini nyingi na vijifupa vidogo vidogo kwa pamoja ambapo huunda ungio la kifundo pamoja na vijiungio vidogo vidogo katika eneo la funiko la mguu.

Akiwa nchini Norway katika matibabu na uchunguzi wa awali ilionyesha kuwa hakupata mvunjiko wa mfupa au mifupa. Hii ni kwa mujibu wa daktari wa timu ya taifa ya Norway, Ola Sand.

Daktari huyo alilieleza gazeti la VG la Norway kuwa Odegaard hakupata mvunjiko wowote, lakini tishu laini zilipata majeraha ambayo yanaweza kupona kwa wiki tatu, hivyo kuwa nje mwezi wote wa Septemba.

Shida kubwa ambayo ameipata ni kujeruhiwa kwa tishu laini ikiwamo ligamenti zinazoshika na kuunganisha mfupa mmoja na mwingine katika ungio la kifundo na maungio madogo ya vijifupa vya eneo la funiko la mguu.

Jeraha hilo alilipata mara baada ya kutua vibaya hatimaye kifundo kujipinda katika mwelekeo hasi, hali iliyochangia kuvutika kupita kiwango kwa ligamenti na tishu nyingine.

Hali kama hiyo inaweza kusababisha kuvutika sana kwa ligamenti, kuchanika, kukatika pande mbili au kuchomoka kutoka katika mfupa ilipojichimbia.

Kabla ya mchezo huo wa Jumapili, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alieleza kwa kifupi hali ya kiungo huyo kuwa bado anahitaji kufanyiwa majaribio na kutathimini ukubwa wa jeraha alilolipata.

Alieleza kuwa Odegaard ni mchezaji muhimu ambaye muda wote anatamani kuwepo uwanjani kuisaidia timu ili kupata mafanikio. Lakini kwa sasa inatazamwa kwanza afya yake.


TATHMINI YA JERAHA

Klabu kubwa za kulipwa duniani mchezaji anayewapa mafanikio ana umuhimu mkubwa na ni mtaji. Hata kama mchezaji ameumia nje ya majukumu ya klabu lazima wajiridhishe kwa kufanya tathmini ya kitabibu.

Kwa Arsenal, Odegaard ni mchezaji ambaye msimu uliopita aliwapa mafanikio makubwa, hivyo kulinda utimamu wa mchezaji huyo ni muhimu kwa maendeleo ya klabu.

Tathmini hufanyika ili kujua ukubwa wa jeraha na hatimaye kuchukua hatua sahihi za kitabibu ikiwamo matibabu kutoka kwa daktari bingwa.

Wakati anapata jeraha hilo ilidhaniwa pengine huenda amepata mvunjiko wa mifupa inayounda ungio la kifundo, lakini picha za awali za MRI zilionyesha kuwa hakupata mvunjiko wa mfupa au mifupa.

Idara ya afya ya Arsenal iliyo ndani ya benchi la ufundi ndiyo ambayo ina jukumu hilo. Hutathmini na kuamua nini kifanyike pamoja na kutoa ushauri wapi matibabu yafanyike.

Idara hiyo ikiona kuwa jeraha hilo liko nje ya uwezo wake huamua kwenda katika huduma za juu za matibabu kwenye vituo maalumu ambavyo klabu ina mkataba navyo au makubaliano maalumu.

Kwa sasa na ubora aliounyesha msimu uliopita Odegaard ana thamani inayokadiriwa kuwa kati ya Paundi 55.2 milioni hadi 92, hivyo hata wakiamua kumuuza klabu itapata faida kubwa.

Hii ni moja ya sababu inayofanya mchezaji kama huyo kupata huduma muhimu za afya za kisasa ili hatimaye kupona kwa wakati akiwa timamu na huku pia utimamu wake kiafya ukiboreshwa na kulindwa usiweze kuharibika.

Katika kutathmini ukubwa wa jeraha kunasaidia kukadiria muda wa mchezaji kupona kikamilifu na kurudi uwanjani akiwa timamu kama awali.

Katika umri wake wa miaka 25 na kiwango alichonacho vinamfanya kuwa mmoja wa wachezaji ambao wapo katika mpango wa muda mrefu wa Arsenal, hivyo kulindwa utimamu wake ni jambo lisiloepukika.