Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MEDDIE KAGERE: AS Vita watatuvusha

Muktasari:

Simba inasaka alama moja pekee kujihakikishia kusonga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika katika michezo miwili iliyosalia.

Simba inasaka alama moja pekee kujihakikishia kusonga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika katika michezo miwili iliyosalia.

POINTI 10 tulizopata mpaka sasa katika mechi nne za awali za makundi kwenye kundi letu hazitupi uhakika wa kufuzu hatua ya robo fainali kwani timu nyingine zinaweza kuzifikia tusipokuwa makini.

Ukiangalia tunaongoza Kundi A, huku tumebakiwa na mechi mbili kama zilivyo timu nyingine.

Hesabu zilivyo hizi pointi zetu tulizonazo kama tutashindwa kupata pointi nyingine katika mechi mbili zilizobaki hatutakuwa katika mahala salama na tutashindwa kufuzu robo fainali kama ambavyo wengi wanadhani.

Kwani Al Ahly ambao wapo nafasi ya pili wanapointi saba kama watashinda mechi zao mbili maana yake watakuwa wamefikisha pointi 13, jambo ambalo watakuwa wametuvuka pointi tatu.

Wakati huo huo Al Ahly wanamchezo mmoja na sisi ambao tunacheza kwao Misri na ukweli usiopingika kuchukua pointi angalau moja kule Uarabuni kama ambavyo wamefanya AS Vita si jambo rahisi.

AS Vita ambao wapo nafasi ya tatu kama wakishinda mechi zao mbili watakuwa wamefikisha pointi kumi tulizonazo wakati huu huku tukiangalia mechi zetu mbili zilimalizika kwa matokeo ya aina gani.

Kwa hali ilivyo Al Merrikh ambao wapo katika nafasi ya nne kama watashinda michezo yao miwili watafikisha pointi saba ambazo wakati huu wamezishikilia Al Alhy.

Dakika 90 za mechi yetu ya AS Vita zinaweza kuamua hatma ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kama ambavyo mashabiki wengi wanadhani, lakini kabla ya mechi hiyo kwangu naona bado nafasi ni ngumu kwani kila timu inaweza kufuzu kutokana na hesabu zilivyo.

Unajua hawa AS Vita watakuja wakiwa katika hali na morali ya ushindani kwani tuliwafunga nyumbani kwao bao 1-0, kwa maana hiyo hawatakubali kupoteza kwa mara ya pili dhidi yetu.

AS Vita mchezo wetu dhidi yao utaamua kwamba wanaweza kubaki katika mbio za kwenda robo fainali kama watashinda au kupata pointi dhidi yetu itakuwa faida kwa upande wao hivyo watakuwa kwa kupambana ili kufanikisha hilo.

Nasi hatutakubali kupoteza dhidi yao au kushindwa kupata pointi kwanza tupo nyumbani, ingawa tunawakosa mashabiki wetu lakini tutashindwa kuwa na uhakika wa kucheza robo fainali.

Bado tuna kazi ngumu na dakika 90, za mchezo wa AS Vita kumalizika ndio itafahamika kwamba Simba tunakwenda katika hatua inayofuata lakini ikiwa tofauti kazi itakuwa ngumu mno kutokana mchezo ujao tunacheza ugenini kule Misri.

Ugumu ambao nauona katika mchezo wetu na AS hawa jamaa wameweza kuweka rekodi msimu huu katika mashindano haya kwa kuchukua pointi kule Misri.

Kama ambavyo nilisema hapo awali ni ngumu kupata pointi pale Misri lakini AS Vita wameweza hilo kwahiyo wanaweza kuja na hali na morali kama ambavyo walikwenda nayo Misri na wakataka kuonyesha dhidi yetu.

Ukiangalia hiyo mechi walicheza vizuri na wao licha ya kuongoza kwa bao la kwanza walikuja kusawazisha baada ya Al Ahly kufunga mabao mawili la kusawazisha na kuongoza.

AS Vita katika mechi hiyo ya ugenini walifanikiwa kupata penati jambo ambalo ni gumu mno kutokea katika uwanja huo timu ngeni kupata penati.

Ugumu mwingine ambao upo katika mchezo huo na AS Vita ambao umeshika hatma yetu ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali hawa jamaa mara ya mwisho wanakuja hapa nchini tuliwafunga.

Tuliwafunga katika mechi ambayo ilikuwa ya maamuzi na baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1, tulisonga katika hatua ya robo fainali kama ambavyo tunahitaji wakati huu.

Aina ya mazingira ya mechi kama wakati ule yanafanana kwani wao wakishinda wanakuwa katika nafasi nzuri ya kwenda robo fainali na tukishinda sisi tutakuwa tayari tumesonga kwenye hatua hiyo.

Hivyo mechi itakuwa ngumu kulingana na mazingira yalivyo na kama ambavyo nimeeleza tunahitaji ushindi katika mchezo huo na baada ya dakika 90, kumalizika ndio tutakuwa na uhakika huo.

Kwa maoni kuhusu safu hii tuma ujumbe mfupi kwa meseji ya kawaida au Whatsapp kwenda namba 0658-376-417