Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mundhir Iman: Winga wa Chipukizi anayevuna kwa Maxi, Mpanzu

IMANI Pict

Muktasari:

  • Hivyo ndivyo anavyoanza kuzungumza winga wa Chipukizi United kutoka Pemba, Mundhir Iman ambaye msimu wa Ligi Kuu Zanzibar uliomalizika hivi karibuni amekuwa na mchango mkubwa kikosisi akihusika na mabao 21 - akifunga 12 na asisti tisa. 

“MCHEZO wa mpira wa miguu ni fursa, ajira na biashara inayoweza kukutoa kwa haraka na kutengeneza maisha vizuri, hivyo vijana ambao wapo katika kipindi cha utafutaji lazima wajitoe ili baadaye wapate maisha wanayoyahitaji.”

Hivyo ndivyo anavyoanza kuzungumza winga wa Chipukizi United kutoka Pemba, Mundhir Iman ambaye msimu wa Ligi Kuu Zanzibar uliomalizika hivi karibuni amekuwa na mchango mkubwa kikosisi akihusika na mabao 21 - akifunga 12 na asisti tisa. 

Chipukizi United iliyomaliza nafasi ya tisa kwenye msimamo imecheza mechi 30, ikishinda 10, sare 11 na kupoteza tisa huku ikifunga mabao 28 na kuruhusu 24, ikikusanya pointi 41.

Katika mahojiano na Mwanaspoti, Mundhir amezungumzia mambo mbalimbali, lakini katika soka kwa sasa anachota maujuzi kwa mastaa wawili Maxi Nzengeli wa Yanga na Elie Mpanzu anayecheza Simba, huku nje ya Tanzania akifuatilia kwa karibu anachokifanya Cristiano Ronaldo uwanjani na anaamini ipo siku atakuwa kama yeye.

IMA 01

“Nilianza kucheza mpira wa miguu nikiwa na umri wa miaka minane. Nimewahi pia kuichezea timu ya Mkoa wa Kusini Pemba katika mashindano ya Copa Coca-Cola (2014), timu ya Taifa Tanzania chini ya umri wa miaka 14 (2015), kisha mwaka 2018 nilianza rasmi kuichezea Chipukizi hadi sasa nikiwa nimekaa hapa kwa kmiaka minane.

“Kitu pekee ambacho kilinifanya niendelee kucheza mpira wa miguu ni ule wakati ambao kila mechi nilikuwa napewa nafasi ya kucheza,” anasema.


MSIMU BORA

Mundhir anasema kitu ambacho kimemfanya kuwa bora zaidi ni kufanya mazoezi binafsi na kutenga muda mwingi wa kuupumzisha mwili.

“Msimu wa Ligi Kuu Zanzibar mwaka huu umekuwa ni mzuri kwangu na wenye mafanikio kwani nimeisaidia timu katika mabao 28 nimehusika kwenye 21 nikifunga 12 na asisti tisa,” anasema.

“Siri ya mafanikio haya ni mazoezi binafsi na kufuata maelekezo ya mwalimu kitu ambacho kinaniongezea umahiri na ubora katika mchezo.

IMA 02

“Licha ya kwamba nimefanikiwa kufunga mabao hayo ambayo ni mengi, nilikuwa na malengo makubwa zaidi ya kuwa mfungaji bora msimu huu, lakini imeshindikana.

“Nimeshindwa kuwa mfungaji bora kwa sababu wapo walionitangulia, lakini najivunia kuwa mchezaji wa pembeni ninayecheza namba saba na 11 kufunga mabao.” 


SHAVU KWA WENZAKE

Mundhir anasema timu ni muunganiko wa wachezaji, walimu na viongozi, hivyo kufanya kwake vizuri kumechangiwa na wenzake kutokana na kupatiwa pasi nyingi za kufunga ambazo zikifika ni nadra kukosa bao.

IMA 03

HAISAHAU MLANDEGE 

Anasema mechi ambayo hawezi kuisahau msimu huu ni ile waliyocheza dhidi Mlandege kwani ni miongoni mwa mechi ngumu ambapo ilikuwa lazima kushinda na wakatoka na ushindi bao 1-0.

Winga huyo anasema, mechi hiyo ilikuwa lazima kwao kushinda kwa sababu ya kujiweka katika nafasi nzuri.


WALIPOKOSEA

Malengo ya Chipukizi United msimu huu ilikuwa ni kumaliza nafasi za juu ikiwemo kubeba ubingwa, lakini imeshindikana Mundhir akifichua sababu iliyofanya hayo kutokea.

Nyota huyo anasema sababu kubwa ni usajili kwani waliaza msimu bila wachezaji saba tegemeo.

“Timu imeuza wachezaji saba ndio maana msimu huu hatukuwa vizuri sana. Huko nyuma ilikuwa hatufiki nafasi kuanzia ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar, lakini huu tumevuka zaidi ya hapo. Hiyo yote kwa sababu muunganiko ulikuwa mdogo, wachezaji hatujazoeana tofauti na hapo awali.”

IMA 04

Hata hivyo, Mundhir anasema makocha wanapaswa kupongezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya kwani licha ya kufanyika mabadiliko makubwa ya wachezaji, lakini timu hiyo imeendelea kusalia katika ligi kwa msimu ujao.


NDOTO YA KUCHEZA BARA

Kila mchezaji mwenye malengo anatamani kufika mbali, hivyo nyota huyo anatamani kucheza Ligi Kuu Bara akisema ni kubwa kuliko ya Zanzibar.

Licha ya matamanio hayo, anasema sio mwisho wa safari ila anataka kuvuka mipaka kwenda nje ya Tanzania.


MTUMISHI WA SERIKALI

Kama hujui Mundhir ni mtumishi wa umma, hivyo anapokuwa nje ya uwanja anafanya majukumu ya kitaifa.

Hata hivyo, winga huyo hataki kutaja sehemu anayofanyia kazi akidai kuna changamoto anakutana nazo kwani anapotoka mazoezini anatakiwa kuwahi kazini.

Anasema kuna wakati humuwia vigumu kujigawa japokuwa ana ruhusa maalumu kazini huku akili yake ikiegemea zaidi katika kipaji cha soka na ameamua kufanya hivyo kwa sababu kiwango cha fedha anachopata hakikidhi mahitaji.

IMA 05

CHANGAMOTO, USHAURI 

Mundhir anasema changamoto kubwa wanazokutana nazo wachezaji wengi wanaocheza soka Zanzibar wakati mwingine ni kupoteza vipaji vyao na ni kwa sababu ya hali duni za maisha walizonazo.

“Licha ya serikali kujitahidi kuwekeza katika michezo, bado wachezaji tuna hali duni za maisha. Baada ya kutoka mazoezini badala ya kupumzika inabidi tufanye kazi za nguvu ili kupata kipato cha kukidhi maisha. Kwa maana hiyo mpira kwa Zanzibar haulipi.”