Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MACHO MANNE : Angban ametumwa na nani ampige Kessy?

Muktasari:

Kwa sasa ndani ya Simba kumbe adhabu hazitolewi na makocha au viongozi tena, bali mchezaji yeyote akiamua anaweza kumwadhibu mwenzake na ikachukuliwa poa tu!

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Hali inayoendelea ndani ya klabu ya Simba inashangaza kidogo.

Kwa sasa ndani ya Simba kumbe adhabu hazitolewi na makocha au viongozi tena, bali mchezaji yeyote akiamua anaweza kumwadhibu mwenzake na ikachukuliwa poa tu!

Wiki iliyopita pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilichapwa bao 1-0 na Toto African ya Mwanza, matokeo ambayo wengi yaliwastaajabisha kwa vile ni kama hayakutegemewa kwa jinsi Simba ilivyokuwa ikipata matokeo mazuri katika mechi zilizopita sasa ikaja kupotea na timu inayopigana kubaki kwenye ligi.

Simba ilipata kipigo hicho ikiwa ni wiki moja tu tangu iondolewe katika michuano ya Kombe la FA na vibonde wa Ligi Kuu Bara, Coastal Union kwa mabao 2-1. Mechi zote ambazo Simba imepoteza ni zile za nyumbani.

Waziri Junior aliifungia Toto dakika ya 20 tangu mchezo huo uanze kikosi cha Simba kikiwa kimesheheni ndani kwa maana wachezaji wote 11 walikuwamo huku kocha wao Jackson Mayanja akiwa benchi, lakini timu ilishindwa kusawazisha bao hilo ingawa walikuwa wanajitahidi kufika eneo la hatari na mipira yao ilikuwa inapaa tu.

Simba ilikwama kurejesha bao hilo hadi ikienda mapumziko, ingawa kocha Mayanja alikuwa ameishatimuliwa katika benchi la ufundi kwa kukiuka masharti ya uwanjani, ila kutimuliwa kwake kulifuata baada ya bao hilo kufungwa.

Timu hizo zilirudi uwanjani ambapo dakika chache tu baada ya mpira kuanza, Hassan Kessy alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Edward Christopher, hapo ndipo songombingo lilipoanzia.

Kumbe waliobaki uwanjani walikuwa wanacheza na kinyongo na akili zao zilikuwa zikiwaza ni jinsi gani watamwadhibu mwenzao (Kessy) kwa kosa hilo.

Mpira ulimalizika na timu kurudi vyumbani, kipa Vincent Angban aliamua kuchukua sheria mkononi ya kumtwanga Hassan Kessy. Chanzo changu ambacho kilikuwepo chumbani humo kilisema Angban alimtwanga Kessy baada ya kupishana kauli, kipa huyo raia wa Ivory Coast alidaiwa kumuuliza kwa ukali beki huyo aliyetokea Mtibwa Sugar kwamba ni kwanini mara kadhaa amekuwa akifanya rafu za kuigharimu timu.

Inawezekana wote walikuwa na hasira ama mmoja kujifanya mbabe tu, Kessy naye imeelezwa alimjibu kwanini anamuliiza maswali hayo kwani yeye nani? Ndipo alipoanza kuchezea kipigo hicho ambacho hakikuamuliwa na yeyote. Najiuliza hivi Angban ulipata wapi ujasiri wa kumtwaga mwenzake? Nani alimtuma afanye hayo yote wakati wewe ni profesheno jamani!

Hata kama Kessy alifanya kosa, yeye Angban mara ngapi amekuwa akifungwa kizembe, nani aliwahi kumuadhibu? Na angeeleweka kama kutoka kwa Kessy ndiko kungezalisha bao lililoizamisha Simba, bao lilifungwa Kessy na wenzake wote walikuwa uwanjani, Angban alifanya juhudi gani kuiokoa Simba?

Mbona kina Hamis Kiiza na washambuliaji wengine walikuwa wakikosa mabao ya wazi langoni mwa Toto, lakini hao hawakuadhibiwa na mikono ya kipa huyo? Hapo ndipo kunakoleta shaka na kuzua maswali, au Mu Ivory Coast huyo alitumwa na mtu.

Wachezaji wengine wanajifunza nini kutoka kwa kipa huyo mwenye umri mkubwa kwa Kessy na hata wachezaji wengine?