Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KULA BATA: Ndo muda wa mastaa Bongo kujiachia

BATA Pict

Muktasari:

  • Baada ya kumalizika kwa msimu klabu mbalimbali hutoa muda wa mapumziko kwa wachezaji na benchi la ufundi kabla ya kuingia kambini tena kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

JUNI 29 itakuwa tamati ya msimu wa mashindano ya soka Bara wakati itakapopigwa mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), kati ya Yanga ambayo ni bingwa mara tatu mfululizo dhidi ya Singida Black Stars, mbungi ikitarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Baada ya kumalizika kwa msimu klabu mbalimbali hutoa muda wa mapumziko kwa wachezaji na benchi la ufundi kabla ya kuingia kambini tena kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Katika misimu miwili mfululizo, Yanga imekuwa ikicheza fainali dhidi ya Azam FC, lakini msimu huu imekuwa tofauti baada ya matajiri hao wa Chamazi kutolewa katikahatua ya 32 Bora na Mbeya City, huku Singida ikiiduwaza Simba kwa kuipiga mabao 3-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, Manyara.

Fainali nyingine ya Yanga iliyobeba ubingwa ilivaana na Coastal Union ambayo safari hii imeitoa hatua ya 32 Bora.

BAT 01

Yanga imepenya fainali kwa kuifunga JKT Tanzania katika nusu fainali iliyopigwa Mkwakwani jijini Tanga. Siku chache zilizopita zimewashuhudia baadhi ya mastaa wanaokipiga katika ligi mbalimbali duniani wakimiminika nchini kutembelea hifadhi za taifa na vivutio mbalimbali vya utalii baada ya ligi zao kwisha, na sasa wakihitaji muda wa kupumzika, kutuliza akili na kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao.

Msimu huu hadi sasa mastaa wa nje waliofika nchini kutalii ni pamoja na nyota wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania, Pedro Gonzalez maarufu kama Pedri na nyota wa zamani wa Manchester United na AC Milan, Zlatan Ibrahimovic ambao walionekana wakila raha kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Haishangazi kwamba huenda pia wangeenda sehemu zingine pia kama Eneo la Hifadhi la Mamlaka ya Ngorongoro (NCAA) kujionea bonde la ufa, lakini pia Hifadhi ya Taifa Tarangire na hata kuupanda Mlima Kilimanjaro.

Kuona wachezaji wa Kibongo wakitoka nje ya mipaka ya Tanzania wakienda kutembelea miji mikubwa ya utalii ya kihistoria, kupumzika na kuweka akili sawa kwa ajili ya msimu ujao imekuwa ni nadra sana, na hii pia hata kwa hapa nchini ambapo kuna vivutio kibao vya utalii katika kila mkoa Bara na Zanzibar.

BAT 02

Mwaka juzi beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, ndiye aliyesafiri kwenda Dubai kula bata na familia yake, huku Kibu Denis akienda zake Marekani na familia mwaka jana, na aliyekuwa nyota wa Yanga anayekipiga Wydad Casablanca kwa sasa, Stephane Aziz Ki aliwahi kwenda Dubai kupumzika akiwa na mkewe Hamisa Mobetto.


WASIKIE HAWA

Denis Nkane, winga wa Yanga anasema: “Mmmh gharama za huko nitaziweza kweli, labda nikusanye mshahara wangu wa msimu mzima.”

Beki wa Mashujaa, Ibrahim Ame anasema, “kwa upande wangu natamani sana kusafiri kwenda nje, lakini naogopa gharama, hapo sio chini ya milioni 20, hiyo si najenga nyumba kabisa.”

Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Utalii wa Dubai, Amna Bin Hendi anadai Dubai ni moja ya nchi zinazoingiza watalii wengi kwa mwaka kutoka mataifa mbalimbali na kwamba si matajiri tu, bali watu wote wakiwamo wenye uchumi wa kati na makundi maalumu.

BAT 03

Amna anaongeza kuwa kila kitu kipo katika makundi kwani mtu akitaka kutembea sehemu za bei ghali zipo na za bei rahisi pia huku akitoa mfano kwenye malazi zipo hoteli zinazoanzia Dola 40 (takriban Sh86,000) na maeneo ya utalii ambayo mtu anaweza kutumia kati ya Sh 12,500 na 25,000 kufurahi akiwa na familia, ilhali tamaduni za Kibongo na huko kuna mahali zinashabihiana.

Nimeona watu huku wanavaa abaya na kufunika vichwa, ni sawa tu na kule kwetu. Hayo ndio mavazi ya kwetu na kwa wanaume huvaa kanzu,” anasema na kuo-ngeza kwamba hata upande wa vyakula vipo vya aina ya mbalimbali kama biriani na vingine mchanganyiko kwani kuna watu kutoka mataifa zaidi ya 200 duniani.

BAT 04

KUPUMZIKA MBALI

Mwanaspoti liliwahi kufanya mahojiano na meneja wa Tshabalala, Carlos Sylvester ‘Mastermind’ kuhusu safari ya nyota huyo kwenda nje ya nchi mwaka juzi aliyedai kuna faida ya mchezaji kwenda maeneo ya mbali kupumzika baada ya msimu kumalizika.

“Ni nzuri sana kwa mchezaji kwenda nje ya mazingira yake aliyoyazoea, inasaidia kwa afya ya mchezaji kiakili na kurudisha morali ya kupambana. Anaweza kwenda labda Mwanza au hata Arusha, lakini maeneo yale yakamkumbusha matukio ya maumivu labda alishawahi kusafiri wakapata majanga njiani katika harakati za mpira,” anasema.


Carlos anaongeza kuwa safari hizo husaidia kutengeneza au kuongeza thamani ya mchezaji kwani, “mpira siku hizi ni biashara mbali na mpira mchezaji anaweza kupata dili nyingine kujitengenezea thamani, ukiacha mapambano ya dakika 90 pia kujijali kwa kujipongeza ni nzuri zaidi.”

Daktari wa Kagera Sugar, Abel Shindika aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Kitendo cha mchezaji kwenda kutembelea mazingira mapya kwenye macho yake ni tiba kiakili, inamsaidia kutoa vitu kichwani vya kimchezo na kuingiza vipya vitakavyompa taswira ya kujua maisha mengine nje na soka.”

BAT 05

Daktari wa Tanzania Prisons, Damas Chinyile anaongeza kupata mapumziko nje ya mazingira uliyoyazoea husaidia kuimarisha ubunifu na umakini kwani akili huwa mpya na husaidia kujijenga upya kwa seli ambapo huimarisha kinga ya mwili kwani soka ni mpira wa kugongana na wakati mwingine kuanguka.

Mwanasaikolojia Charles Nduki anasema: “Mabadiliko ya mazingira husaidia kupunguza msongo wa mawazo (stress) na kuongeza furaha na utulivu wa akili kwani mazingira mapya huamsha hisia chanya kama furaha, msisimko na matumaini.”