Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Josiah; Kocha mpya aliyeshikilia hatma ya Prisons

Josiah Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo kongwe nchini katika michezo 16 iliyocheza imevuna pointi 14 na kuwa nafasi ya 13 kwenye msimamo na tayari imeanza mazoezi kujiandaa na mwendelezo wa michuano hiyo.

Tanzania Prisons ni miongoni mwa timu zinazopambana kukwepa kushuka daraja baada ya kutokuwa na mwendelezo mzuri kwenye Ligi Kuu na kuweka presha ndani na nje ya uwanja.

Timu hiyo kongwe nchini katika michezo 16 iliyocheza imevuna pointi 14 na kuwa nafasi ya 13 kwenye msimamo na tayari imeanza mazoezi kujiandaa na mwendelezo wa michuano hiyo.

Hata hivyo Maafande hao walianza msimu na Kocha Mbwana Makata, ambaye alisitishiwa kibarua baada ya mabosi kuona hali si shwari na tayari wamempa kazi Aman Josiah.

Josia mwenye leseni A ya Caf, amejiunga na Wajelajela hao akitokea Geita Gold ya Championship hivyo itakuwa mara yake ya kwanza kuongoza timu ya Ligi Kuu akiwa Kocha Mkuu.


JO 01

Historia yake

Josiah anaanza kuinoa Prisons baada ya mtangulizi wake, Mbwana Makata kufungashiwa virago akiwa na Msaidizi wake Renatus Shija kutokana na matokeo yasiyoridhisha katika Ligi Kuu.

Josiah amejiunga na Maafande hao akitokea Geita Gold ya Championship lakini kabla ya hapo aliitumikia Biashara United na Tunduru Korosho ya First League na kesho Januari 3 ataanza kazi rasmi.

Hata hivyo, kwa muda huo amekuwa na rekodi kadhaa japokuwa hazikuvuma kutokana na maeneo mengine kuwa chini ya makocha wakuu, ikiwamo kupandisha Biashara United.

Katika msimu uliopita akiiongoza Biashara United aliifikisha hatua ya play off ya kupanda Ligi Kuu, lakini matokeo ya jumla ya 2-1 dhidi ya Tabora United yaliinyima nafasi ya kupanda daraja.


JO 05

Yuko tayari kwa kazi

Josiah amesema pamoja na kuwa mara ya kwanza kuongoza timu ya Ligi Kuu, lakini uwezo wake na imani aliyopewa haoni kitu kipya bali ni kujiamini.

“Ni namna nitakavyowatumia wachezaji, bahati nzuri nimeona hata waliokuwa majeruhi wamerejea, sioni kitu kipya kwakuwa nimeaminiwa lazima nifanye kazi.

“Kwa kuwa tupo katika kipindi cha usajili, tayari nimeongea na viongozi kujua wapi tuboreshe kikosi, kwa ujumla matarajio ni kufanya vizuri,” amesema Josiah.

Kocha huyo ameongeza kuwa licha ya muda kutotosha lakini hadi kufikia Machi 1 mwaka huu ligi itakapoendelea atakuwa amepata pakuanzia huku akifurahishwa na mapokezi kikosini.


JO 02

Mastaa wafunguka

Josiah ni kocha ambaye amekuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wengi nchini na hilo linajidhihirisha kwa Tanzania Prisons ambayo wachezaji wake wamefurahishwa na ujio wake huku wakiahidi kumpa ushirikiano.

“Tunamkaribisha kocha mpya. Tunashukuru baadhi ya tuliokuwa majeruhi tumerejea, tunaamini tutafanya vizuri,” amesema beki na nahodha, Salum Kimenya.

JO 04

Naye kipa wa timu hiyo, Edward Mwakyusa amesema hawakuwa na mwanzo mzuri, lakini kwa muda huu ligi imesimama watajifua vyema kuhakikisha wanarejesha heshima.

“Mashabiki wawe na matarajio makubwa, tutatumia vyema muda huu kujifua ili kupata matokeo mazuri mzunguko wa pili, hatujakata tamaa na morali ipo juu,” amesema kipa huyo.

JO 03

Uongozi

Kaimu Mtendaji Mkuu wa timu hiyo John Matei amesema matarajio yao mzunguko wa pili ni kusahihisha makosa na kujinasua nafasi za chini kwa usajili watakaoufanya.

“Tutaboresha kikosi, mzunguko wa pili utakuwa wa mafanikio kwetu, tutajitahidi kutekeleza ripoti ya benchi la ufundi kwakuwa tunao majeruhi wengi ambao lazima tuwe na mbadala wao” amesema Kigogo huyo.