Prime
Ibrahim Twaha 'Messi' Winga aliyegeuza matatizo kuwa fursa, anasubiri simu ya Diamond, Zuchu

Muktasari:
- Maje
MAUMIVU na nyakati ngumu alizowahi kuzipitia winga wa zamani wa Simba na Coastal Union, Ibrahim Twaha 'Messi' zilimbadilisha mtazamo wake na sasa amekuwa msaada kwa wachezaji wenzake kuhakikisha hawakatizi ndoto zao.
Majeraha yalikatisha ndoto zake za kufika mbali katika soka na kutokana na hayo, akapata wazo la kufanya kitu kingine cha kuwasaidia wanasoka na watu wengine ili afya zao kuwa bora.
Katika mahojiano yake na Mwanaspoti, anasema pamoja na ugumu anaoweza kupata mtu anapopitia nyakati mbaya, anashauri ziwe za kufanya utafiti wa kurejea na jibu litakalompa hatua zaidi.
"Nakumbuka kuna kipindi nilivunjika mguu nikawekwa hogo, nilikaa wiki moja tu nikalitoa mwenyewe kwani nilianza kujifanyia utafiti mwenyewe, niliporudi hospitali nikaambiwa nipo sawa, natakiwa kuanza mazoezi ya taratibu," anasema Messi.
COPA COCA COLA HADI LIGI KUU
Simba ilimsajili Messi kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miaka miwili mwaka 2012 hadi 2014. Alicheza mechi 30 za Ligi Kuu, kabla ya kuumia na hakuwahi kurejea katika ufiti, jambo lililomtoa katika mstari wa kuzipigania ndoto zake za soka.
"Nilianza kucheza Ligi Kuu nikiwa mdogo msimu 2011/12 Coastal Union, kipindi hicho nilikuwa nasoma kidato cha tatu, viongozi wa timu hiyo waliniona katika mashindano ya Copa Coca-Cola," anasema Messi na kuongeza;
SAMATTA AMPELEKA SIMBA
"Kiwango nilichokionyesha Coastal kilizivutia Yanga, Azam FC na Simba, lakini nilishauriwa na Mbwana Samatta kipindi hicho anacheza TP Mazembe aliniambia nikipigiwa simu na Zacharia Hans Poppe (marehemu) nisijiulize mara mbili kusaini, mwingine alikuwa kocha Hemed Suleiman 'Morocco' aliyeniambia ni timu inayowapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao."
AIKOSA YANGA
Anakumbuka ilikuwa Oktoba 10, mwaka 2012, walikuwa wanafanya mazoezi Bamba Beach ya kujiandaa kucheza dhidi ya Yanga siku inayofuata, aliumia bila kuguswa na mtu baada ya kupokea mpira kutoka kwa kipa Abel Dhaira raia wa Uganda ambaye kwa sasa ni marehemu.
"Tulikuwa tunafanya mazoezi ya kufunga ilipofika zamu yangu Dhaira alinirushia mpira baada ya kuudaka kwa mikono nikajisikia maumivu makali ya miguu, nikashindwa kabisa kusimama kila mtu akabaki anashangaa nini kimetokea," anasema Messi na kuongeza;
"Nilikuwa nimepangwa kucheza kikosi cha kwanza dhidi ya Yanga, hivyo viongozi wa Simba wakawa wanalazimisha nicheze hiyo mechi, wakaagiza dawa ili nichomwe sindano za kutuliza maumivu, kambini chumba nilichokuwa nalala kilikuwa karibu na Dhaira na Joseph Owino waliniambia bado ni mdogo nisikubali kuchomwa sindano.
AOMBA KUONDOKA SIMBA
"Viongozi wa Simba walipokuja na daktari nikakataa kuchomwa sindano nikawaomba nipate muda wa kujiuguza, sasa nikawa nimekaa nje takribani mwaka mzima bila kucheza, kilikuwa kipindi kigumu kwangu, ikafikia hatua nikaomba niondoke ili nisiwe napokea mshahara ambao sijaufanyia kazi, wakakataa wakataka kuniongezea mkataba mwingine."
Anasema Simba ilileta kocha mpya, Mcroatia Zdravko Logarusic alikuta ripoti ya kocha aliyeondoka ya kuwaondoa wachezaji 13 likiwemo jina lake, kabla ya maamuzi aliwataka awaangalie katika mazoezi.
"Kwa sababu sikuwa fiti nikapewa dakika tano za kufanya mazoezi ajabu kocha Logarusic akanibakiza wenzangu 12 waliondolewa, lakini sikupenda kubaki nilihitaji kurudi Coastal ili nikajitafute upya, aliyenisaidia hilo hadi kuondoka ni Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio'," anasema na kuongeza;
KIPAJI KIMEMBEBA, AGEUKIA MASOMO
"Baada ya kuondoka Simba 2014/15 nikarejea Coastal nikakutana na hali mbaya kiuchumi, nikaondoka na kujiunga na Kagera Sugar msimu wa 2016/17, timu zilizofuata kuzichezea ni Polokwane City ya Afrika Kusini F.C, Fanja ya Oman nikakutana na Mbuyu Twite aliyekuwa anacheza Yanga kisha nikaenda Kenya ambako nilikaa muda mfupi nikarudi Tanzania, timu zote hizo kilichokuwa kinanibeba ni kipaji kwani sikuwa fiti kabisa hivyo msimu wangu wa mwisho kucheza ilikuwa 2017/18."
Anasema mwaka 2019 alijikita kufanya safari za Kenya, ambazo zilimsaidia kusoma na maisha yake kuendelea kama kawaida, ingawa anakiri vipo vitu alivipata kutokana na soka kama magari na mashamba.
SABABU YA KUSOMEA TIBA (THERAPY)
Anasema sababu iliyomshawishi kusomea mambo ya tiba (cupping therapy) ni baada ya kupata majeraha na kutibiwa bure chini ya daktari Gilbert Kigadye, akaona anaweza akafanyika msaada mkubwa kwa wachezaji wenzake.
"Daktari Gilbert hajawahi kucheza soka lakini ana moyo wa pekee wa kuwasaidia wachezaji, nikashawishika kwenda kusoma Uingereza kwa ngazi ya Diploma ambayo nilihitimu mwaka 2022," anasema na kuongeza;
APATA MCHONGO WA 1 MILIONI
"Baada ya kuhitimu nikarejea Tanzania na kuanza kuyafanyia kazi mafunzo, wakati huo huo nilikuwa nacheza soka la mtaani na nilivunjika mguu nikawekwa hogo katika hospitali ya Muhimbili, wakati narudi nyumbani nilimtumia ujumbe Yusuph Bakhresa kumuomba aniajiri katika timu yake niwe kati ya watu wa kuwatibu wachezaji.
"Baada ya dakika kama 20 nikaona ujumbe katika simu wa kuonyesha amekuwa rafiki yangu katika mtandao wa Instagram, hakuishia hapo nikakuta amenijibu na kuhitaji nikamfanyie huduma hiyo, aliuliza vifaa ninavyotumia kwa bahati mbaya simu ikazima chaji, nilivurugwa ikabidi nitafute pakuchaji kisha nikampigia akanielekeza niende nyumbani kwake."
Anasema akamfuata nyumbani kwake akiwa ameongozana na rafiki yake mwanamuziki Jaivah aliyemsaidia kuendesha gari, kwani alikuwa hawezi kutokana na mguu kuwa na hogo.
"Nikiwa njiani nikawa nawaza Yusuf ni mtu mkubwa itakuaje, lakini alifurahia huduma yangu akanipa zaidi ya Sh1 milioni, nikapata nguvu ya kuifanya kazi hiyo kwa bidii na kuhitaji kusoma zaidi," anasema Messi anayejiendeleza kusoma fani hiyo kwa njia ya mtandao na anatarajia kuhitimu ngazi ya shahada (degree) Aprili mwaka huu.
WATU MAARUFU ALIOFANYA NAO KAZI
Anawataja baadhi ya watu maarufu ambao amefanya nao kazi kwa upande wa wanasoka ni Mbwana Samatta, Kelvin John, Bakari Masoud, Said Ndemla, Moses Phiri, Bakari Mwamnyeto, Abdi Banda na Victor Akpan.
"Wasanii wa muziki ambao nimefanya nao kazi na wengine naendelea kufanya nao ni Ali Kiba, Shilole, Marioo, Jaivah, Abbah Music, Mbosso, Chino WanaMan, Ricardo Momo. Pia watu wengine maarufu kama Yussuf Bakhresa (Azam), Said Mtanda (Mkuu wa Mkoa Mwanza) wengine ni wakuu wa wilaya, kifupi hao ni baadhi watu ni wengi sana," anasema.
MALENGO YAKE
Anasema anatamani kampuni yake ya Safari Cupping Therapy iwe kubwa na awe na matawi maeneo mbalimbali, kuhakikisha anawafikia watu kwa urahisi.
"Kwa sasa nafanya kwa oda Ligi Kuu inaposimama nakuwa Dar es Salaam, pia nasafiri kwenda Nairobi, Mombasa na jijini Arusha ninapoishi na familia yangu kwa maana ya wazazi pia mke na watoto wangu, ambako nakutana na viongozi mbalimbali wa serikalini," anasema.
DIAMOND, ZUCHU NI SUALA LA MUDA
Anasema supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alihitaji huduma hiyo ili kinachokwamisha wanapishana ratiba, hivyo anaona ni suala la muda kufanya nao kazi.
"Diamond na Zuchu ni suala la muda, wanaweza wakanitafuta muda mwingine nakuwa nipo Kenya, nikirudi Tanzania na wao wanakuwa wapo na ratiba nyingine, ndiyo maana nasema ni suala la muda," anasema Messi ambaye familia anatokea familia ya kisomi ila hakuwa tayari kuelezea kitu chochote kuihusu mitandaoni.
UCHAWI WA SOKA NI HATARI
Messi anasema uchawi uliopo katika soka unatisha na hausimuliki kutokana na matukio aliyoyashuhudia, lakini hakutaka kutaja mwaka wala timu.
"Kuna siku nilishuhudia anachinjwa paka ili kutengua uchawi wa timu pinzani, siku nyingine kondoo aliandikwa majina ya wachezaji pinzani akazikwa mzima hadi unamuonea huruma, tukio lingine akaja mganga akasema ajitokeze mchezaji jasiri atoe moyo wa kondoo akiwa mzima, hakuna aliyeweza mganga akamtoa kwa kutumia kitu chenye ncha kali akachomoa moyo kondoo aliugulia maumivu hadi akafa akasema nyama yake katupeni porini," anasema na kuongeza;
"Matukio hayo yalinifanya niogope sana, kilichokuwa kinanisaidia nimesoma sana dini na familia yangu ni watu wa Pwani, hivyo wanasoma dua ya vitabu."
LIGI KUU INA MVUTO
Kuhusu anavyoiona Ligi Kuu kwa sasa anasema imeboreshwa na imekuwa na ushindani, unaowavutia wageni wengi kuja kucheza.
"Ningekuwa nacheza hadi sasa hao wachezaji wanaotajwa ni moto wa kuotea mbali nakuhakikishia kocha angepata mtihani wa nani aanze na nani akae benchi kwa timu za Simba na Yanga, ila nampa heshima yake Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa msimu uliopita siyo kazi rahisi," anasema na kuongeza;
"Ukisema namkubali nani katika nafasi yangu kwa sasa siwezi kukutajia kwa sababu hakuna mawinga kama Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Vicent Barnabas ambao walikuwa na mbio za kuwachosha mabeki."
raha yalikatisha ndoto zake za kufika mbali katika soka na kutokana na hayo, akapata wazo la kufanya kitu kingine cha kuwasaidia wanasoka na watu wengine ili afya zao kuwa bora.