Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juni 25 ni Dabi ya ufundi na mbinu zaidi

NONDO Pict

Muktasari:

  • Njia iliyotuvusha ni ya baadhi ya watu kutolewa kafara na mechi kupangiwa Juni 25 mwaka huu kama siku ya kupigwa mtanange huo.

BAADA ya sintofahamu kuhusiana na hatma ya mchezo wa kiporo wa Dabi ya Kariakoo, hatimaye mpira umeshinda kama ilivyokuwa kiu yangu kuona mpira unashinda kwa kutumia njia moja kati ya mbili ambapo upande mmoja kwenye mvutano uumie au watu, au njia ya busara itumike kukubaliana katika wasiyokubaliana nayo, mwisho wa yote mpira uchezwe.

Njia iliyotuvusha ni ya baadhi ya watu kutolewa kafara na mechi kupangiwa Juni 25 mwaka huu kama siku ya kupigwa mtanange huo.

Tukirudi katika mechi yenyewe, nje ya uwanja kuna mambo mengi ya kuvutia. Kwanza ni viwango na hali ya ushindani ndani ya kiwanja kwa timu hizo kila moja ikiamini ina wakati mzuri kuliko nyingine, hata mijadala ya wafuasi wa timu hizi kila upande unahisi ushindi uko upande wao kwa kuangalia vikosi na viwango vya wachezaji na kama timu zote zitawapata kikamilifu mastaa tutarajie mechi bora sana kimbinu na kiufundi kulingana na walimu waliopo.

Tukianza na Simba, mbali na kuwa na kikosi kinachotengenezwa lakini kocha Fadlu Davids amefanikiwa kutengeneza utaratibu mzuri wa timu kujibu maswali yanayoletwa na vipindi vitano vya mchezo kwa maana timu inapokuwa na umiliki wa mpira, timu pinzani inapokuwa na umiliki wa mpira, timu inapopoteza mpira, timu inapopokonya mpira na mipira ya kutenga iwe kushambulia au kuzuia kwa dakika zote tisini, haya ndio matukio yanayojirudiarudia.

NON 01

Muundo wao wa 4-2-3-1 ndio unaowafanya kuwa timu yenye umiliki mkubwa wa mpira kwenye michuano waliyoshiriki msimu huu.

Matarajio kikosi kitakachoanza, langoni atasimama Moussa Camara, beki wa kulia Shomari Kapombe, kushoto Mohammed Hussein, mabeki wa kati Chamou Karaboue na Abdulrazak Hamza, viungo wawili wa kuzuia Yusuf Kagoma na Fabrice Ngoma, viungo watatu wa kushambulia Elie Mpanzu kushoto, Kibu Denis kulia na nyuma ya mshambuliaji ni mbunifu Jean Charles Ahoua, huku mshambuliaji kiongozi akisimama Steven Mukwala. Hiki ndicho kikosi bora cha msimu huu kwa Simba.

Uimara uko eneo la pembeni kwenye kujenga na kushambulia, huko ndiko yanakotengenezwa mabao, lakini ndio maeneo yanayotumika na wapinzani kuwashambulia.

Kwa upande wa Yanga, yenyewe inajivunia timu iliyokaa muda mrefu na ubora ilionao katika kikosi chao huku kocha Miloud Hamdi akitengeneza tafsiri nzuri ya matukio ndani ya uwanja, nikiitazama mechi ya duru la pili la ligi pale Chamazi dhidi ya Azam kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza, zilitosha kulitazama benchi la ufundi kwa jicho la ziada.

NON 02

Kwa muundo wao wa 4-2-3-1 bila uwepo wa Stephane Aziz Ki, bado Yanga ina kikosi bora.

Matarajio ya kikosi cha Yanga, langoni atakuwa Djigui Diara, beki wa kulia Israel Mwenda, kushoto Chadrack Boka, mabeki wa kati Ibrahim Bacca na Dickson Job, viungo wa kuzuia Khalid Aucho na Mudathir Yahya, viungo watatu wa kushambulia kushoto Pacome Zouzoua, kulia Clement Mzize, nyuma ya mshambuliaji Maxi Nzengeli huku mshambuliaji kiongozi akianza Prince Dube, hiki ndicho kikosi chao bora kinachoweza kuitetea nembo yao.

Ukiangalia timu zote zinafanana kwenye muundo wa kujipanga kiwanjani na hata utendaji kazi hasa wakati wa umiliki wa mpira walinzi wa pembeni ndio huipatia timu mapana huku washambuliaji wa pembeni wakiingia ndani kupokea mipira nyuma ya viungo wa kuzuia wa timu pinzani, viungo wawili wa kuzuia mmoja hutumika kuvunja mistari ya ulinzi ya timu pinzani kwa pasi, Simba humtumia ngoma huku Yanga wakimtumia Aucho, ndio maana nasema wanafanana.

NON 03

Vita kubwa itakuwa katikati ya uwanja kujimilikisha eneo hilo ambalo atakayelimiliki ameumiliki mchezo, ushindani mwingine utakuwa maeneo ya pembeni mwa uwanja ambapo ndipo kwenye matukio mengi ya kuamua mchezo.

Simba inategemea ubora wa Kapombe ambaye amekuwa chachu ya utengezaji nafasi za kufunga, huku Mpanzu akitumika kuvuruga utaratibu wa timu pinzani kujilinda kwa uwezo wa kukokota mpira.

Yanga ina Mwenda anayefanya kazi kama Kapombe na Pacome akitumika kama Mpanzu, ndio maana nasisitiza timu zinafanana kwa vingi, kitakachotofautisha ni daraja la mchezaji.

Mzize upande wa kulia simtofautishi sana na Kibu kwenye matumizi na aina yao ya uchezaji, acha siku ifike tufaidi mbinu na ufundi wa wachezaji.

Kagoma kama muhimili wa ulinzi eneo la katikati, Mudathir ni kiranja wa zamu kwenye boksi zote mbili kwenye kuzia na kushambulia ndio uti wa mgongo wa Yanga kwenye kujibu maswali yanayoletwa na mchezo.

NON 04

Eneo la ubunifu Ahoua amejitambulisha kama mchezaji wa kulelewa aliyeshiba mafunzo ya kimbinu na kutafsiri matukio kwa uweledi na ndio muhusika mkuu wa mabao mengi ya timu huku mbele ya wapenda burudani akiacha mijadala ya kuhoji ubora wake ila kwa wanaoutazama mchezo kwa jicho la taaluma wanamuelewa.

Maxi ni bidhaa nyingine kutoka chuo cha mpira ila ikiwa na umtaani mwingi ambao unamfanya kuwa tofauti na wanachuo wenzake, unampata kimbinu lakini wapenzi wa burudani nao hawaondoki bila ya kupata cha kusimulia.

Tukutane Juni 25, mimi naamini itakuwa kati ya Dabi ya Kariakoo bora kimbinu na kiufundi.