Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FRESHI! Walipotezwa wakaitwa tena

MAKOCHA wamekuwa wakitimuliwa kila wakati kutokana na presha kubwa ya kupata matokeo, lakini kuna usemi usemao makocha wanaajiriwa ili kutimuliwa.

Hilo linathibitika kutokana na timuatimua ya makocha inayofanyika katika timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara ikiwa hadi sasa ni makocha sita wameondolewa kwenye timu ambao ni Didier Gomes, Salum Mayanga, Hitimana Thiery, Joseph Omog, Hemed Suleiman ‘Morocco’ na Etienne Ndayiragije.

Kiufundi inafikirisha makocha waliotimuliwa katika timu, lakini baadaye wakarejeshwa tena kuendelea na majukumu yao. Huu ni mchanganyiko wa makocha wa ndani na nje walioondoka ambao Mwanaspoti limebaini uwepo wao ulionekana awali hawafai, ingawa timu ziliona umuhimu wao na kuamua kuwarudisha ya kuongeza nguvu.


CEDRICK KAZE (YANGA)

Kaze alikuwa ndani ya Yanga msimu wa (2020/21) ambapo hakukamilisha mzunguko wa pili baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua kumfungashia virago.

Kwa mujibu wa Yanga ilieleza kuwa Kaze alishindwa kuwapa kile ambacho walikuwa wanakitaka jambo ambalo liliwafanya wafikie makubaliano ya kuachana naye.

Mechi yake ya mwisho alishuhudia vijana wakigawana alama dhidi ya Polisi Tanzania na bao la Yanga lilifungwa na mchezaji Fiston Abdulazak ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi.

Kaze amerudi tena Yanga msimu huu akiwa kocha msaidizi chini ya Nasreddine Nabi


SALUM MAYANGA (MTIBWA SUGAR)

Baada ya kumtema Joseph Omog uongozi wa Mtibwa Sugar umemrudisha kwa mara ya tano kocha Mayanga ambaye ndiye kocha aliyeipa mafanikio timu hiyo tofauti na wengine waliopita kuinoa na Januari 7,2022 ametangazwa kocha mkuu wa Mtibwa Sugar.

Hii ni mara ya pili kwa Kocha Mayanga kuifundisha klabu ya Mtibwa Sugar kama kocha mkuu. Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 2008/09 na 2009/10, 2016/17 na 2017/18 ambapo aliweza kuipatia Mtibwa mafanikio makubwa kwa kuiwezesha kutwaa Kombe la Tusker, Kombe la Mapinduzi na pia kutwaa Ngao ya Jamii.


CHARLES MKWASA (YANGA)

Jina lake maarufu ni ‘Master’ ni kocha mwenye leseni A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) aliyoipata mwaka 2014. Pia ni mkufunzi daraja la kwanza wa CAF tangu wakati huo.

Mkwasa alianza kuifundisha Super Star na Yanga SC kuanzia 1989 hadi 1993, kisha 1994 alifundisha iliyokuwa timu ya Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kwa miaka miwili na kutimkia Oman katika Klabu ya Al Khaboura ya Oman alikodumu hadi 1999.

Alirejea nchini 1999 na kupata kibarua cha kuinoa Tanzania Prisons ya Mbeya ambayo mwaka 1999 aliipa ubingwa wa iliyokuwa Ligi ya Muungano.

Baada ya mafanikio hayo Yanga ilimuajiri kama kocha mkuu mwaka 2001 akimrithi Raoul Shungu kutoka DR Congo.

Baada ya kutua Yanga aliiwezesha kutinga hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini baada ya kufungwa mabao 3-2 ugenini na kutoa sare ya mabao 3-3 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Mwaka 2002 alipewa mkataba wa kuinoa Coastal Union alikodumu kwa msimu mmoja kabla ya mwaka 2003 kurejea Prisons alikodumu hadi 2005 alipohamia Moro United.

Mwaka 2006 akahamia Miembeni ya Zanzibar aliyoipa ubingwa wa Zanzibar na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na mwaka 2008 akawa kocha wa African Lyon kwa msimu mmoja na 2009 akahamia Ruvu Shooting alikodumu hadi 2013 alipokwenda Yanga SC kama msaidizi wa Mholanzi Hans van der Pluijm.

Mwaka 2014 alijiunga na timu ya Al Shoolai ya Saudi Arabia lakini akadumu kwa miezi mitatu tu na kurejea nchini na mwaka huo huo akarejea Yanga kama kocha msaidizi chini ya Pluijm na kuipa Yanga ubingwa.

Mwaka 2019 alirudi Yanga kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera aliyetimuliwa na mwaka huu amejiunga na maafande wa Ruvu Shooting.



ARISTICA CIOABA (AZAM FC)

Msimu wa 2017/18 kikosi cha Azam hakikufanya vizuri msimu huo ambapo kiliondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho (FA) kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mbali na kuondolewa huko, timu hiyo ilimaliza ligi katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 45 huku ikicheza michezo 23.

Azam chini ya Cioaba imecheza jumla ya mechi 12 ndani ya msimu wa 2019/2020 ilishinda mechi nane na kulazimisha sare moja mbele ya JKT Tanzania kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Azam Complex imepoteza mechi tatu ambapo ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri.

Mechi ya pili ilikuwa dhidi ya KMC katika Uwanja wa Uhuru na ya tatu ilikuwa dhidi ya Yanga iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex na zote ilipoteza kwa kufungwa bao mojamoja. Akiwa Azam, Cioaba alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi 50 ambapo alishinda 28, sare 11 na kupoteza 11 msimu wa 2019-20.


JUMA MWAMBUSI (YANGA)

Januari 21, 2021 Mwambusi alijiondoa mwenyewe Yanga baada ya kueleza kuwa ana matatizo ya kiafya anaomba kupumzika ndipo Mwenyekiti wa klabu, Dk Mshindo Msolla akathibitisha kujiuzulu kwa kocha huyo aliyefanya kazi kwa awamu ya pili Yanga baada ya awali kufanya kazi chini ya kocha Mholanzi Hans van der Pluijm na Mzambia George Lwandamina.

Awali, Mwambusi aliwahi kukinoa kikosi hicho akiwa kocha msaidizi chini ya Hans Pluijm na hata walipoondoka walikwenda wote kwenye kikosi cha Azam FC.


ABDUL MINGANGE (NDANDA)

Ni kama familia sasa kwenye timu hiyo alianza kuinoa msimu wa 2017/18 hakumaliza msimu na timu hiyo kutokana na matokeo mabayta na kutimuliwa ndani ya timu hiyo msimu wa 2019/20 aliishusha Ndanda na kuondoka hadi sasa hayupo tena na timu hiyo.


HANS PLUIJM (YANGA)

Pluijm, aliyezaliwa Januari 3 mwaka 1949, alikuwa anafundisha Yanga katika awamu ya pili baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts.

Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari 2015.

Huwezi kutaja mafanikio ya Yanga ya kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo katika miaka ya hivi karibuni bila kumtaja Pluijm. Alianza kushinda msimu wa 2014/15 kabla ya kutwaa tena 2015/16. Zaidi ya VPL Pluijm ndio alikuwa kocha wa kwanza kutwaa kombe la shirikisho (FA) msimu wa 2015/16 akiwa na Yanga.

Alianza vizuri msimu wa 2016/17 akiwa na Yanga kabla ya kuondolewa kwenye nafasi ya ukocha mkuu na kukabidhiwa nafasi ya kuwa mkurugenzi wa ufundi na nafasi yake kuchukuliwa na Mzambia George Lwandamina, lakini hakudumu na nafasi hiyo ambapo aliachana na timu na kuteuliwa rasmi kuwa kocha wa Singida United ambayo imepanda ligi msimu huu wa 2017/18.


WENGINE

Makocha wengine ni Steward Hall John (Azam), Milovan Cirkovic, Patrick Phiri, Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kihwelo (wote Simba).