Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Faida na hasara za mbio za marathoni hizi hapa

KILELE cha mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2023 kilikuwa ni Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Ushirika, mjini Moshi ikishirikisha wakimbiaji toka ndani na nje ya nchi.
Mashindano haya maarufu kimataifa hivi sasa yametimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 yakiwa chini ya Mdhamini Mkuu TBL kupitia bia ya Kilimanjaro Premium  Lager.
Mashindano haya ni moja ya matukio makubwa katika kutangaza utalii wa Tanzania ikiwamo mlima wa kilimanjaro na vivutio vya utalii vya visiwani Zanzibar.
Umaarufu wake ni fursa kwa makumpuni makubwa ya kibiashara kujitangaza kupitizia udhamini ikiwamo Tigo iliyodhamini Kili Half Marathon 2023 mbio za km 21 na Grand Malt mbio za km 5.

Wadhamini wengine ni pamoja na Kilimanjaro Water, Total Energies, Simba Cement na TPC Sugar.
Kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na idara zake iliwakilishwa na Katibu Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Adamu Katundu walishiriki mbio kwa lengo la kutelekeza sera ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Zoezi la kukimbia ndio linashika namba moja duniani kwa kuleta matokeo makubwa kwa afya ya mwili. Ndio maana wakimbiaji wa wanaishi maisha marefu zaidi kwani wanaepukana na unene uliokithiri.
Jicho la kitabibu linatazama zaidi faida za kiafya za mashindano haya ikiwamo uboresha Afya ya Moyo na utimamu wa mwili ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.


MARATHON NI NINI?
Katika historia ya  riadha duniani inaonyesha mwaka 1921 mbio za marathon zilianzishwa shirika la riadha dunia IAAF ikichagua kiwango cha juu cha mbio ndefu kushindaniwa ni km 42.2 .
Umbali huu ulichanguliwa katika mashindano ya mbio zilizofanyika jijini London mwaka 1908. Ingawa pia zikaboreshwa kwa kuweka nusu marathoni km 21 na mbio za chini kabisa kushindaniwa ni km 5.
Marathon huwa na maana ya kukimbia mbio ndefu kwa kushindana au ushiriki jukumu au kazi ngumu katika tamasha maalum au tukio maalum au shindano maalum kama ilivyokuwa kwa Kili Marathoni.
Kwa kawaida mshiriki wakawaida anahitaji kufanya maandalizi ya muda mrefu kujiweka fiti ili kushiriki kwa ufanisi. Hivyo wakati wa maandalizi ndipo mshiriki anapopata faida za kiafya za kufanya mazoezi hayo.


FAIDA ZAKE NI HIZI
Moja ya faida kubwa wanayopata washiriki ambao wengine huwa ni wanariadha na wapenda riadha ambao hujiandaa kama ni ajira yao kama ilivyo kwa wanariadha wakulipwa.
Hapa ndio wanapopata utimamu wa mwili hatimaye kuwaepusha na unene ambao ni kihatarisha cha kupata agonjwa yasiambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, shinikizo la juu la damu, kiharusi, saratani na ugonjwa sugu wa figo.
Magonjwa haya yanatokana na mienendo na mitindo mibaya ikiwamo kutoushughulisha mwili na mazoezi au kazi zinazoushughulisha mwili, ulaji holela wa vyakula, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.
Mbio hizi zinaleta hamasa kwa jamii kujenga tamaduni za kufanya mazoezi au kushiriki michezo ili kuufanya mwili kuwa timamu hatimaye kuepukana na unene ambao ndio chanzo cha magonjwa hayo ambayo ni mzigo kwa jamii na serikali kwani ni gharama kuyatibu.
Kushiriki tamasha kama hili lenye mkusanyiko wa watu wengi inakupa hamasa ya kukimbia umbali mrefu kwa haraka hata uwezo wako ni mdogo au umechoka.
Tafiti za sayansi ya tiba zinaonyesha kuwa ushiriki wa mazoezi wa makundi kama ya tamasha hili huongeza ari ya mshiriki hatimaye kuweza kukimbia zaidi kwa haraka.
Unapojichanganya katika mashindano kama haya kunakupa fursa za kujifunza na kupiga hatua kwani hapa utakutana na watu mbalimbali wenye ufahamu wa mambo kama ulaji wa vyakula ili kukabiliana na unene, mazoezi ya kupunguza mwili na njia za kujikinga na magonjwa.
Mbio hizo zinaboresha afya ya akili na kukupa utulivu wa kimwili kwani mashindano haya pia ni burudani na vile vile kuna burudani ya mziki na vinywaji.
Pia kukutana na marafiki wapya na kubadilishana mawazo mbalimbali ni fursa pia ya kupeperusha mawazo yanayoleta hisia hasi zinazoteteresha afya ya akili.
Mazoezi haya yanawezesha kuchangamana kijamii na wengine ikiwamo wale mnaofanya nao kazi hivyo kuleta mshikamano madhubuti katika eneo la kazi hatimaye kuleta hisia chanya ambayo ni faida kwa akili.


HASARA ZA MARATHONI
Faida ya mbio kama hizi ni kubwa kuliko hasara chache zinazoweza kumpata mshiriki ndio maana serikali imeendelea kuunga mkono tamasha hili.
Hasara ya kwanza ni unywaji wa pombe kupitiliza, hii inaweza kuchangiwa na furaha iliyopitiliza na kukutana na marafiki au jamaa wengine huku kukiwa punguza la bei za pombe.
Ni kawaida kwa baadhi ya washiriki kujiachia na kubugia kinywaji kwa muda mrefu hatimaye kesho yake kupata mning’inio kutokana na jana yake kukesha na kunywa pombe kupita kiasi.
Mning’inio unaweza kuambatana na kichwa kuuma, uchovu, kichefuchefu, kutapika, kukosa utulivu, mapigo ya moyo kuwa juu, kutoka jasho, hofu, maumivu ya tumbo na kutopatana na mwanga.
Mkusanyika wa watu wengi kama vile na aina ya mavazi wanayovaa baadhi ya washiriki inaweza kuleta vishawishi hatimaye kuingia katika mahusiano kirahisi na kujamiana bila kinga.
Mahusiano kama haya ya ghafla yanaweza kuwa chanzo cha watu kupata maambukizi ya VVU kirahisi.
Hatari ya kupata magonjwa ya matumbo kwa wageni ikiwamo food poison, hii inatokana na watu kujichanganya maeneo mengine ambayo uandaaji wa vyakula haukuzingatia kanuni za afya.
Hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa hewa kirahisi ikiwamo mafua makali. Ikumbukwe mwezi uliopita visa vya mafua katika maeneo ya pwani viliongezeka.
Ni kawaida kwa washiriki kupata uchovu mkali wa mwili au kujijeruhi ndani kwa ndani kwani baadhi wanakuwa wametumia nguvu kupita kiasi hivyo misuli kujeruhiwa hatimaye kubana au kukakamaa na pia kujijeruhi kwa kujikwaa au kudondoka.


USHAURI
Katika marathoni hii tahadhari za kiafya huwekwa wazi, vizuri washiriki kushikamana na njia zote za kujikinga na magonjwa zinazotolewa na wataalam wa Afya.
Angalau kujiandaa miezi mitatu kabla kwa kufanya mazoezi mepesi dakika 30-60 kwa siku katika siku 5 za wiki ili kuwa timamu. Vile vile pasha viungo moto kabla ya kuanza mbio  hii inasaidia kupunguza hatari ya kupata majeraha yasiyo na lazima.
Njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ni rahisi, magonjwa haya yanapompata mtu ni gharama kuyatibu hivyo ni muhimu jamii kushikama na mazoezi na kushiriki michezo kama njia ya kujikinga.
Serikali chini ya wizara ya afya iendelee kushirikiana na wadau wa marathoni ili kutumia fursa hizi kuhamasisha na kuelimisha kuhusu magojwa yasiyoambukiza na umuhimu wa mazoezi.