Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EXCLUSIVE… Alphonce Modest: Niitieni MO kabla sijafa #3

Modest Pict
Modest Pict

Muktasari:

  • Leo anaendele kueleza nini anachotaka kwa sasa na kipi anachotamani afanyiwe kwa kuamini kitamsaidia, ikiwamo kuomba bilionea wa Simba, Mohamed 'Mo' Dewji amtembelee kabla hajaaga dunia. Ebu endelea naye kujua zaidi...!

KATIKA sehemu ya pili ya makala haya ya beki wa zamani Alphonce Modest yaliyotokana na mahojiano maalumu aliyeofanyiwa akiwa nyuumbani kwao mjini Kigoma, nyota huyo aliyewahi kutamba na Pamba, Simba, Yanga na Mtibwa Sugar alisimulia jinsi alivyoanza kuugua, kupata ulemavu, kisha maisha yake kuhamia kitandani.

Leo anaendele kueleza nini anachotaka kwa sasa na kipi anachotamani afanyiwe kwa kuamini kitamsaidia, ikiwamo kuomba bilionea wa Simba, Mohamed 'Mo' Dewji amtembelee kabla hajaaga dunia. Ebu endelea naye kujua zaidi...!


ANACHOTAKA

Modest anasema anahitaji madaktari wa kumfanyia mazoezi ya viungo kwani kuna wakati misuli inakaza na kumsababishia maumivu makali yanayofanya ashindwe kuzungumza kabisa.

Kinachomuumiza zaidi hata akisikia maumivu mikono yake haiwezi kushika popote, wala miguu kutembea anajikuta akiishia kulia na kusubiri hadi maumivu yapoe.

“Kuna wakati natamani mikono yangu ingekuwa na nguvu ama ingekuwa inafanya kazi, kwamba naweza kushika panaponiuma. Naishia tu kupata maumivu ambayo hayaelezeki.

Anaongeza kuwa, ”natamani siku moja itokee niweze kutoka nje nione jua kama wenzangu wanavyoliona. Natamani mikono ikae sawa niweze kula mwenyewe kuliko ninavyolishwa kila siku na ndugu zangu.

“Nikipata madaktari wa kunifanyia mazoezi ya mwili nitajihisi mwepesi zaidi tofauti na ninavyojisikia kwa sasa.

“Sitaki kuwasumbua kabisa watu. Ninachoomba nisaidiwe kupata NSSF yangu. Baada ya kustaafu soka nilikuwa nafanya kazi katika kiwanda cha Mtibwa Sugar, ingawa nilikuwa napokea kiasi kidogo. Nikafanikiwa kupata pesa hiyo itanisaidia, kwa maana hata ya kupata matibabu.”

Anasema kama baba wa watoto watatu anajisikia vibaya kuona hawezi kuwajibika kwa wanawe na anajiona kabakia kuwa baba kwa jina

“Ndio maana nikipata kiasi kilichopo NSSF angalau nitaweza kuangalia namna gani ya kuwasaidia (watoto). Mfano nina binti yangu anaitwa Vicky ambaye nilizaa mapema kabla ya kuoa angalau nije nimpe mtaji.”

Anasema anatamani kupata mawasiliano na meneja wa kiwanda cha Mtibwa kupitia Mwanaspoti, amsaidie kuona anaweza akapataje NSSF yake.

“Tulikuwa kwenye mchakato wa kwenda kuapa mahakamani ambapo mzee wangu ndiye alikuwa anafuatilia hilo. Kutokana na mlolongo wake kuwa mrefu, mzee akachoka.”


ANATAMANI AZUNGUMZE NA MO DEWJI

Modest anafurahia ugeni wa Mwanaspoti kuona unakwenda kutimiza ndoto yake kubwa ya kupata nafasi ya kuzungumza na mfadhili wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’, ingawa anachotaka kumwambia ni siri yake hakutaka kukiweka wazi.

“Natamani nipate nafasi ya kuzungumza na MO nikiwa hai, ila kutokana na mikono yangu kutoshika chochote na sina simu kupitia gazeti hili naamini anaweza akaona mwenyewe ama walio karibu naye wakamwambia ombi langu.”

Anasema: “Ikiwezekana naomba uende ofisini kwake umwambie namhitaji zaidi nizungumze naye. MO ni msikivu, ana roho ya kibinadamu naamini atakusikia na atanipa nafasi ya kuzungumza naye, angali nipo hai.”

Mwanaspoti linapomuuliza nje na kutaka kuzungumza na MO anataka Watanzania wamsaidie kitu gani? Anajibu, “sitaki kuwachosha ndio maana miaka 14 ya kuumwa kwangu hujawahi kunisikia mitandaoni wala popote.

Sitapenda kutukanwa, wengi hawajui nilichopitia nyuma ya pazia. Ninachosubiri ni kazi ya Mungu itimie juu ya maisha yangu.”

Tulipomuuliza swali lingine ukibahatika kuzungumza na Rais Samia Suluhu utamwambia nini? Akajibu: “Nitamuomba awakumbuke mabinti wanaocheza soka. Nimeona Simba, Yanga zinapocheza kimataifa huwa anatoa pesa za bao. Ili kuzipa moyo, namuomba afanye hivyo kwa mabinti ambao soka ni kazi yao.

“Unaona ninachokipitia mfano akipitia wachezaji wa kike ambao hawapati pesa nyingi kama wanaume je watakuwa na hali gani. Mmi ni baba nina watoto wa kike ndio maana nawaza mbali sitaki kuwa mbinafsi, kwanza sitaki kumsumbua Rais Samia ana majukumu mengi ya nchi.”


MIKASA

Modest alikuwa na nyumba mbili Dar es Salaam wakati anaanza kuugua aliyekuwa mkewe na kubahatika kuzaa naye watoto wawili, lakini anasema  mwanamke huyo alimshauri wauze ili wapate pesa za matibabu na kilichofuata hakutaka kufafanua sana, badala yake akarudia kauli yake kuwa kuna wanawake ni wakatili sana.

“Siwezi kusema sana eneo hilo kwa sababu nina watoto naye wawili Kelvin na Rachael. Hivyo acha hilo libaki ndani ya moyo wangu, labda ninachotamani kingine angalau niwaone wanangu ambao tangu walipoondoka na mama yao sijawahi kuwatia machoni,” anasema mkongwe huyo.

“Nilichojifunza kabla sijapata umarufu nikiwa bado Kigoma nilikuwa na dada ambaye alikuwa ananipenda sana. Sikuwahi kumpa hata sumni, nikaenda mjini nikapata vinavyong’ara ila mwisho wa siku nikapigwa tukio.

“Ajabu yule mwanamke ambaye sikuwahi kumjali alizalishwa mtoto mmoja na mwanaume mwingine lakini hajaolewa. Ndiye anayekuja kunisaidia, kunijulia hali kuna muda aliomba akaniuguzie nyumbani kwake maana amefanikiwa kujenga. Nilikataa kwa sababu sikuwahi kumtunza, hata ndugu zake wataniona mtu wa hovyo kabisa. Nilimuomba msamaha sana, aliniambia alishanisamehe na moyo wake una huruma na mimi ndio maana anataka akaniuguze.”

Kutokana na mkasa huo anawashauri watu maarufu kutambua kuwa baadhi ya wanawake wanaokutana nao kwa sasa asilimia kubwa wanafuata pesa na kujulikana kwao, wala hawana mapenzi ya dhati.

“Kwa mfano wachezaji waige alichokifanya  staa wa Al Nassr, Msenegali Sadio Mane ambaye wakati anavuma sana hakutaka kuoa, amekuja kuoa kipindi hiki tena binti wa kijijini kwao. Wale ambao wana watu wao walioanza nao chini basi wasiwapuuze, maana wakilia machozi ya kweli yanaweza yakageuka laana katika mahusiano yao mengine. Mastaa wengi wana vilio vya mapenzi baada ya umarufu wao kupungua.”

Jambo lingine analoona linavunja mahusiano ya wachezaji ni umbali na majukumu ya kutotulia nyumbani

“Unapomlisha vizuri mwanamke chakula kinafanya kazi unategemea anapohitaji tendo la ndoa atalipata wapi kama muda mwingi hushindi naye. Umempendezesha, lakini huna muda wa kukaa naye karibu anajikuta anaingia kwenye mahusiano na masharobaro wanaoshinda dirishani kwako wanaangalia tv, kisha wanamtamani anaanza kukuchiti nao, mahusiano ya mastaa ni magumu sana,” anasema.

Kitu kingine anachotaka wachezaji wakifanye ni kujua kutofautisha ushikaji na familia zao ili kuepuka kuchukuliana wanawake na kujenga visa ama visasi.

“Ni kweli kuna urafiki ule ambao mnaweza mkawa kama ndugu, ila kuna maisha mengine ya wachezaji kuzoeana sana kwenye familia mwisho wanaanza kuchukuliana wanawake. Jambo la kufanya wanaweza wakajiepusha kwa kuweka kando ushikaji na ndoa,” anasema mchezaji huyo.

“Chunguza asilimia kubwa ya mastaa wengi ndoa zao zinawasumbua ama wanawake walioanza nao mwanzo hawapo nao, halafu wamebaki na wachuna pesa, wakizipata wanasepa.”

Unajua alichokisema baba yake mzazi wa nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania? Usikose itaendelea...