Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CARLOS KAISER: Tapeli aliyewaletea wachezaji wenzake mademu warembo #2

TAPELI Pict
TAPELI Pict

Muktasari:

  • KAISER alikuwa akichukua wanawake kutoka klabu kisha akawapeleka hadi katika hoteli ya timu ambako taa huzimwa, kisha aliwagawa wanawake hao kwa wachezaji wenzake ambao aliwaruhusu kutumia chumba chake kwa ajili ya kunywa na kufanya starehe nyingine.

KATIKA sehemu ya kwanza ya visa tuliona visa mbalimbali vya Carlos Henrique Raposo maarufu kama Carlos Kaiser ambaye aliwahi kuwa mchezaji mpira kwa zaidi ya miaka 20, akisajiliwa na timu za mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Mexico, Ufaransa na hata kwao Brazil ambazo alisaini nazo, lakini hakuwahi kucheza hata mechi moja katika kipindi chote hicho kwa visingizio mbalimbali.

Kaiser alikuwa mtu wa ‘saundi’ ile mbaya, ukikubali kumsikiliza tu umeingia mkenge na ndicho alichofanya kwa kujiweka karibu na mastaa wakubwa na marais wa klabu mbalimbali ambao ‘aliwajaza’ kwa maneno na sifa za uongo na wakawa wakimpa dili. Na wachezaji wenzake walimpenda kwa sababu alikuwa akijitolea kubeba lawama pale mambo yalipoenda ovyo klabuni na pia alikuwa akiwaletea wanawake warembo. Sasa endelea...  

KAISER alikuwa akichukua wanawake kutoka klabu kisha akawapeleka hadi katika hoteli ya timu ambako taa huzimwa, kisha aliwagawa wanawake hao kwa wachezaji wenzake ambao aliwaruhusu kutumia chumba chake kwa ajili ya kunywa na kufanya starehe nyingine.

“Nilikuwa nikiwatafutia wanawake. Na si wanawake wachache tu, bali wanawake wengi, na warembo zaidi.â€

Matokeo ya hili alilokuwa analifanya yalikuwa ni chanya sana kwani ndio walikuwa wakizuia asivunjiwe mkataba katika timu.

Alisema:”Kila wakati rais wa klabu alipotaka kuniondoa, wachezaji wangejikusanya na kuwaomba wasifanye hivyo kwa sababu nilileta thamani kubwa kwa timu. Nilikuwa naunganisha kikosi pamoja.”


TP01
TP01

SABABU, MWISHO WAKE

Katika mahojiano yake maalumu yaliyopewa jina la ‘Kaiser: The Greatest Footballer Never To Play Football’, Kaiser ambaye alikulia katika mitaa ya favelas huko Botafogo, alisema alijifunza tangu akiwa mdogo kwamba alitakiwa kutumia zaidi akili yake ili kuishi.

“Mimi ni mfano wa mtu ambaye ameishi kwa kutumia ujanja na nguvu ya mapenzi. Unapozaliwa kwenye familia maskini Brazil, kuna njia tatu za kupata heshima, lazima uwe mzuri katika mpira wa miguu, uwe mzuri katika mapigano, au uwe mzuri kwa wanawake.” 

Mpira wa miguu ulikuwa njia ya Kaiser kutoka katika umaskini, hata hivyo ilipofikia miaka ya  1980, teknelojia ilikuwa zaidi na ikawa ngumu tena kufanya hicho alichokuwa anakifanya.

Baada ya miaka mingi ya ulaghai ndani na nje ya Brazil aliamua kuachana na soka na kazi yake nyingine ikawa ni kushawishi wanawake kumpa pesa kutokana na ustaa wake.

Alifanya kazi hiyo kwa muda na sasa staa huyu anafundisha mazoezi ambayo ni kwa wanawake tu na hadi leo bado anawasimulia stori zake.


TP02
TP02

KARIBU KUKAMATWA

Ulaghai maarufu na hatari zaidi wa Kaiser aliowahi kuufanya ulitokea wakati anaitumikia timu ya Bangu, klabu ndogo iliyopo eneo la Magharibi ambayo ni  sehemu yenye heshima kubwa katika soka la Brazil kwani ndiko ilikochezwa mechi ya kwanza ya mpira wa miguu nchini Brazil.

TP05
TP05

Mwaka  1985, Bangu walikosa kushinda kombe la Ligi Kuu Brazil(Campeonato Carioca) kwa penalti,  mafanikio ambayo yangekuwa na alama kubwa kwani haikuwa timu tishio na ilifanikiwa kushangaza watu wengi msimu huo, hadithi yao inafanana na ile ya Leicester ya mwaka 2015.

Wakati huo Bangu, ilimilikiwa na Castor de Andrade, ambaye alikuwa ndio bosi wa michezo ya kamari Brazil na alikuwa na utajiri wa kutosha na alikuwa rafiki mkubwa wa aliyewahi kuwa rais wa Fifa  Joao Havelange.

Castor alikuwa mtu hatari na mafia. Kuna wakati baada ya mechi moja aliwahi kumfukuza mwamuzi akiwa na bastola kiunoni.

Hata hivyo, aliingia katika mtego wa Kasier na akamsaini, kichwa cha habari cha moja ya magazeti ya wakati huo kiliandika: “BANGU IMEPATA MFALME WAKE”, usajili wake ulivuma sana.

Alipofika katika timu kwa mara ya kwanza aliendelea kuwaambia kwamba ana majeraha kama kwaida yake.

Rais wa timu, Castor alimpenda sana Kaiser kutokana na ujasiri wake, namna anavyoshirikiana na wenzake na anavyokubalika na wanawake.

Alipenda tabia ya Kaiser kiasi kwamba alitamani sana kuona muda wote akicheza mpira kiwanjani jambo ambalo hakuwahi kuliona.

 Mwishoni mwa juma, Kaiser alikuwa akifanya mazoezi ya kurudisha utimamu wa mwili, ilikuwa ni mida ya saa nne asubuhi, akapokea taarifa kwamba rais wa timu amesema anataka kumuona katika benchi siku inayofuata.  Kaiser alishtuka sana na kuanza kulalamika kwamba hakuwa amepona sawasawa.

Kocha wake akamtuliza na kumwambia kuwa hatocheza bali atakuwa tu katika benchi.

TP04
TP04

Bangu ilianza mchezo vibaya na ikawa inaongozwa kwa mabao 2-0. Castor alituma ujumbe kwa kocha kwamba ni wakati wa kumtumia mchezaji nyota ambaye ni  Kaiser.

Hadi kufikia wakati huo Kaiser  alikuwa na chaguzi mbili. Angeweza kuingia uwanani jambo ambalo hakutaka kabisa litokee na njia yapili ilikuwa ni kukataa  kuingia, na angefanya hivyo, alikuwa amekwisha kwani angemkasirisha sana Castor ambaye alikuwa akiogopeka.

Hivyo Kaiser alipata njia ya tatu. Wakati akiendelea kufanya mazoezi, Kaiser alisikia shabiki wa timu pinzani akimuita jina la kumkejeli, hivyo akatumia  hiyo kama kisingizio cha kuanzisha ugomvi na mashabiki wa timu ya ugenini. Aliondolewa uwanjani kabla ya kuingia. 

Kaiser alialikwa kumwona Castor baada ya mchezo na kuulizwa kwanini alifanya hivyo, akajibu:”Mungu amewachukua wazazi wangu wote lakini alinipa baba mwingine ambaye ni wewe na walikuwa wanakushtumu kama muongo. Hivyo nilipandwa na hasira na kwenda kuwavaa. Lakini usijali kwa sababu mkataba wangu unamalizika ndani ya wiki moja, hivyo nitaondoka ikiwa umechukia.”baada ya maneno hayo rais wa timu,  Castor aliongeza mshahara na mkataba kwa pamoja.

Haya ndio yalikuwa maisha yake na ilikuwa ngumu kumkamata ingawa hii ilikuwa karibu zaidi kumuumbua.


TP03
TP03

ALICHOJUA NI WANAWAKE TU

Mara tu aliposainiwa na timu, Kaiser alitumia umaarufu wake kuishi maisha ya sherehe na katika mahojiano yake alithibitisha kuwa amewahi kukutana na wanawake karibia 1,000. 

Alijifanya hata kuwa rafiki yake na mchezaji mwenzake wa Brazil, Luis Carlos Toffoli ‘Gaucho’, akiwaonyesha wanawake video za staa huyo  akifunga magoli na kusema kwamba alikuwa ni yeye. 

“Kila usiku nilikuwa katika vilabu vya usiku hadi asubuhi, kutoka Jumatatu hadi Jumatatu. Kwa kweli, sikuwa kamwe katika hali nzuri ya kufundishwa au kucheza asubuhi mpira asubuhi,” alisema Kaiser. 

“Nilihakikisha kwamba nakuwa karibu  na wachezaji wakubwa wa mpira wa miguu wa Brazil. Kuwa mchezaji wa mpira wa miguu kulinifanya kuwa kivutio kwa wanawake.  Ningeweza kulala na wanawake angalau watatu kwa siku.”