Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KIJIWE CHA SALIM SAIDI SALIM: Bird Kinara wa kupiga KO

NDONDI ni kati ya michezo iliyopata umaarufu miaka mingi iliyopita na kupendwa na wazee na vijana.

Kwa miaka nenda miaka rudi mchezo huu umeshuhudiwa wapiganaji wazuri na waliopata umaarufu mkubwa ambao wamekuwa sehemu muhimu ya historia ya mchezo huu duniani.

Kwa kizazi cha hivi sasa na hata kwa watu wengi wa kizazi kilichowatangulia na ambao bado wanapumua, wapo wapiganaji masumbwi ambao pale panapokuwapo simulizi za wapiganaji wazuri wa zamani huwa hawatajwi.

Watu wanaofuatilia sana mchezo huu mara nyingi huwasimulia kwa urefu wapiganaji wa miaka ya 1960 hadi mwishoni mwa karne iliyopita.

Miongoni mwa wanandondi hawa ni Muhammad Ali, Mike Tyson, Floyd Patterson, Joe Luis, Rocky Marciano, George Chuvalo, Sugar Ray na wale ambao walitamba miaka ya hivi karibuni na wale ambao wanang’ara hivi sasa.

Sheria, taratibu na namna ambavyo mashindano ya ndondi yanavyoendeshwa na staili za wapiganaji vimepitia mabadiliko mengi, zaidi ni yale ya kujitahidi kukinga wapiganaji kupoteza maisha kwenye ulingo au kupata madhara makubwa ya kimwili au akili kwenye ulingo wa ndondi.

Mchezo huu umeshuhudiwa rekodi za aina nyingi za mafanikio, wapiganaji wenye uzito mkubwa zaidi na wale dhaifu sana waliowapiga waliowazidi kwa tambo, warefu mithili ya twiga na wafupi sana kama mbilikimo wa msitu wa Congo, wnandondi waliopigana wakiwa na umri mkubwa sana au mdogo kama wa wanafunzi wa sekondari na aina nyingine za rekodi.

Katika kila orodha ya wanandondi wa aina hii inayotolewa kila mwaka huwa halikosi kuwamo jina la mpiganaji maarufu wa zamani wa Uingereza, Billy Bird.

Hata hivyo, kutokana na waandishi wengi wa michezo wa sasa kutojua habari zake, huoni akielezewa alivyotamba katika ulingo na hata kusababisha vijana wengi walioonyesha ubabe mitaani zamani kubandikwa jina lake.

Billy Bird alizaliwa Chelsea, England Januari mosi, 1899 na hadi alipostaafu kupigana ndondi alikuwa ameshiriki mapambano 356 katika kipindi cha miaka 28 cha kupigana ndondi.

Mwanandondi huyu ndiye kwa sasa anayeshikilia rekodi ya dunia ya mashindano ya ndondi za kulipwa ya kufaulu mashindano mengi zaidi kwa kupata ushindi kwa njia ya kuwatoa wapinzani wake nje ya ulingo kabla ya kumalizika muda uliopangwa kwa huo mchezo.

Aliingia kwenye ulingo wa mashindano ya ndondi mara 356 na ni wapiganaji wachache waliokubali kurudia kupambana naye. Baadhi yao walisema walikataa kwa sababu hawakuwa tayari kupoteza maisha mapema ndani ya mikono ya huyu jamaa asiyekuwa na huruma.
Rekodi yake ya ushindi wa mapema (KO) ni wa mapambano 132 aliyoyacheza kati ya mwaka 1936 hadi 1963.

Mwanandondi anayemfuata kwa mafanikio ya kushinda mashindano mengi kwa kumtoa mapema mpinzani wake nje ya ulingo (KO) ni Archie Moore ambaye aliyepigana kutoka 1935 hadi 1963 na kushinda KO 132. Moore ni Mmarekani ambaye alishika ubingwa wa ngumi za uzito wa juu kabisa kwa muda mrefu kuliko mwanandondi mwengine - kutoka Desemba 1952 hadi Mei 1962.
Bird ambaye kutoka 1920 hadi 1948 alipigana katika uzito wa welter alikuwa hana utani sio ndani ya ulingo wa masumbwi tu, bali hata nje. Ni mtu ambaye alikuwa hapendi utani na havumilii kuona mtu anaonewa.

Mpiganaji huyu alikuwa ni dereva wa taxi maarufu katika mji wa Chelsea na pale abiria alipoleta ubishi juu ya malipo aliyodai alimtwanga makonde, kisha akapekua na kufungua pochi na kuchukua malipo yake.

Katika tukio moja la aina hii alimng’oa jino mteja wake na polisi walipomuuliza kwa nini alifanya hivyo jawabu yake ilikuwa muulize kwa nini hakupatana kwanza nauli au kueleza kama alikuwa anataka msaada (lifti).

Polisi walipokuwa wanaendelea kumdadisi alitimua makonde kituoni, alishitakiwa na kulipa faini baada ya kuahidi kumnunulia jino bandia yule mteja wake, lakini akasema isitokee mara ya pili kutaka kutumia taxi yake maana hatokubali upumbavu.

Mara nyingi aliposikia jirani anapenda kumpiga mke wake alifika katika nyumba hiyo kumtaka huyo mwanaume asifanye hivyo na aliporudia jawabu lake ni kwenda kumtia makonde na kumwambia na wewe ni vizuri ukaonja ladha ya kupigwa na aliyekuzidi nguvu.

Bird alipenda kwenda kuangalia mashindano ya ngumi yaliyofanyika London mpaka alipoiaga dunia Februari 6, 1951.

Baadhi ya vijana wa Chelsea mpaka hii leo hupenda kuvaa fulana yenye picha yake akiwa na ndege aliyetawanya mbawa zake akiwa anaruka (Bird kwa Kiingereza ni ndege).