Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasanii wanawake waungana kutoa elimu ya ujasiriamali

Muktasari:

Chama hicho kinachojulikana kwa jina la African Leading Women Impact mpaka sasa imesajili wanachama 50 kutoka katika tasnia ya muziki na filamu.

Dar es Salaam.Wasanii wanawake kutoka katika tasnia tofauti za burudani wameungana na wanawake wengine mashuhuri kutoa elimu ya ujasiriamali.

Chama hicho kinachojulikana kwa jina la African Leading Women Impact mpaka sasa imesajili wanachama 50 kutoka katika tasnia ya muziki na filamu.

Akizungumza leo Februari 4, 2020, katika Hotel ya Protea jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa chama hicho Charity Dadi amesema muunganiko huu utainua wanawake hapa nchini.

"Lengo letu ni kusaidiana wanawake katika nyanja mbalimbali ili kuondoa zana ya kuwa tegemezi ukizingatia wengi wetu wapo katika nafasi zinazoweza kuwawezesha wengine" alisema Charity.

Aliongeza kuwa Machi mwaka huu wanatarajia kufanya kongamano la kukutanisha jamii na wanawake hao miongoni mwa wanachama ni Johari Chaula, Mayasa Mrisho, Tabu Mtingita na Asha Baraka, Zawadi, Husna Maulid, Hidaya Njaidi, Eva Dude, Angella Bondo Witness muimbaji  wa zamani wa kundi la Wakilisha na wengine wengi.