Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugomvi wa Khadija Kopa, Mama Diamond ni hivi

Kopa Pict
Kopa Pict

Muktasari:

  • Tangu mwaka huu uanze kumekuwa na stori ya ndoa ya wawili hao na mara kadhaa mashabiki wamekuwa wakisikilizia kama Mondi amepeleka posa kwa kina Zuchu, lakini mambo yamekuwa yakibadilika na sasa kuibukia kwa wazazi.

TIFUTIFU la Diamond Platnumz na Zuhura 'Zuchu' halipoi.
Baada ya kuzuka mitandaoni kwa stori ya nyota huyo akihusishwa kutoka kimapenzi na dada anayejiita 'Ritah', huku kukiwa na ishu ya ndoa na msanii wake wa WCB, Zuchu, hali imegeuka kwa wazazi watu wakizusha Mama Diamond (Sanura Kassim) na Mama Zuchu, (Khadija Kopa) wana ugomvi.

Tangu mwaka huu uanze kumekuwa na stori ya ndoa ya wawili hao na mara kadhaa mashabiki wamekuwa wakisikilizia kama Mondi amepeleka posa kwa kina Zuchu, lakini mambo yamekuwa yakibadilika na sasa kuibukia kwa wazazi.

Ni hivi. Baada ya kuibuka kwa stori za dada huyo ambaye ni Video Vixion katika wimbo wa Diamond 'My Baby' kumeibua mapya ikiwamo Khadija Kopa kuzushiwa ugomvi na Mama Diamond kutokana na kipande cha sauti kilichozunguka kwenye mitandao ya kijamii.

Katika rekodi hiyo, inasikika sauti ya Kahadija Kopa akimuwakia mtu kwa maneno makali na hivyo wengi kujua ni kumhusu Mama Diamond.

KP 01

Sauti hiyo inasema; "Nimeona huko kwenye mitandao, unasema amefanyiwa nini mwanangu, haya niambie amefanyiwa nini mnafki mkubwa wewe. Kwanza nataka kumjua aliyekuambia hayo maneno na kujua amefanyiwa kitu gani niambie nimuendee uso kwa macho huyo mtu. Nimechoka mimi nataka kuununua huu ugomvi. Tena nitaununua ugomvi kwa bei yeyote ile. Nimechoka kila siku kumsimanga na kumsema mwanangu maneno maneno machafu. Kwa taarifa yenu mwanangu hana dosari yotote ile nimemlea kwa nidhamu na ana heshimu watu wazima na wadogo. Sasa hivi mnataka kumzidi kichwani, nipo hai. Kama vile hana mama mzazi, sasa lolote na liwe, sitakubali."

"We ungekuwa mwanao ungekubali? Mbona wewe una yako kibao na familia yako na huyasemi? Sitaki mumpachike mwanangu maneno maneno na hata huko kwenye lebo yao ya Wasafi kama wamekwambia hawamtaki niambie sasa hivi, basi yuko tayari kutoka muda wowote na pesa zozote watakazotaka tutalipa."

Jambo hilo lilisababisha Mwanaspoti kumsaka Khadija Kopa ili kujua ukweli wa sauti hiyo kama inamuhusu Mama Diamond na mwenyewe anasema hakuna ugomvi unaoendelea baina yao.

Mkali huyo wa miondoko ya Taarabu Bongo amesema sauti hiyo inazunguka ikidaiwa anamzungumzia mwanaye Zuchu kutokana na kile kinachoendelea kwenye mahusiano yake hasa kusemwa na watu kuhusu Diamond na kuzuka kuna ugomvi baina yake na mama Diamond.

"Mimi sina shida na mtu yeyote licha ya uvumi wa kuwa nina ugomvi na Mama Diamond. Sema maneno maneno ya watu ya uzushi  naona ndiyo yanataka tuwe hivyo, lakini sisi wenyewe tunaelewana, yaani mambo ya watoto ndiyo nije kikosana na mtu wakati tunaweza kukaa chini na kuyamaliza kama kuna tatizo? Tafadhali sana watu wasimhusishe mama wa watu na sauti yangu inayosimbaa kumpa makavu mtu," amesema Khadija Kopa.

Amesema watu ndio wanaochochea wao wagombane na ukweli kuhusu zile sauti ni za yeye akimsema mtangazaji mmoja wa kike (anamtaja jina) anayependa kufuatilia mambo ya watu hasa mtoto wake na siyo Mama Dangote kama watu wanavyodhani na alipiga simu kumuuliza habari za Zuchu ndipo akampa makavu.

"Sikia nikwambie, kuna watu  wapo kwa ajili ya uchochezi wa haya maugomvi maugomvi ya watu, wameanza kwa Zuchu na bosi wake Diamond sasa wanakuja kwangu na Mama Diamond, mtu anaweza kukuuliza swali la kimbea tu, yaani halipo kabisa. Analitunga ilimradi apate kwenda kuhadithia kwa watu na sijui napatwa na faida gani. Mimi wanikome na hayo mambo yao, naheshimiana na kila mtu," amesema Khadija Kopa.

KP 02

Amesema amechoka na habari za mtoto wake Zuchu kuzungumziwa kila wakati na kutoa onyo kwa sasa yuko kifua cha mbele kumtetea.

"Mimi ni mzazi na huwa najisikia vibaya sana pale kila kukicha kuona mtoto wangu anazungumziwa vibaya, yaani huwa nasema nivipuuze, lakini sasa naona vinazidi, hivyo naanza kula sahani moja na wale wote wenye kumkosesha raha mtoto wangu, tena natoa tahadhali wamuache mara moja na wasidhani ni yatima yule," alisema Mama Diamond.