Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tessa wa Huba afariki Dunia

Msiba Pict
Msiba Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo mkongwe aliyewahi kutamba na makundi mbalimbali likiwamo la Shirikisho Msanii Afrika lililowika na michezo katika kituo cha ITV, amekumbwa na mauti kwa kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi, japo hayakuwekwa wazi hadi sasa.

MWIGIZAJI nyota aliyekuwa akitamba kupitia tamthilia mbalimbali ikiwamo ya Huba, Grace Mapunda a.k.a Mama Kawele au Tessa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Nyota huyo mkongwe aliyewahi kutamba na makundi mbalimbali likiwamo la Shirikisho Msanii Afrika lililowika na michezo katika kituo cha ITV, amekumbwa na mauti kwa kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi, japo hayakuwekwa wazi hadi sasa.

Taarifa ya kifo cha mkongwe huyo zimetolewa na wasanii wenzake Idriss Sultan na Jimmy Mafufu kwenye mitandao yao ya kijamii.

Idriss Sultan ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiposti picha yake kwamba "Nimechagua kukukumbuka hivi Innallillah wainna illlaihi rajiighun," mwisho wa kunukuu, huku Jimmy Mafufu aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba "Muigizaji kinara mama yetu Grace Mapunda ametwaliwa na Bwana, ni muigizaji namba moja kwa wamama wote nchini , amekuwa mhimili mkubwa kwa tasnia yetu Mungu amemchukua pumzika kwa amani Mama yetu kipenzi."

Msanii mwingine aliyekuwa akiigiza mtoto wa Tessa katika tamthilia ya Huba ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ya kwamba " MAMA huku akiwema Emoj ya picha ya Majonzi, Mwenyezi mungu akusamehe na akujaalie  kile chema kwenye safari yako,

Nilipokuona jana ICU niliumia sana sikuwa na uwezo wakubafilisha hali niliyoiona machoni.kwangu Umenilea ,umenifundisha na leo umeniacha Pendo lako ni kubwa sana kwenye maisha ya tasnia yangu na tasnia kwa ujumla pumzika kwa Aman mama DEV aliandika Rammy Galis aloyeitwa Dev kwenye tamthilia ya Huba huku Grace Mapunda maarufu kama Tessa akiwa mama yake..

Mama Kawele, alianza kuvuma miaka ya mwanzoni mwa 2000 akiwa na kundi la Shirikisho la kutamba na michezo kadhaa ikiwamo Tamu Chungu, lDumaza, Hatia, Gumbizi na mengine akishirikiana na wakali wengine kama Bakar Makuka 'Beka', Richard Mshanga 'Bosi Masinde', Samson, Vailet, Grace Mapunda 'Mama Kawele' na Jaji Khamis 'Kash' ambaye kwa sasa ni marehemu na wengineo.

Enzi za uhai wake, Mama Kawele alijaaliwa watoto wawili, Ritha na Happiness aliyewahi kuigiza naye katika filamu ya Fake Smile, Watoto wake hao pi wanajihusisha na muziki wa kizazi kipya.

Mbali na kuigiza tamthilia, lakini Mama Kawele alikimbiza sana katika filamu na baadhi ya kazi hizo ni House of Death, Hard Price, Nilindiwe, Kichupa, Majuto, Mwaka wa Hasara, Chloroquine love, Chungu ya Nafsi, Poor Minds, Jibu la Ndoto, Back to Life na zinginezo.

Fuatilia hapa kujua taratibu za mazishi za msiba wa mwigizaji huyo mkongwe wa kike nchini.

(Imeandikwa na Johnson James)