Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Naira Marley ashikiliwa na Polisi Nigeria kufuatia kifo cha msanii MohBad

Polisi nchini Nigeria inamshikilia msanii Naira Marley kuhusiana na kifo cha nyota wa muziki wa ‘Afrobeats’ Ilerioluwa Oladimeji Aloba, maarufu MohBad.

Kwa mujibu wa BBC Swahili, msemaji jeshi hilo jijini Lagos, Benjamin Hundeyin amesema kuwa Marley anashikiliwa "kwa mahojiano na mambo mengine ya kiuchunguzi."

Katika akaunti yake kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), Marley aliwajulisha mashaki zake kuwa alikuwa akisaidia mamlaka katika uchunguzi wa kifo cha MohBad na alikuwa "akikutana na polisi akiwa na matumaini ya ukweli kuwekwa wazi na haki kutendeka."

MohBad alifariki katika mazingira yanayodaiwa kutokueleweka katika hospitali moja jijini Lagos, Septemba 12, 2023; na kisha “kuzikwa kwa haraka na familia yake.”

Kifo cha nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kilizua maandamano ambapo mashabiki wake, walitaka uchunguzi wa kina ufanyike, jambo ambalo lilisababisha polisi kuufukua mwili wake kwa uchunguzi zaidi.

Mashabiki walielekeza hasira zao kwa Marley, ambaye alikuwa amemsainisha MohBad chini ya lebo yake ya muziki ya Marlian Records.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa MohBad alijitoa kwenye lebo hiyo mwaka jana, baada ya kutofautiana na Marley.

Kufuatia kifo chake, video kadhaa za MohBad akilalamika kuhusu kuteteleka uhusiano wake na Marlian Records ziliibuka tena.