Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu athibitisha ni mke wa Diamond

Muktasari:

  • Uvumi uliosambaa ukibeba madai kwamba Diamond amempa talaka tatu Zuchu, uliwastua wengi hasa kwa kuwa haikuwahi kufahamika kwamba mastaa hao walikuwa wamefunga ndoa.

WAKATI sintofahau ikiendelea kuhusu kuwapo ama kutokuwapo kwa ndoa kati ya mastaa wawili wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz na Zuchu, mwanadada huyo amethibitisha uhalali huo.

Uvumi uliosambaa ukibeba madai kwamba Diamond amempa talaka tatu Zuchu, uliwastua wengi hasa kwa kuwa haikuwahi kufahamika kwamba mastaa hao walikuwa wamefunga ndoa.

Na sasa wakati anga la wapenda burudani likiwa limegubikwa na maswali ya kama ni kweli wameoana au wametalikiana, Zuchu amethibitisha kuwa ni mke halali wa Diamond baada ya kubadili status yake ya kwenye ukurasa wake wa Instagram akijitambulisha kama Mrs Nasib.

Mrs Nasib amewatangazia wafuasi wake milioni 6.8 wa katika Instagram kwamba sasa anatambulika kama mke wa Diamond Platnumz, jambo ambalo limewafanya mashabiki wake na watu mbalimbali kuzifuata posti zake za hivi karibuni na kuandika hisia zao.

"WIFE WIFEEEEEEW WIFEEEEEE. WIFEEEEEEEE," aliandika mwanadada mjasiriamali maarufu, Niffer, huku mwingine akiandika "Tuna furaha sana leo."

Na mwingine akaandika: "Hata uolewe wiki, ni kwamba umeshawahi kuwa mke wa Nasib. Tena mke wa kwanza, mimi najua hicho tu." Kisha mwingine akaongeza: "Mume unaeeee na unatamba naye. Wewweeeee!"

Na kwa wenye mitazamo tofauti, mmoja wao aliandika: "Tanzania kwa unafiki 2 ha2jambo."

Mijadala ya wawili hao kufunga ndoa ilianza Juni 1, 2025 pale Diamond Platnumz alipoandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akieleza kuwa aliwahi kufunga ndoa.

"Miongoni mwa vitu ambavyo nimejifunza ni ukomavu wa kukaa kimya... ukomavu huu unataka uvumilivu wa hali ya juu, inataka uwe na moyo wa subra na hasa kukaza roho pindi mtu au watu wanapokuwa wanakupakazia ubaya fulani kwenye jamii halafu wewe una ukweli wake lakini unatakiwa ukae tu kimya usijibu ilhali ukweli unao ndani...Kwakweli si jambo jepesi linataka ustahimilivu wa hali ya juu sana, na siwezi sema eti nauweza sana, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu amenijaalia hekima hiyo kwa kiwango chake, na nimekua nikiishi hivyo kwa muda mrefu kukaa kimya pindi yeyote akijaribu kusema lolote dhidi yangu, na ndio maana hata interview nimekuwa naepuka kufanya siku hizi... japo si jambo jepesi lakini faida yake nimeiona na ni kubwa maana vita vyako inakuwa unapambaniwa na Mwenyezi Mungu na inakufanya uwe mshindi kila siku....

"Anyways: Najua kila mmoja wenu ana picha tofauti kabisa kuhusu Diamond Platnumz na KUOA, ila tu nataka leo niwaambie kuwa HUYU DIAMOND PLATNUMZ ALISHAWAHI KUOA, na kuna siku nitawaambia ikawaje."

Kauli kwamba "Diamond alishawahi kuoa" ikatafsiriwa na wengine kuwa huenda kuna ukweli katika uvumi wa kumtaliki Zuchu.

wakati hayo yakiendelea Mwanaspoti lilifanya jitihada za kumtafuta Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Kawambwa ambaye alithibitisha alifungisha ndoa ya Diamond Platnumz na Zuchu miezi michache iliyopita.

Shekhe Walid amesema aliwafungisha ndoa hiyo wanamuziki hao miezi mitano iliyopita, lakini habari za kuachana hazifahamu.

"Kwanini watu wanapenda watu wengine wazini? Diamond na Zuchu ni kweli nimewafungisha ndoa mimi toka miezi mitano iliyopita, ila hilo swali lako unaloniuliza kuhusu wameachana mimi silifahamu sababu kama wangekuwa wameachana Diamond angekuja kuniambia," amesema Shekhe Walid.