Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra amaliza utata Yanga

DIARRA Pict

Muktasari:

  • Diarra anayemiliki clean sheet 15 hadi sasa katika Ligi Kuu Bara anahusishwa na mipango ya kuondoka klabuni, jambo lililowafanya mabosi wa Yanga kuanza kusaka mbadala wake.


KIPA namba moja wa Yanga, Diarra Djigui yupo kambi ya timu ya taifa ya Mali, lakini kabla ya kuondoka nchini amemaliza utata uliokuwa ukiwavuruga mashabiki wa klabu hiyo.

Diarra anayemiliki clean sheet 15 hadi sasa katika Ligi Kuu Bara anahusishwa na mipango ya kuondoka klabuni, jambo lililowafanya mabosi wa Yanga kuanza kusaka mbadala wake.


Hii inaweza kuwa taarifa nzuri kwa mashabiki wa Yanga, baada ya kipa Djigui Diarra kutoa msimamo wa kusalia kikosini hadi msimu ujao tofauti na aliokuwa nao awali wa kutaka kuondoka klabuni hapo wikichache zijazo.


Mwanaspoti linafahamu, kabla ya kipa huyo kuondoka kwenda katika majukumu ya kuichezea timu ya taifa ya Mali, bilionea wa klabu hiyo Ghalib Said Mohammed ‘GSM’, alifanya naye kikao kirefu na Diarra kisha wakakubaliana.

Taarifa zinasema bosi huyo alifanya mazungumzo na Diarra na kufikia makubaliano ya kusalia ndani ya kikosi hicho tena hadi mkataba utakapomalizika kwani umesalia miaka miwili baada ya msimu huu kumalizika.

Awali kabla ya kikao hicho kulikuwa na presha kubwa kutoka kwa Diarra kutaka kutimka Yanga, akipambana kutafuta ofa tofauti ili aweze kuuzwa ikiwemo ofa ya klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Kupitia Mwanaspoti taarifa za ndani ya klabu hiyo zilisema kuwa; “Diarra hataweza kuondoka tena atabaki hapa kumalizia mkataba aliona, alikutana na GSM na kuzungumza kwa kirefu na wakakubaliana hivyo, kuna mambo ambayo siwezi kuyaweka wazi lakini yalichochea kipa huyo kutamani kuondoka na kimsingi yeye (Diarra) ndiye aliyekuwa kwenye presha ya kutafuta timu kwa kuwa Yanga, wanajua kwamba kipa huyo ana mkataba wa miaka miwili umesalia.”

Hata hivyo, Kaizer ilithibitisha kwamba, haina mpango wa kumchukua kipa huyo kwenda kuungana na makocha wa zamani Nasreddine Nabi na msaidizi Cedric Kaze, wanaoifundisha timu hiyo kwa sasa.


DILI LA MANULA

Makubaliano hayo ya kusalia kwa Diarra ndani ya Yanga, kunaelezwa kumechangia kuua dili la kipa Aishi Manula aliyekuwa akipigiwa hesabu kama kipa mzawa ambaye hata hivyo amekubali kurejea Azam FC na wameshamalizana.

Awali jina la Manula lilipelekewa kwa bosi wa Yanga baada ya kuona presha na Diarra kutaka kusepa. Misimu mitatu aliyoichezea Yanga, Diarra amekuwa kipa bora mara mbili, huku tuzo hiyo ikichukulia na Ley Matampi msimu uliopita kwa kuzidiwa ‘cleen sheet na safari hii anachuana na Moussa Camara wa Simba.