Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MUSIC FACTS: Hii ndiyo maana kamili ya Chibu Dangote, ndege Sh62.9 bilioni

KWA miaka sasa mwimbaji wa Bongo Fleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amekuwa akitumia jina la Chibu Dangote, jina la Bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote mwenye utajiri wa Dola13.5 bilioni wastani wa Sh31.4 trilioni.

Diamond ambaye utajiri wake unakadiriwa ni Dola 10 milioni wastani wa Sh23.3 bilioni baada ya kuikataa ripoti iliyotaja utajiri wake ni Dola 5 milioni wastani wa Sh11.6 bilioni, alijipachika jina hilo ili kujipambanua kama msanii mwenye mafanikio zaidi. Je, hilo linasadifu vipi maisha yake?, karibu;


SH163.1 MILIONI - SHOW

Malipo ya Diamond kwa shoo za kimataifa ni Dola70,000 wastani wa Sh162.5 milioni na ndiye msanii pekee Bongo anayechukua kiasi hicho cha fedha, huku mara ya mwisho akisema malipo yake kwa shoo za ndani ni Sh100 milioni.


SH192.3 MILIONI - WAAH!

Baada ya video ya wimbo wake, Waah! kufikisha views milioni 100 YouTube, Diamond kaingiza zaidi ya Euro80,665 wastani wa Sh192.3 milioni. Kumbuka ana video tatu zenye views zaidi milioni 100, huku video zake zote zikiwa na views bilioni 1.8.


SH200 MILIONI - UBALOZI

Kwa mwezi Diamond anapokea Sh200 milioni kutokana na dili zake za Ubalozi kutoka kampuni mbalimbali, hiyo ni sawa na Sh55 milioni kwa wiki, Sh7 milioni kwa siku, Sh300,000 kwa saa na Sh6,000 kwa sekunde.


SH238.4 MILIONI - PETE

Pete tano zinazokaa kwenye vidole vya Diamond zina thamani ya Dola 100,000 wastani wa Sh238.4 milioni, fedha hiyo ni wastani wa show zake mbili tu za kimataifa ambazo atachukua Sh326.2 milioni.


SH335.7 MILIONI - SAA

Diamond amevaa saa ya kifahari inayojulikana kama Richard Mille (RM) ambayo hutengenezwa Uswizi, yeye ana aina ya RM 011 Felipe Massa Red Baden ambayo thamani yake ni Dola141,000 wastani wa Sh335.7 milioni.


SH422.0 MILIONI - CHENI

Ukimtazama shingoni cheni anazovaa Diamond zinagharimu Dola 177,000 wastani wa Sh422.0 milioni. Hivyo pete, saa na cheni zake tu ni Dola 318,000 wastani wa Sh741.4 milioni.


SH700 MILIONI - USHURU

Kwa mujibu wa Diamond, alilipa zaidi ya Sh 700 milioni kama ushuru kwa kuingiza nchini gari lake la kifahari aina ya Rolls-Royce Cullinan, Staa huyu ana magari zaidi ya manne ya kifahari likiwemo Cadillac Escalade Sky Captain.


SH2.3 BILIONI - GARI

Gari lake aina ya Rolls-Royce Cullinan amelinunua kwa bei ya Sh2.3 bilioni akiwa ndiye msanii wa kwanza Tanania, huku akiungana na Mastaa wengine wa Afrika kama Burna Boy, D’Banj, Phyno, Mr. P, J Martins, DJ Cuppy, Davido na wengineo.


SH62.9 BILIONI - NDEGE

Kama Diamond amenunua ndege binafsi ya Bombardier Challenger 605 kama ile ya msanii wa Nigeria, Davido, basi mfukoni kwake ametoa Dola27 milioni wastani wa Sh62.9 bilioni.

Hivi karibu Diamond aliithibitishia DW Africa kuwa amenunua ndege ili kuongeza thamani yake, akiungana na wasanii wengine Afrika kama Cassper Nyoves, DJ Cuppy na P Square.