Mtanzania apata shavu FIFA

Tuesday September 21 2021
fifa pic
By Ramadhan Elias

THAMANI ya Muziki wa Tanzania imezidi kuwa kubwa baada ya mwanamuziki wa nyimbo za asili, Msafiri Zawose kutoka Bagamoyo kupata nafasi ya kusikika kwenye gemu jipya la video la FIFA22.

Msafiri amepata shavu hilo baada ya wimbo wa ‘Trebidation’ alioshirikishwa na mholanzi Feiertag kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nyimbo 122 za wasanii 27 zitakazosikika kama ‘Sound track’ za gemu hilo.

Katika orodha hiyo Msafiri ndiye msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyepata fursa hiyo huku wengine wengi wakiwa kutoka katika mataifa ya Ulaya.

Sambamba na wimbo wa Trebidation, Msafiri ananyimbo nyingine kama Penye Safari, Yale na Heyyey na Albamu tatu za Tanganyika yenye jumla ya nyimbo 11, Tija yenye nyimbo tisa na Uhamiaji yenye nyimbo 13.

Gemu hilo linalosubiriwa kwa hamu zaidi na wachezaji wake linatarajiwa kuachiwa rasmi Septemba 26 mwaka huu chini ya kampuni ya Erectronic Arts ikiwa ni muendelezo wa kila mwaka/msimu.

Advertisement