Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misso Missondo ni upepo tu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

KWENYE tasnia ya burudani kwa sasa anayetrendi ni DJ anayeitwa Misso Missondo ambaye kwa sasa ‘upepo’ umemgeukia na kila kona unayopita lazima utamsikia.

Misso mzee wa ‘Umepigaje hapo’, ametrendi baada ya video zake fupi zikimuonyesha akipiga muziki huku baadhi ya mashabiki zake wanaonekana kuvalia makoti makubwa wakicheza kwa aina ya kipekee katika mazingira ya vijijini mkoani Mtwara.

Misso mwenye umri wa miaka 23 amefunguka kuwa hajasomea UDJ lakini kupitia kujitafuta akajikuta anakuwa DJ kutokana na kupenda kazi hiyo na ana muda wa zaidi ya miaka miwili akipiga ngoma Kanda ya Kusini lakini kwa sasa ndio amekuwa maarufu Tanzania.

“Wakati wa Mungu ndio wakati sahihi. Nimekuwa nikipiga muziki huko Kusini na wengi wananitambua lakini katika maeneo mengine nadhani walikuwa hawajazingatia kama ilivyo sasa, nadhani huu ndio muda sahihi na mimi nipo tayari kupambana kwa muda wowote ili Watanzania wafurahi,” alisema Misso Missonda.

Misso aliweka wazi namna alivyokutana na madansa wake ambao staili yao ni kuvaa makoti makubwa machafu na kuunda timu.

“Wale jamaa tulijuana kwenye shoo moja ambayo mimi na wao tulialikwa tukafanye kazi kila mmoja kimpango wake, baada ya kuona tunaendana ikabidi tuanze kufanya kazi kwa pamoja. Nawakubali na siwezi kuwaacha,” alisema.

Hadi sasa Misso Misondo amefanya ngoma na Staa wa Bongo fleva, Rayvanny iitwayo ‘Kitu Kizito’, na tayari amehamia Dar es Salaam kutoka Mtwara baada ya kupata shavu katika moja ya vituo vya redio vya jijini hapa.