Paula: Sijutii kubadili dini

Muktasari:
- Paula alisema kila mwanadamu ana nguvu yake ya kumfanya abadilike na kuwa tofauti kabisa na huko nyuma ilikuwa upande wa dini ya kikristo na sasa ameamua kuwa muislamu.
MWANAMITANDAO, mrembo na mzazi mwenza na nyota wa Bongo Fleva, Marioo, Paula Kajala amesema hajutii kitendo cha kubadili dini kwa lengo la kufunga ndoa na baba watoto wake huyo.
Paula alisema kila mwanadamu ana nguvu yake ya kumfanya abadilike na kuwa tofauti kabisa na huko nyuma ilikuwa upande wa dini ya kikristo na sasa ameamua kuwa muislamu.
“Kitu ambacho siwezi kujutia katika maisha yangu ni uamuzi wa kubadili dini ili niolewe, nafurahia sana kitu nilichoamua kwa hiyari yangu kwani ni kikubwa kwenye maisha yangu, sijui nisemaje na niwaambie tu watu, nimeshaanza mazoezi ya kusali na nimejua kuvaa mavazi mazuri ya heshima na hicho ndicho kikubwa kwangu,” alisema Paula.
Hii itakuwa habari njema kwa baadhi ya watu wanaotamani wawili hao wafunge ndoa wakiwamo wazazi wao, projuza P Funk na Kajala kwa upande wa Paula na mama mzazi wa Marioo.
Awali Marioo aliongea na Mwanaspoti juu ya ndoa hiyo na kudai itafanyika hivi karibuni kwani Paula amekubali kubadili dini.
“Sisi hapa tunatarajia kuoana, kwa sasa bado tunaishi kihuni lakini tutaoana na Paula ndiye atakayebadili dini na kuwa muislamu,” alisema Marioo.