Maya: Hakuna kama Kanumba

Mwigizaji wa kike na mpambaji wa wasanii, Mayasa Mrisho ‘Maya’
Muktasari:
Maya alisema kukosekana kwa Kanumba kumemfanya aachane na kazi za usimamizi na upambaji katika filamu na kurudia uigizaji.
MWIGIZAJI wa kike na mpambaji wa wasanii, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ambaye ameamua kurudi rasmi kwenye uigizaji amesema kwa sasa hapa Bongo hakuna mtayarishaji aliyekuwa akijali kazi yake kama marehemu Steven Kanumba.
Maya alisema kukosekana kwa Kanumba kumemfanya aachane na kazi za usimamizi na upambaji katika filamu na kurudia uigizaji.
Maya alisema Kanumba alithamini utendeji wa kazi na watayarishaji wengine ni wabinafsi hawajali utendaji wake wa kazi na kumtaja Jacob Steven ‘JB’ kidogo anajitahidi kwa kuthamani kazi yake.
“Niwe muwazi katika tasnia ya filamu, kwa sasa hakuna kama marehemu Kanumba, sioni faida ya kufanya kazi kama nilizokuwa nikizifanya na Kanumba, nimerudia kuigiza hakuna mtayarishaji anayejali kazi yangu,” anasema Maya.