Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 wasiyoyafahamu rafiki zako kuhusu Vanessa

Mambo 10 wasiyoyafahamu rafiki zako kuhusu Vanessa

Kwa kipindi cha takribani miaka saba katika muziki wa Bongofleva, Vanessa Mdee alijipambanua kama msanii mwenye kiu ya kulikamata soko la kimataifa, na kweli alifanikiwa kwa kiasi chake.

Licha ya kutangaza kuachana na muziki huo, bado alama aliyoiachana inaoneka na kuwa mfano wa kuigwa na wengi, kwa kulitambua hilo, Bongo Music Facts inakusogezea mambo 10 wasiofahamu rafiki zako kuhusu Vanessa Mdee.


1. Albamu ya Vanessa, Money Mondays iliyotoka Januari 2018 iligharimu ShMilioni 100 hadi kukamilika, fedha hizo zilitumika kwenye kulipia studio, kuwalipa wasanii walioshiriki, kutengeneza video pamoja na matangazo.

Ndani ya mwezi mmoja albamu hiyo iliuza nakala 4,000 na kila mmoja ilikuwa ikiuzwa kwa Sh10,000, hivyo kwa kipindi hicho iliweza kufikisha mauzo ya Sh40 milioni.


2. Wimbo wa kwanza kuutoa Vanessa unaitwa Closer ambao ulishinda Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 2013 kama Wimbo Bora wa RnB, huku ukiandika rekodi ya kupata downloads 30,000 ndani ya wiki moja.


3. Wimbo namba nane kwenye albamu yaVanessa, Money Mondays unaitwa Pumzi ya Mwisho, huu umechukua vionjo kutoka kwenye wimbo wa Marehemu Mubaraka Mwishehe, Jogoo la Shamba.

Hata hivyo, wimbo huo Vanessa alipewa na Joh Makini ambaye pia amesikika kwenye ngoma hiyo pamoja na msanii kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest.


4. Awali Vanessa alikuwa akichana kabla ya kuanza kuimba na kufanya vizuri, alionyesha uwezo huo aliposhirikishwa na DJ Choka kwenye wimbo, Press Play, pia hata kwenye wimbo wake ‘Pumzi ya Mwisho’ amefanya hivyo.


5. Vanessa ndiye aliyewashauria Aika na Nahreel wanaounda kundi la Navy Kenzo kuendelea na muziki baada ya kukata tamaa na kutaka kuacha muziki na kwenda kusoma Masters nje ya nchi.

Kutokana na ushauri wa Vanessa, Navy Kenzo wakatoa wimbo wao, Bokodo ambao ulikuja kufanya vizuri na ukawa mwanzo wa mafanikio yao. Hata hivyo, sasa Vanessa ameacha muziki rasmi akiwa na albamu moja, huku Navy Kenzo wakijiandaa kuachia albamu yao ya nne.


6. Wakati Vanessa akiwa Mtangazaji aliwahi kufanya mahojiano na wasanii wakubwa duniani kama Kelly Rowland, French Montana, Trey Songs, Rick Ross, Ludacris na wengineo.


7. Mwaka 2017 Vanessa Mdee alikutana na Rais wa Gabon, Ali Bongo wakati wakirekodi project ya The African Queens ya Rais huyo pamoja na msanii mkongwe nchini humo, Frédéric Gassita.

Pia ni mwaka huo huo ambao msanii Mwana FA alipigiwa simu na aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli akimueleza kuwa anaupenda wimbo wake, Dume Suruali ambao Vanessa Mdee ndiye aliyeimba kiitikio chake.


8. Wasanii wa kike wanaomvutia Vanessa kwenye muziki kutoka nje ya Tanzania ni Alicia Keys, Whitney Houston, Lauryn Hill, Toni Braxton, Celine Dion, Monica, Destiny’s Child, Aaliyah, Mary J. Blige na Mariah Carey.


9. AYamemshirikisha Vanessa kwenye wimbo wake, Money, halafu akamshirikisha mdogo wake na Vanessa, Mimi Mars kwenye wimbo wake mwingine, Stakaba.

Hivyo hivyo kwa Mwana FA aliyemshirikisha Vanessa kwenye wimbo wake, Dume Suruali, kisha baadaye naye Mimi Mars akamshirikisha Mwana FA kwenye wimbo wake, EX Remix.


10. Kwa mara ya kwanza Vanessa na Mchumba wake, Rotimi walikutana kwenye Tamasha la Essance nchini Marekani ambapo wote walitumbuiza kwa wakati tofauti na jukwaa tofauti. Pia kwa mara ya kwanza Vanessa na aliyekuwa mpenzi wake, Jux walikutana studio, B Hit’s Music Group na aliyewakutanisha ni Marehemu Prodyuza Pancho Latino.