Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombinesheni ya watu hawa ni hatari

KOMBINESHENI Pict

Muktasari:

  • Wawili hao wamefanya kazi mbalimbali kama Chanya na Hasi, vita ya Mtukufu na Goliath na nyingine nyingi, ambazo zimekuwa na mvuto mkubwa kutokana na Julias kuwa mrefu zaidi na Mtukufu mfupi.

MSANII wa maigizo na filamu za mapigano, Julias Charles ‘Giant’ amezungumzia kombinesheni yake na msanii mwenzake anayejulikana kwa jina la kisanii Mtukufu (mfupi) kupendwa zaidi na jamii, wanapoachia kazi zao mitandaoni.

Wawili hao wamefanya kazi mbalimbali kama Chanya na Hasi, vita ya Mtukufu na Goliath na nyingine nyingi, ambazo zimekuwa na mvuto mkubwa kutokana na Julias kuwa mrefu zaidi na Mtukufu mfupi.

“Tuna miaka takriban mitatu tunafanya kazi pamoja, kuna kazi yetu iliwahi kupostiwa hadi katika mitandao mbalimbali ya Marekeni, kilichokuwa kinawavutia mimi ni mrefu na Mtukufu ni mfupi hivyo anakuwa anakimbia chini ya miguu yangu ambayo siwezi kuinama kwa haraka kumshika wakati ananiletea mauzauza, ila na mimi nikimnyanyua juu juu anakuwa hana cha kufanya zaidi ya kuwa mpole,” alisema Giants shabiki wa Simba lialia na kuongeza;

“Katika mitandao yetu ya kijamii Mtukufu ana watu wengi kuliko mimi, jambo ambalo linasaidia zaidi kazi zetu kupata umarufu kwa haraka katika jamii.” Msanii huyo alijulikana zaidi baada ya kushirikishwa katika wimbo wa muimbaji wa injili Rose Mhando wa Secret Agenda na anafanya vizuri tamthilia ya Huba.