Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joshua Pianno: Ngoma ya Mondi imetembelea nyayo zangu!

PIANO Pict

Muktasari:

  • Ambacho hukijui, Pianno ni mtunzi na mwimbaji, alitoka Mbeya na kuja Dar es Salaam kufanya biashara na alikuwa mfanyabishara wa nguo maeneo ya Ubungo huku akiwa hana makazi maalum, akawa analala chini ya meza na kwenda kwa Mkubwa Fella kwa ajili ya kuomba nafasi ya kujiunga kuimba kutokana na kuwa na kipaji hicho.

JOSHUA Pianno, moja ya majina chipukizi yanayokimbiza kwenye muziki wa Dansi. Alikotokea ni stori ndefu na mwenyewe anasema alipanda milima na mabonde hadi kufika alipo.

Ambacho hukijui, Pianno ni mtunzi na mwimbaji, alitoka Mbeya na kuja Dar es Salaam kufanya biashara na alikuwa mfanyabishara wa nguo maeneo ya Ubungo huku akiwa hana makazi maalum, akawa analala chini ya meza na kwenda kwa Mkubwa Fella kwa ajili ya kuomba nafasi ya kujiunga kuimba kutokana na kuwa na kipaji hicho.

Pianno anasema alijiunga kwa Mkubwa Fella na hadi kuingi bendi ya Twanga Pepeta.

Siku hiyo walikuwa mazoezini kwa Mkubwa Fella, ndipo Asha Baraka mmiliki wa bendi ya Twanga Pepeta, alimpigia simu Mkubwa Fella anahitaji vijana wa kujiunga na bendi yake.

Kwa sababu alikuwa anapenda muziki wa dansi, alipochaguliwa kwenda kujiunga na bendi hiyo alikubali kiroho safi, akakutana na Asha Baraka na siku hiyo hiyo wakapandishwa kwenye ukumbi wa Mango Garden kwa ajili ya kuimba kwa majaribio, hiyo ilikuwa mwaka 2017.

Katika mahojiano ya Mwanaspoti na Pianno yaliyofanyika maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, anasema siku ya kwanza kupanda jukwaani alikuwa anatetemeka akiangalia kwenye ukumbi watu walikuwa wamejaa sana.

PIA 02

“Yaani siku ya kwanza kupandishwa jukwaa la Twanga Pepeta nilikuwa najiuliza nitaimba nini, lakini namshukuru Mungu nilikuwa nimejifunza kuimba live tokaka kwa Mkubwa na Wanawe, na uzuri kichwani nilikuwa nimekariri wimbo wa Aminata kutoka bendi ya Twanga Pepeta,” anaanza kueleza.


Tangu ujiunge Twanga Pepeta ushatunga nyimbo ngapi?

“Nimetunga wimbo mmoja unaoitwa Shobo na ndiyo ulionitambulisha kwenye ulimwengu wa muziki wa dansi, lakini nimeshiriki kuimba kwenye nyimbo nyingi za bendi ambazo ni Dr Ruby, Penzi Sigara Kali, Chombo ya Fundi, Twanga Mbele na Povu.


Unatamani kuwa nani?

“Kwa wanamuziki wa dansi kwa nje ya nchi natamani kuwa kama Fally Ipupa kwa sababu huwa haweki vitu vingi kwenye muziki wake, ana melody tamu, anafanya vizuri kimataifa na hata akiwa jukwaani analitendea haki jukwaa.

“Kwa Tanzania natamani kuwa kama Ally Choki, kwa sababu ni mwanamuziiki ambaye hadi leo akisimama jukwaani akiimba sauti yake haijwahi kubadilika wala kuchoka na amefanya mambo mengi makubwa kwenye muziki wa dansi na utunzi wa  nyimbo zake zinaishi.

PIA 04

Muziki wa dansi unadaiwa umeshuka, ilikuwaje ukajiingiza huko ikiwa bado wewe ni chipukizi?

“Mimi nadhani mwenyezi Mungu ndiye anayepanga, kila siku wanavyosema muziki wa dansi umeshuka basi huenda mimi ndiye nimekuja kuupandisha na ndiyo maana sikuwa na hofu kujiingiza kwenye hii tasnia, pia kushuka kwa muziki huu kunasababishwa na sisi wenyewe wanamuziki wa dansi kushindwa kutangaza kazi zetu yaani tupo tofauti na wenzetu wa Bongo Fleva.

PIA 03

Unazungumziaje miaka 30 ya Asha Baraka kwenye muziki wa dansi?

“Hii ya miaka 30 ni kitu kikubwa sana, anapaswa kupongezwa sana kwa sababu amefanya mambo makubwa kwenye huu muziki, niseme tu mama yangu Asha Baraka ni jasiri na siku ya tukio nitajiandaa kwa ukubwa zaidi kwa vitu tofauti tofauti.”


Wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?

“Mimi ni wa pili katika watoto watano.


Upo kwenye Mahusino?

“Ndiyo, nipo kwenye mahusiano tena nampenda sana mpenzi wangu kwa sababu ananiheshimu na mimi namheshimu.

PIA 01 (1)
PIA 01 (1)

Wewe ni timu gani?

“Nashabikia Simba, ila sio shabiki wa mpira kihivyo, niseme tukifungwa nakosa raha, kiufupi huwa sifuatilii mpira, ila katika wa wachezaji wa Simba nawajua wawili tu, Mohamed Hussein na Aishi Manula.


Mbali na Dansi muziki gani ulishawahi kufanya?

“Naimba na kutunga Bongo Fleva, nafanya muziki wa aina yoyote, wimbo wangu wa Bongo Fleva nilioanza kuutoa unaitwa Sielewi, ukiusikiliza unafanana na wimbo wa Diamondi unaoitwa Sikomi, nilianza kuutoa mimi, kisha Diamond akafuata kutoa wake,” anasema Pianno.