Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata hivyo, Yammi bado analipa...!

Yammy Pict
Yammy Pict

Muktasari:

  • Katika TMA 2023, Yammi aliwania kipengele cha Msanii Bora Chipukizi kupitia wimbo wa Namchukia washindani wake walikuwa ni Xouh (Lalala), Appy (Watu Feki), Mocco Genius (Mi Nawe) na Chino Kidd (Gibela) aliyeibuka mshindi.

LICHA ya kutoshinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2023, bado haiondoi ukweli kwamba Yammi alifanya vizuri mwaka uliopita baada ya kutambulishwa katika rekodi lebo ya The African Princess inayomilikiwa na Nandy.

Katika TMA 2023, Yammi aliwania kipengele cha Msanii Bora Chipukizi kupitia wimbo wa Namchukia washindani wake walikuwa ni Xouh (Lalala), Appy (Watu Feki), Mocco Genius (Mi Nawe) na Chino Kidd (Gibela) aliyeibuka mshindi.

Utakumbuka Januari 20, 2023 ndipo The African Princess Label ilimtambulisha Yammi akiwa msanii wa kwanza kusainiwa na lebo hiyo, ujio wake ukiambatana na EP, Three Hearts (2023) yenye nyimbo tatu ambazo hakumshirikisha msanii yeyote.

Hiyo ni baada ya Nandy kumuona Yammi akiimba nyimbo za wasanii mbalimbali katika mtandao wa TikTok na kuvutiwa na kipaji chake, basi wakakutana na kuzungumza biashara ya muziki kisha akamsaini.

Ukitazama namba katika majukwaa ya kidijitali ya kusikiliza muziki Yammi yupo juu ya wote aliokuwa anawania nao TMA. Nyimbo zake zina namba kubwa hata mara mbili ya washindani yake. 

Mathalan katika YouTube, mtandao unaotumiwa na mashabiki wengi Bongo ukichukua nyimbo zilizowapa tiketi ya kuwania Msanii Bora Chipukizi TMA 2023, Yammi ndio yupo juu wimbo wake Namchukia ukiwa umetazamwa (views) mara milioni 3.7. Hao wengine namba zao zipo hivi; Xouh (Lalala) - views 743k, Appy (Watu Feki) - milioni 2.6, Mocco Genius (Mi Nawe) - milioni 3, na Chino Kidd (Gibela) - milioni 1.7, na hawa wote hizi ndio video zao pekee zenye namba kubwa zaidi YouTube. 

Lakini kwa Yammi, wimbo alioingia nao TMA sio ndio wenye namba kubwa zaidi kwake, kuna mwingine, Tiririka (2023) ambao video yake ina ‘views’ milioni 10 na ulikuwa na sifa ya kuwania kipengele hicho maana nao umetoka mwaka uliopita. Sijui kwanini Yammi au TMA waliuacha wimbo huu (Tiririka) na kuuchukua ule mwingine (Namchukia) yenye namba za chini kwake lakini ukiwa juu zaidi kwa washindani wake. 

Kwa kutazama kigezo hiki, pengine Yammi ndiye alistahili ushindi kama Msanii Bora Chipukizi, lakini ipo hoja kuwa kufanya vizuri katika majukwaa ya kidijitali sio kipimo cha mwisho cha msanii kukubalika. Hata hivyo, bado Yammi kupitia muziki wake anaonekana kuwa na ushawishi zaidi, tangu ametambulishwa katika tasnia hapo Januari 2023 ameweza kuwavutia wafuasi (followers) zaidi ya milioni 1 Instagram kitu ambacho hao washindani wake wameshindwa!.

Ukiachana na Zuchu ambaye alipata wafuasi milioni 1 Instagram ndani ya miezi mitano baada ya kutambulishwa na WCB Wasafi, Yammi ndiye msanii anayefuata kwa kuwa rekodi nzuri zaidi eneo hilo.

Hata hivyo, labda Yammi alikosa tuzo hiyo kutokana na historia ya kipengele hicho kutoa washindi wachache wa kike, kwa mfano, tangu msimu wa TMA 2010 hadi 2015 ziliposimama ni msanii mmoja tu wa kike aliyeshinda ambaye ni Linah 2011.

TMA ziliporejea 2022 kwa kuanza kuwatunza waliofanya vizuri 2021, kipengele hicho cha Msanii Bora Chipukizi kiligawanywa kwa kuzingatia jinsia ndipo Rapcha na Phina wakashinda msimu 2021, na Kontawa na Gachi 2022.

Lakini msimu huu wa 2023 ambao hafla yake ilifanyika Oktoba 19 mwaka huu katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki ukaondoa utaratibu huo wa kutoa mshindi kwa kila jinsia katika kipengele hicho cha Msanii Bora Chipukizi TMA.

Ingawa Yammi ameondoka mikono mitupu TMA 2023, bado analipa, ikumbukwe ni msanii wa tatu wa kike Bongo aliyesikilizwa zaidi (most streamed) katika mtandao wa Boomplay Music mwaka uliopita akiwa ametanguliwa na Zuchu na Nandy. Utakumbuka Nandy, mshindi wa tuzo nne za TMA, alipata wazo la kufungua lebo pindi alipoachia albamu yake ya kwanza, The African Princess (2018) chini ya Epic Records.