Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mose Iyobo, Aunt Ezekiel vita yao ni kali

IYOBO Pict

Muktasari:

  • Mose na Aunt wamezaa mtoto mmoja wa kike aitwae Cooke na baadae kuachana na kwa sasa kila mmoja yupo katika mahusiano mengine.

MSANII wa Bongo Movie Aunt Ezekiel na mzazi mwenzake, Moses Iyobo wameingia katika vita nyingine ya kurushiana maneno sababu kubwa ikiwa ni malezi ya mtoto wao.

Mose na Aunt wamezaa mtoto mmoja wa kike aitwae Cooke na baadae kuachana na kwa sasa kila mmoja yupo katika mahusiano mengine.

Hata hivyo, licha ya kuwa na mwanzo mzuri na kufikia hatua ya kupata mtoto pamoja, wawili hao kwa sasa wamekuwa wakitupiana maneno katika vyombo vya habari na mitandaoni, huku Aunt akidai Mose sio mzazi bora na anapambana mwenyewe kumlea.

Akiwa katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Mose alijinadi anamlea mtoto huyo kama kawaida na ana uhuru wa kuonana kwa rahisi.

Baada ya mahojiano hayo, Aunt aliibuka na kuandika katika ukurasa wake wa Instagram hataki kuongelea suala hilo na kumchana Mose sio mzazi bora kwa mtoto wao hata anapomchukua kwenda kumsalimia.

Imekuwa kawaida kwa wawili kurushiana maneno mitandaoni na Mose aliwahi kusema analea watoto tena wawili kwani Aunt ni mkubwa kwa mzazi mwenza wa Aunt wa sasa, Kusah.

Mwanaspoti liliwatafuta wawili hao kwa nyakati tofauti kuzungumzia vita yao hiyo ya maneno na nini hasa kinaendelea na haya ndiyo yalikuwa maelezo yao. Mose alisema;

"Mimi niko salama kabisa na naendelea vyema na maisha yangu, ila nikuambie kitu, ukiona mtu uliyeachana naye kwenye mahusiano anakuongeleaongelea basi jua bado anakuhitaji au kuna kitu kizuri anakumbuka. Sasa mimi ni mwanamume  niliyepitia kwenye changamoto nyingi kutokana na watu, kwanza kudharau kazi yangu ya kudansi na kuona kama hailipi, lakini nimeonyesha watu kuwa kazi ni kazi na ukiifanya kwa ubunifu wangu nikatoboa ndiyo maana hadi leo naendesha maisha yangu kupitia kudansi, sasa anavyokuja mwanamke na kuniambia nina maisha magumu mara simhudumii mtoto wakati ukweli anaufahamu, naona kama anaamua tu kuongea, halafu mimi sitaacha kumuongelea mwanangu sehemu yeyote kwani nina haki naye. Yaani niulizwe kuhusu mtoto wangu nishindwe kujibu kisa sina mawasiliano mazuri na mama yake? Kikubwa simzungumzii mama yake nazungumzia mtoto damu yangu. Yaani nikiulizwa mtoto hajambo nisijibu (kicheko), sema haya mambo yanayoendelea mimi nitayamaliza mwenyewe na mimi sio mtu wa kuongeaongea mitandaoni au kwa watu watu," alisema Mose.

Kwa upande wa Aunt Ezekiel, alisema; "Mimi nishaandika kile nilichotaka kumfikishia ujumbe Mose Iyobo, ujumbe kaupata, nishamaliza, kikubwa afate ushauri wangu."

Hata hivyo, Mwanaspoti lilimuuliza Aunt kama ni sahihi kufikisha ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram na alisema;

"Mie naona ni sahihi tu, sababu yeye ameongelea hadharani kwa nini na mimi nisimweke hadharani, halafu siku nyingi alikuwa anataka nimuongolee ndiyo nishampa 'airtime'" alisema Aunt.