Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hadithi ya ndoto za Diamond inavyojirudia

Muktasari:

  • Basi wakajichanga mwenye jero akatoa, mwenye bati akatoa. Wakapita kwa Mangi wakachukua sembe, wakapandisha rodi kwa Mama Chachambu wakachukua miguu ya kuku miksa pilipili ya mbilimbi. Wakarudi bondeni, ghetoni wakatoa kitu na kuanza kula. Walivyomaliza kula Naseeb akasema, “wanangu mnajua nini? Siku moja nitakuwa msanii mkubwa na tajiri zaidi Tanzania.”

UKIMTAFUTA mshkaji mmoja aliyekuwa na Diamond Platnumz kule Tandale atakusimulia hii stori. Jioni fulani hivi walikuwa wamekaa kijiweni na Diamond kipindi hicho anaitwa Naseeb. Mara wakahisi njaa, mshikaji mmoja akatoa wazo: “Wanangu nina ubao. Tunafanyaje.” Mwingine akasema, “mafuta ya taa yapo kwenye jiko ghetto, hapa tukipata unga na miguu ya kuku kwa Mama Chachambu itakuwa unyama.”

Basi wakajichanga mwenye jero akatoa, mwenye bati akatoa. Wakapita kwa Mangi wakachukua sembe, wakapandisha rodi kwa Mama Chachambu wakachukua miguu ya kuku miksa pilipili ya mbilimbi. Wakarudi bondeni, ghetoni wakatoa kitu na kuanza kula. Walivyomaliza kula Naseeb akasema, “wanangu mnajua nini? Siku moja nitakuwa msanii mkubwa na tajiri zaidi Tanzania.”

Sasa unajua wanawe walimwambia nini? “We naye ukishibaga unakuwa jau sana. Hebu nenda msalani ukajisaidie bana.”

Mimi nimewaza tu, sina uhakika kama stori atakayoisimulia rafiki wa Diamond itakuwa kama hii, lakini nina uhakika itaisha na funzo hili hili kwamba watu hawakuamini kama ndoto ya Naseeb ya kuwa msanii maarufu zaidi Tanzania na tajiri inawezekana, lakini leo hatuwezi kukataa kwa sababu tunaiona inaishi.

Majuzi kati, Diamond akiwa anazindua Wasafi Festival akajikuta anawaaambia watu ndoto yake kubwa zaidi. Alisema: “Ndoto yangu ni kuwa tajiri namba moja duniani na nitakuwa tajiri namba moja duniani.” Otea baada ya kusema hivyo hali ilikuwaje mtandaoni. Unaambiwa watu wakaanza kumshambulia, ‘kuwa tajiri namba moja duniani mchezo. Labda uwe tajiri namba moja kwenye ukoo wa Juma Lokole.’ Hapohapo wakatokea wachambuzi wa uchumi na masuala ya fedha wakasema "Diamond hawezi kuwa tajiri namba moja dunaini." Na wachambuzi wakaanza kumwaga sababu zao za kichambuzi.

Wengine walisema hawezi kuwa tajiri namba moja duniani kwa sababu ukitazama Top 10 ya matajiri wakubwa duniani hakuna msanii wala mwanamichezo, matajiri wakubwa duniani ni wagunduzi kwa sababu walileta kitu kipya duniani au waliboresha kitu kilichokuwepo. Sasa mtu wa kuimba Komasava ataingiaje hapo.

Wengine wakasema hawezi kuwa tajiri wa kwanza duniani kwa sababu hivi tunavyozungumza tu tajiri wa kwanza duniani, Elon Musk ana utajiri wa Dola 252 bilioni za Marekani  ambazo tukizileta kwa shilingi sijui hata zinaitwaje.

Wakati makadirio ya utajiri wa Diamond kwenye mtandao na siyo makadario ya uhakika kwa sababu hayajafanywa na vyanzo vya uhakika, ni kama Dola 10 milioni za Marekani tu. Kwa maana hiyo pesa za Elon Musk zinaweza kutosha kutengeneza kina Diamond wengine kama 25,200.

Kwa kifupi walichokuwa wanajaribu kusema wachambuzi na wadau ni kwamba Diamond anaota kwelikweli - tena ndoto za alinacha haziwezi kutimia na ikiwezekana aamke kutoka kwenye huo usingizi.

Wakati nawasoma wachambuzi akili yangu ikaniambia unaona jinsi leo wachambuzi na wadau wanamzomea na kumpiga masingi Diamond kwa kusema kuwa ndoto yake ni kuwa tajiri namba moja duniani? Ndivyo ambavyo miaka 16 au 18 nyuma washikaji zake walikuwa wanamwambia maneno hayohayo.

Kiuhalisia kweli ndoto ya kuwa tajiri namba moja duniani ni ndoto kubwa na iliyo mbali na uhalisia kwa watu wengi duniani, lakini swali langu ni je kuna shida gani kuota?