Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BONGO MUSIC FACTS: Mchizi Mox kamwandikia sana Albert Mangwair nyimbo!

Muktasari:

  • Huyu ni miongoni mwa wasanii waliounda kundi la Wateule akiwa na wenzake kama Jay Moe, Solo Thang na Jaffarai, pia kuna Lady Lou na Mack 2B ambao tayari wametangulia mbele ya haki. Mfahamu zaidi Mchizi Mox.

KWA sasa Mchizi Mox ni miongoni mwa wakongwe wenye heshima kubwa ndani ya Bongofleva, alifanya vizuri akiwa ndani ya kundi na hata alipotoa kazi zake kama solo bado zilipata mapokezi mazuri kwa mashabiki.

Huyu ni miongoni mwa wasanii waliounda kundi la Wateule akiwa na wenzake kama Jay Moe, Solo Thang na Jaffarai, pia kuna Lady Lou na Mack 2B ambao tayari wametangulia mbele ya haki. Mfahamu zaidi Mchizi Mox.


1.  Mchizi Mox alianza muziki akiwa shule ya msingi Lumumba, Dar es Salaam ambako kwa wakati huo alikuwa anapiga tarumbeta, filimbi na ngoma katika bendi ya shule na kila jioni baada ya masomo alifanya mazoezi ya muziki.


2. Baadaye Mchizi Mox alikuja kukutana na Jay Moe na Jaffarai ambao alikuwa akiishi nao mtaa mmoja, Makumbusho na kwa vile wote walikuwa na kiu ya kufanya muziki, basi wakawa marafiki wa karibu zaidi.


3. Wakiwa katika harakati za muziki, shule iliwatengenisha, Mchizi Mox na Jay Moe walienda kusoma Mbeya ila shule tofauti, hivyo hivyo kwa Jaffarai naye akashika njia yake kimasomo ila kila likizo walikutana na kuendelea na muziki.


4. Baada ya Mchizi Mox, Jay Moe, Jaffarai na wenzao kuibuka washindi katika mashindano ya kusaka vipaji vya muziki ambayo P-Funk Majani na Master J walikuwa ndio majaji, ndipo likazaliwa kundi la Wateule na kusainiwa Bongo Records.

Kundi la Wateule lililoanza mwaka 1998 lilifanya vizuri na nyimbo zao kama Msela, Si Ndio, Pengo, Nipende Nichukie, Tumerudi Tena, Vile Vile n.k.


5. Mwaka 2000 ndipo Wateule walisainiwa Bongo Records na Majani na mwaka uliofuatia Jay Moe akasainiwa kama solo na kufanikiwa kutoa albamu zake mbili, Ulimwengu Ndio Mama (2002) na Mawazo ya Jay Moe (2004).

Hata hiyo, Solo Thang kutoka Wateule na Juma Nature ndio wasanii wa kwanza kusainiwa Bongo Records rasmi katika mtindo wa kibiashara, ila awali lebo hiyo ilisimamia kazi za Dolla Sol, Hashim Dogo na kundi la No Name ambalo Majani pia alikuwepo.


6. Katika nyimbo mbili ambazo alishirikiana na marehemu Ngwea, ‘Mikasi’ na ‘Demu  Wangu’, zote Mchizi Mox ameandika yeye japokuwa katika ‘Mikasi’ kutoka katika albamu, A.K.A Mimi (2004) mistari ya mwanzoni Ngwea aliandika mwenyewe akiupa mwanzo wa stori  wimbo huo.

Ngwea ambaye alianza muziki ndani ya kundi la Chemba Squad lililoanzishwa mwaka 1999, naye alipata nafasi ya kusainiwa Bongo Records baada ya kufanya vizuri na wimbo wake, Ghetto Langu (2022).


7. Kundi la Chemba Squad lililoundwa na  Mez B, Ngwea, Dark Master na Noorah, wasanii wake walikuwa na ushirikiano mkubwa na Wateule ndio sababu Jay Moe aliweza kufanya kazi kama ‘Kimya Kimya’ akiwa na Ngwea.

8. Tangu akiwa mdogo, Mchizi Mox alikuwa na ndoto ya kuwa baharia, kazi aliyofanya baba yake na walisafiri pamoja sehemu mbalimbali kitu kilichomfanya kupenda ubaharia ila muziki ukaja kuua kabisa ndoto hiyo.


9. Mtu wa kwanza kumpeleka Mchizi Mox studio alikuwa ni mama yake mzazi aliyempeleka studio ya Big November, Kariakoo na kurekodi wimbo wake wa kwanza, Watoto wa Mitaani (1999).


10. Video ya wimbo wa Mchizi Mox, Chupa Nyingine (2009) iliachiwa rasmi mwaka 2022 ikiwa ni miaka 13 tangu wimbo huo utoke. Hii ni sawa na video ya wimbo wa Mandojo na Domokaya, Nikupe Nini (2005) ambayo ilitoka rasmi 2020 ikiwa ni baada ya miaka 17 tangu wimbo ulipotolewa.