Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bi Sonia afariki dunia

Dar es Salaam. Msanii wa filamu  Farida Sabu maarufu kwa jina la  'Mama Sonia' amefariki.
Mama Sonia amewahi kutesa katika maigizo mbalimbali ya kundi la Kaole na karibuni alitamba na tamthiliya ya Kapuni.


Taarifa hiyo imethibitishwa leo Alhamisi Julai 21, 2022 na  Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji, Chiki Mchoma

Mchoma amesema mama Sonia amekutwa na umauti leo akiwa Zanzibar kwa mtoto wake aliyekuwa akimuuguza.
"Msiba upo Zanzibar na atazikwa hukohuko," amesema Mchoma

Mara ya mwisho alikuwa akionekana katika tamthiliya ya Ndoano iliyokuwa inaruka kituo cha Azam ambayo ilishirikisha wasaniii waliowahi kuigiza Kaole ikijulikana kama kundi la 'Return of Kaole'