Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Babu Tale mbaroni kwa amri ya Mahakama

Mkurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections, Hamis Taletale ‘Babu Tale’

Muktasari:

  • Februari 16, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Wilbard Mashauri alitoa amri ya kukamatwa Babu Tale na nduguye Idd Taletale na kupelekwa Gereza la Ukonga kama wafungwa wa kesi ya madai hadi Mahakama itakapotoa maelekezo mengine.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ ametiwa mbaroni na polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kwa amri ya Mahakama Kuu na kufikishwa kortini.

Februari 16, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Wilbard Mashauri alitoa amri ya kukamatwa Babu Tale na nduguye Idd Taletale na kupelekwa Gereza la Ukonga kama wafungwa wa kesi ya madai hadi Mahakama itakapotoa maelekezo mengine.

Hata hivyo, hakupatikana ndipo mahakama ilipotoa amri nyingine Aprili 4. Tangu wakati huo amekuwa akitafutwa hadi jana alipokamatwa.

Amri ya wawili hao kukamatwa na kupelekwa gerezani ilitolewa baada ya kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama ambayo iliwaamuru kumlipa mhadhiri wa dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, Sh250 milioni baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Baada ya kukamatwa jana, Babu Tale alifikishwa mahakamani saa tisa alasiri kwa ajili ya hatua zaidi.

Hata hivyo, naibu msajili wa Mahakama aliyetoa amri ya kumkamata hakuwepo hivyo alirudishiwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi hadi leo asubuhi atakapopelekwa tena mahakamani kwa hatua zaidi.

Hukumu iliyoamuru Babu Tale na nduguye kulipa fedha ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, 2016 katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013 iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde.