Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ATM YA WIKI: Ed Sheeran Kuimba anajua, maokoto kama kawa

ED Pict

Muktasari:

  • Sheeran ni muimbaji wa muziki aina ya Pop na katika orodha hiyo anayeongoza ni Taylor Swift na Beyonce walioingiza zaidi ya Dola 150 milioni.

LONDON, ENGLAND: KATIKA orodha ya waimbaji waliokunja pesa ndefu mwaka jana, Ed Sheeran anashika namba tatu.

Sheeran ni muimbaji wa muziki aina ya Pop na katika orodha hiyo anayeongoza ni Taylor Swift na Beyonce walioingiza zaidi ya Dola 150 milioni.

Staa huyu ambaye ana umri wa miaka 33, anakadiriwa kuingiza jumla ya Dola 130 milioni mwaka jana kiasi ambacho kimezidi kumfanya awe tajiri zaidi. Hapa tumekuletea mali na utajiri wake anaomiliki hadi sasa.


ED 05

ANAPIGAJE PESA

Muziki wake ndiyo kitu cha kwanza kumwingizia pesa kutokana na shoo mbalimbali anazofanya kote duniani. Pia anaingiza pesa kutokana na malipo ya mtandao wa YouTube na mitandao mengine ya kijamii na kwa jumla kwa mwaka anapata zaidi ya Dola 1 milioni.

Kwa mujibu wa tovuti ya Celebrity Networth, kwa mwaka msanii huyu anakadiriwa kuingiza kati ya Dola 100 milioni hadi Dola 200 milioni na mwaka wake wa mafanikio zaidi ni mwaka 2017 alipofanya ziara  yake ya Ed Sheeran's Divide Tour iliyomwingizia Dola 775 milioni.

Vile vile staa huyu ni balozi wa kampuni ya Dunlop Manufacturing, Hoax na Nando na kwa pamoja humpa zaidi ya Dola 20 milioni kwa mwaka, pia anapata pesa kwa kuwaandikia wasanii mbalimbali mashairi ya nyimbo.

Dili lake kubwa la udhamini ni lile la kampuni ya Heinz ketchup ambalo humpa kiasi kinachofikia Dola 10 milioni kwa mwaka kwa kuitangaza. Kijumla anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 200 milioni.


ED 01

MJENGO

Ana nyumba mbili, moja ni ile anayoishi huko Suffol, England tangu mwaka 2011, nyingine aliinunua mwaka 2014 maeneo ya Notting Hill, London na zote zinakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 10 milioni.


ED 02

NDINGA

-Rolls Royce Cullinan-Dola 355,000

-Ferrari 812 Superfast-Dola 433,765

-Mini Cooper S-Dola23,400.

-Audi Q7-Dola 90,200

-Mercedes-AMG G63-Dola 180,150

-Bentley Bentayga-Dola 263,000

-Aston Martin DB9-Dola 203,000

-Range Rover SV Autobiography-$216,675

-Ferrari 488 GTB-Dola 262,647

-Lamborghini Gallardo Spyder-Dola 251,600


ED 04

MSAADA KWA JAMII

Anafanya kazi kama balozi wa taasisi ya GRAMMY Foundation, Musicians on Call na Elton John AIDS Foundation ambazo husaidia jamii hususan watu wasiojiweza na wenye uhitaji wa matibabu.

Pia amekuwa akitoa misaada ya kupambana na magonjwa ya Ukimwi, kansa na utoaji wa elimu kwa watoto.


ED 03

MAISHA NA BATA

Aliwahi kuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki kutoka Scottland Nina Nesbittkabla kabla ya kuachana mwaka 2012.

Baada ya hapo aliingia kwenye uhusiano na Athina Adrelos kuanzia mwaka 2014 hadi 2015.

Julai 2015, alianzisha uhusiano na rafiki yake wa utotoni Cherry Seaborn ambaye mwaka 2018 walitangaza kuvishana pete na wakaoana kwa siri mwaka uliofuatia. Hadi sasa wamebahatika kupata watoto wawili.