Alikiba, Hamonize habari mpya mjini

Alikiba, Hamonize habari mpya mjini

Muktasari:

  • Picha aliyoposti msanii Harmonize kwenye kurasa wake wa Instagram akiwa na mfalme wa Bongofleva Alikiba imekuwa gumzo.

PICHA ya pamoja waliopiga wasanii wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’ na Ally Saleh ‘Kiba’ katika mitandao imekuwa ndio habari mpya mjini.

Harmonize aliweka picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram akiwa pamoja na Kiba kwenye ndege wakielekea jijini Mwanza.

Watu mbalimbali katika mtandano huo wameiweka katika kurasa zao na kuuliza maswali mengi kama kutakuwa na jambo lingine baada ya picha hiyo.

Msanii huyo baada ya kuweka picha alisindikiza na maneno aliyoandika;” Konde Gang Fc ndani ya Mwanza, tafadhali twende kwa mfalme Alikiba kesho.”

Msanii kutoka Angola, Cabo Snoop aliandika katika sehemu ya kujibu;”Wasanii wakubwa Tanzania katika picha moja.”

Naye msanii wa Hip Hop nchini, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’ aliweka picha ya wasanii hao na kuisindikiza na ujumbe; ”Haya ndio mambo ambayo tunapenda kuyaona.”

Ikumbukwe Harmonize mara kwa mara amekuwa akimuimba vizuri Alikiba na kwenye wimbo wake wa Teacher ameweka mstari unaosema;”Na mwanangu wa Cinderella hapendagi makiki”.

Alikiba leo atakuwa na shoo yake Mwanza huku upande wa Harmonize yeye akiwa na shughuli zake zingine.