Abby anogesha shindano la klabu za kodi TRA

MSANII wa kizazi kipya Abby Chams amenogesha shindano la klabu za kodi kwa shule za Sekondari lililofanyika leo Novemba 09 katika chuo cha kodi Dar es salaam (ITA).
Chams ambaye ameshawahi kutamba na nyimbo mbali mbali ikiwemo 'NANI' aliyoshirikiana na Marioo, aliteka ukumbi kwa zaidi ya dakika 10 kutokana na utumbuizaji wake.
Shindano hilo ambalo limehusisha klabu za kodi kutoka jumla ya shule za Sekondari 59, Pwani na Dar es salaam lilikuwa na vipengele mbali vilivyokuwa vikishindaniwa ambavyo ni Uandishi wa isha zinazohusiana elimu ya kodi, ukusanyaji wa risiti, uwasilishaji wa mada na kipengele cha maswali na majibu ambacho kilijumuisha shule zote.
Mashindano haya yalianzishwa mwaka 2008 chini ya mamlaka ya mapato Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), lengo likiwa ni kutoa elimu ya kodi kwa wanafunzi ambao wanaamini ndio walipa kodi wa kesho.
Shule zilizoibuka kidedea kwenye vipengele mbali mbali zilijinyakulia zawadi za pesa taslimu, kompyuta, printa, medali, vikombe na mabegi.