Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MUSIC FCTS: Dogo Janja amkabidhi Aslay kibunda cha dola

Dogo Janja amkabidhi Aslay kibunda cha dola

ANAFANYA kazi zake chini ya Manzese Music Baby (MMB) yenye wasanii watatu. Miaka yake 10 ndani ya Bongofleva aliweza kurekodi nyimbo 421, huku akifanya shoo 1,562 kwa mashabiki wake wa ndani na nje.

Huyu ni Dogo Janja ambaye ametoa albamu mbili ‘Mtoto wa Uswazi na Asante Mama’ ambayo asilimia 90 amewashirikisha wasanii wa kike. Bongo Music Facts inakuja zaidi:

1. Licha ya kuwa mtu mzima kwa sasa, Dogo Janja hawezi kubadili jina la lake ‘Dogo’ kwa kile anachoamini kama “Forever Young” na hata akifanya hivyo, kibiashara sio nzuri kwani atapoteza mashabiki.


2. Kuna video mbili tu ambazo Dogo Janja ametokea akiwa amevaa sare za shule, video ya kwanza ni ‘Shikamoo Mwalimu’ aliyoshirikishwa na Easy Muchwa na video ya pili ni ‘Kusoma’ aliyoshirikishwa na Dogo Sheby.


3. Video ya harusi ya Dogo Janja na Irene Uwoya imetazamwa zaidi kuliko video za nyimbo zake zote katika mtandao wa YouTube, video hiyo imetazamwa zaidi ya mara milioni 3.1.


4. Dogo Janja alishawahi kutaka kujirusha kwenye gari kisa kuzinguliwa kwenye mapenzi, ni kipindi ambacho hajafunga ndoa na Irene Uwoya ambaye naye walikuja kuachana.


5. Wimbo pekee ya Dogo Janja kufanyiwa remix ni My Life, remix ya ngoma hiyo aliwashirikisha Radio na Weasel ambao walikuwa wanaunda kundi la Goodlyfe kutokea nchini Uganda.


6. Rayvanny amechangia kwa kiasi fulani kuandika wimbo wa Dogo Janja, My Life uliorekodiwa MJ Records, ni ngoma ambayo ilimrejesha Janjaro kwenye muziki baada ya kupotea kutokana na kuzinguana na Madee.


7. Wimbo wa Bongofleva ambao Dogo Janja anapenda kuusikiliza zaidi ni ‘Dunia Njia’ wa Bushoke, ngoma hii huisikiliza sana kipindi ambacho anakuwa katika wakati mgumu kimaisha au akiwa amechukizwa na jambo.


8. Licha ya kukaa ndani ya familia ya Tip Top Connection kwa kipindi kirefu, Dogo Janja hajawahi kusikika katika ngoma yoyote iliyowakutanisha wasanii wa Tip Top kama kundi.


9. Aslay ndiye msanii ambaye amewahi kutunzwa fedha nyingi zaidi na Dogo Janja wakati akitumbuiza jukwaani ambapo alipatiwa Dola1,400 wastani wa Sh3.2 milioni.


10. Wimbo wa Dogo Janja, Ngarenaro ndio wimbo wa kwanza kutoka katika studio ya Rayvanny, Surprise Music iliyokuwa inasimamiwa na Prodyuza Rash Don, sasa ipo chini ya Next Level Music (NLM) ambayo ni lebo ya Rayvanny.