STRAIKA WA MWANASPOTI : Ufisadi uliopo Chapa Dimba, Safaricom uchunguzeni

Muktasari:

  • Swali kwa Safaricom. Najua mko katika maofisinimambo mbalimbali.
  • Kitu ambacho hamfahamu ni kuwa hamna la maana kwa kinachofanyika na haya mashindano yenu.

Nairobi.Mashindano ya chapa Dimba yanayo dhanaminiwa na kampuni ya Safaricom nchini Kenya. Ni mashindano ambayo kwangu sioni umuhimu wowote wa hayo mashindano. Ni mashindano ambayo yamejaa mambo yasiyokuwa ya kimaadili kabisa ya michezo. Ni mashindano ambayo ni kama hayana madhumuni kabisa.

Kampuni ya Safaricom ndio wanaoendesha mashindano hayo na shida kubwa wameacha mashindano hayo kwa watu ambao wengi wao kazi yao bora mpira. Sio mpira bora.

Kitu cha kuudhi ni kwamba tunalia kila siku tunataka kujenga soka letu Kanda hili la Afrika Mashariki.

Lakini tutalijenga vipi na ni mafisadi tuu wengi ambao tumewajaza katika soka letu. Cha kwanza kabisa, kwa mimi sijui madhumuni ya Safaricom kuanzisha mashindano hayo.

Mimi mwenyewe kama mdau wa soka nchni Kenya sitaweza kunyamaza nikiona mambo ya ajabu yakifanyika nchini. Kitu cha kushangaza ni kuwa hata walewale waliocheza soka nchini Kenya wakajua taabu ambazo wachezaji hupitia wengi wao ndio walewale wajiunga na hao wasiio waadilifu wakubwa kuangamiza soka letu.

Swali kwa Safaricom. Najua mko katika maofisinimambo mbalimbali.

Kitu ambacho hamfahamu ni kuwa hamna la maana kwa kinachofanyika na haya mashindano yenu.

1: Mlianzisha mashindano haya kwa madhumuni gani? Nakumbuka mlisema kila timu itakuwa inapata mipira na vifaa vya matumizi kama bibs vile.

Ndugu zanguni iwafikie katika hizo ofisi zenu. Hakuna lolote linalofanyika.

Mipira hakuna na ilishapangwa kuwepo. Viongozi waliopewa majukumu ya kuendesha mashindano hayo ndio wanaojifahidi na hiyo mipira.

2: Bora soka ichezwe. Ni vibaya sana kulazimisha wachezaji kucheza mechi nne kwa siku moja. Mchezaji anahitaji nguvu ya kucheza soka.

Mchezaji anahitaji kula ili arejeshe nguvu ambazo alipoteza katika mechi zile za kwanza. Mechi nne kwa siku ndugu zanguni na bila hata lishe ni balaa. Mnapeana glucose pekee, ifanye nini?

3: Kwangu nilifikiria mko na jopo la kuchagua wachezaji wale wazuri na kuwaweka kambini. Ama angalau kuwapa mafundisho ya siku kadhaa baada ya mashindano. Hawa Ni watoto wadogo.

Chini ya miaka 20. Inaudhi, kisa na maana mko na kila kitu lakini ya kuwezesha mashindano hayo kuwa bora zaidi lakini hamshulikii mashindano hayo. Mmeacha mashindano hayo kwawatu wasio na uchungu wa soka. Na siogopi kuwaambia ukweli.

Nashindwa kufahamu mbona asilimia 70-80 ya zile Pesa mmetoa zinaingia kwenye mifuko ya wachache?

Itakuwaje hata senti hata moja hainufaishi wanao ng’ang’ana viwanjani?

Watoto wanashinda njaa. Pesa zinaingia mifukoni mwa wanaondesha ama wasimamizi wa mashindano hayo.

Kazi bora wameandikisha siku. Hawataki kujua kulikoni kwa klabu ambazo zimeleta wachezaji wao. Klabu zinatoka mkono mtupu.

Itakuwaje mnanzisha mashindano bila kuleta vifaa kamili ambavyo vinafaa kutumiwa. Haya mambo ya kuwavalisha vijana bibs za Safaricom wapige nazo picha halafu mnazichukua inafaa ikome.

Mipira hadi waleo hakuna. Mnaendesha aje mashindano yanayo fanyika nchi nzima bila kuwa na utaratibu unaoeleweka? Wachezaji wanalazimishwa kucheza soka gizani. Itakuwaje refa kipindi cha kwanza kachezesha mechi dakika 20 badala ya dakika 30. Kipindi cha pili dakika 9 badala ya dakika 30. Kamaliza Mpira kwa giza.

Kapeleka matokeo. Badala ya mechi kurudiwa? Safaricom muangalie hilo Jambo ama kila kukicha nitawaambia ukweli hadi siku ya kiyama. Ufisadi ambao umejaa katika haya mashindano yenu, unafaa kuchunguzwa. Ni lazima mfanye jambo la sivyo...afadhali hizo pesa mkapeleke kwa vyumba vya watoto mayatima kote nchini. Hakuna haja ya hizo hela kupotelea katika matumbo za watu hapa nchini.

Wakati mwingine nashangaa sana maana watu waliocheza soka hapa nchini natarajia wasaidie katika kuendeleza soka letu humu nchini lakini unapata ni hao hao ndio wako katika mstari wa mbele kuangamiza soka letu.

Sijui sijui sijui. Sijui nitafanya nini?

Na mjue hizi ni hela za watu mnakula. Pale kuna mayatima, kuna wale hata hawajui wazazi wao wako wapi? Kuna wale wanatafuta kazi,hilo ndio lisho lao na unawanyanyasa,na kadhalika. Vilio vyao ndungu zanguni vitafikia Maulana Mwenyezi Mungu.

Hiyo siku mtajua hamjui. Langu la Mwisho na lifikie mkurugenzi wa Safaricom PLC, Watu umeeka kuendesha mashindano ya Safaricom Chapa Dimba wengi wao ni mafisadi wakubwa wa soka nchini Kenya. Sina la ziada.

Kinachotakiwa ni mabosi wa Safaricom kwenda viwanjani kuona nini kinafanyika kuliko kusubiri au kuangalia kwa mbali na kwa magazeti bila kuona kinachoendelea huko.

Wakiona ninaamini watasikitia fedha wanazotoa kweli zinalingana na kinachofanyika? Kweli waamuzi na mipira vinatolewa kwa wakati unaotakiwa, vinginevyo waliopo nasema watawaharibia mashindano yenu ambayo nilishaanza kuyatoa thamani yake.

Ni hayo tuu kwa leo.