Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga wagoma kutoa kibali cha Morrison

YANGA imesema haiwezi kutoa kibali cha kazi cha winga Bernard Morrison kwani ni mchezaji wao hivyo  wanaishangaa Wizara ya Kazi kuwalazimisha kutoa kibali hicho.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema wana mkataba na Morrison hivyo hawaoni haja ya kurudisha kibali cha kazi cha mchezaji huyo wakati bado wana kesi nae

"Sisi hatujazuia ila tunacho kibali chake cha kazi. Wamekuja Wizara ya Kazi wameleta barua wakitaka turudishe kile kibali ila tumewajibu hatuwezi kurudisha kwani Morrison ni mchezaji wetu tuna mkataba naye na tuna shauri nae.

"Tunashangaa wameshapita makocha hapa wameondoka na hatujawahi kuulizwa na Serikali kuhusu kurudisha vibali, huwa tunarudisha wenyewe, sasa iweje kwa Morrison, ana ushawishi gani?" amesema Bumbuli.

Ameongeza; "Hatujazuia wala hatuna sababu ya kuzuia kwani hata Simba wametuomba uhamisho wa Morrison kwa njia ya barua na njia ya mtandao na tumewaambia kuwa huyu hatujamalizana nae,"

Morrison ambaye aliichezea Yanga msimu uliopita amezua utata mkubwa wa usajili baada ya hivi karibuni kusaini Simba.

Mchezaji huyo alikana kusaini mkataba mpya na Yanga na kudai saini yake imeghushiwa hivyo kupeleka malalamiko Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti Elias Mwanjala ilimpa ushindi Morrison wakidai kweli mkataba halisi wa mchezaji huyo ulikuwa na saini moja tu ya viongozi wa Yanga na haukuwa na saini ya mchezaji huyo, hivyo kumruhusu kucheza timu yeyote.

Wakati hukumu hiyo ikitoka, tayari Morrison alikuwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba na ametambulishwa rasmi wakati wa Simba Day kuwa miongoni mwa nyota watakaoitumikia timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza Septemba 6 mwaka huu.