Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Simba wataja mambo matatu

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Mechi ya mwisho ya msimu huu ni dhidi ya Yanga, wapinzani wao wa jadi.

MIAKA mitatu ya maumivu ya kupoteza taji la Ligi Kuu Bara mbele ya macho baada ya safari ndefu ya mechi 29 za ligi hiyo, Simba imefika mwisho wa njia sehemu ambayo ama izaliwe upya kama bingwa wa msimu wa 2024/25 au izamishwe tena.


Mechi ya mwisho ya msimu huu ni dhidi ya Yanga, wapinzani wao wa jadi. Hii ni Dabi ya Kariakoo ambayo inatarajiwa kupigwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar ikibeba taswira na mitazamo mingi ndani yake ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.


Lakini, katikati ya mateso ya kutonyanyua makombe ya ligi kwa kipindi kirefu, Simba itakuwa na neema ya kuwa na mastaa matata katika kikosi chake, na kwenye mstari wa mbele wa vita hiyo yupo Steven Mukwala, mshambuliaji kiongozi aliyeibeba timu hiyo kwa kutupia mabao 13 msimu huu sawa na Leonel Ateba.

“Hatupambani kwa pointi tu, tunapigania hadhi ya klabu, tunapigania historia yetu, tunapigania mashabiki wetu waliovumilia miaka mitatu ya maumivu,” anasema Mukwala akizungumzia mechi hiyo.

Katika mechi iliyopita dhidi ya Kagera Sugar, Mukwala alifunga bao moja, na sasa anaapa kuipigania Simba hadi tone la mwisho la jasho kuhakikisha wanashinda dhidi ya Yanga.

“Tunajua mashabiki wanatufuatilia. Tunajua wana imani nasi. Sasa ni zamu yetu kurudisha upendo huo kwa kuwapigania. Siwezi kusema mengi, lakini naahidi tutapambana kwa damu na jasho,” ameongeza.

Kwa upande wake nyota raia wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua ambaye amekuwa injini ya Simba akiongoza orodha ya wafungaji Ligi Kuu Bara akifunga mabao 16, ameonyesha kuihitaji mechi hiyo.

“Tutafanya kila ambacho kitawezekana kwa ajili ya mashabiki wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono. Binafsi sina presha na nipo tayari kwa mchezo huo mkubwa, itakuwa ni heshima kwetu kumaliza msimu na ubingwa wa ligi," amesema nyota huyo.

Kwa mujibu wa takwimu, Simba imepoteza mechi nne mfululizo dhidi ya Yanga, tatu za Ligi Kuu Bara na moja ya Ngao ya Jamii.

Na kwa mujibu wa Kocha Fadlu Davids, huu ni wakati wa kulipa kisasi kwa niaba ya klabu, wachezaji na mashabiki waliovumilia mateso kwa misimu mitatu mfululizo, huku mastaa wa timu hiyo, Jean Charles Ahoua na Steven Mukwala wakitaja mambo matatu.

“Tumepoteza mataji matatu mfululizo. Lakini sasa, baada ya miezi kadhaa ya kazi ngumu, tuna nafasi ya kuwa mabingwa kwa kushinda mechi moja. Ni jambo kubwa mno,” amesema Fadlu.

Katika msimamo wa ligi, Yanga inaongoza kwa pointi 79, Simba ikifuatia kwa 78. Mabao ya Yanga ni 81, ya Simba ni 69. Yanga imefungwa mara 10, Simba mara 11. Tofauti ni pointi moja tu.

“Kama mtu angeniletea karatasi wakati nakuja na kuniambia ‘Kocha, kuna mechi moja tu mwishoni mwa msimu itakayoamua ubingwa,’ ningesaini papo hapo. Hii ndiyo hiyo mechi. Ni sasa au kamwe.”

Mara ya mwisho Simba kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga ilikuwa Agosti 13, 2023 kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya kutoka suluhu ndani ya dakika tisini, hiyo ilikuwa ni mechi ya Ngao ya Jamii.