Molinga: Hakuna kama Shikhalo

Kipa wa Yanga, Farouk Shikhalo

Muktasari:

Molinga alisajiliwa msimu huu na Kocha Mwinyi Zahera na tangu ajiunge na timu hiyo ameifungia jumla ya mabao 13 ya mashindano, yakiwamo mawili ya Kombe la FA na 11 ya Ligi Kuu Bara.

STRAIKA wa Yanga, David Molinga amesema katika mwaka wake wa kwanza Tanzania kama atatakiwa kuchagua kipa bora basi kura yake itakwenda kwa Farouk Shikhalo.

Molinga amesema hakuna hatua ngumu kama kumfunga Shikhalo kutokana na ubora wake akiwa langoni.

Molinga ambaye ameibuka Mfungaji Bora wa kikosi cha Yanga akiwa na mabao 11 amesema bado anashangaa kwanini Shikhalo amekuwa hapewi nafasi ya kutosha katika kikosi chao cha Yanga.

"Mimi kwangu kipa bora ni Shikhalo watu hawajui tu huyu ni kipa bora sana anajua sana kusumbua washambuliaji akiwa langoni ni ngumu sana kumfunga," amesema Molinga.

"Nilidhani ni mimi peke yangu naona hivi lakini ukiona mchazaji mkubwa kama Deo Kanda naye anamkubali Shikhalo utaamini ninachosema.

Aidha Molinga amesema ubora mkubwa ambao Shikhalo anajitofautisha na makipa wengine ni jinsi anavyoongea uwanjani lakini zaidi anavyoweza kucheza kwa miguu kuokoa mashambulizi.

"Makipa wachache sana wanaweza kuongea uwanjani kupanga timu kama Shikhalo ni mabeki wamekuwa wanashindwa kuzingatia lakini kipa gani anaweza kucheza na miguu hapa Tanzania kama Shikhalo?

"Ni vigumu sana kumfunga Shikhalo kama nilivyomfunga kipa wa Lipuli anajua kucheza na hesabu za washambuliaji  kama vile."