Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkongomani kumchomoa Diao Azam FC

MCONGO Pict
MCONGO Pict

Muktasari:

  • Azam FC ikiwa na mpango wa kunasa saini hiyo, inaelezwa anakwenda kuchukua nafasi ya Alassane Diao ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

UONGOZI wa Azam FC upo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AC Rangers ya Congo, Enock Lihonzasia.

Azam FC ikiwa na mpango wa kunasa saini hiyo, inaelezwa anakwenda kuchukua nafasi ya Alassane Diao ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Azam FC kimeliambia Mwanaspoti kuwa usajili wa mshambuliaji huyo ni pendekezo la kocha mpya, Florent Ibenge anayetajwa kuchukua nafasi ya Rachid Taoussi.

“Ni kweli tupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo yakiwa ni mapendekezo kutoka kwa kocha Ibenge ambaye ndiye atakayekuwa anakinoa kikosi chetu msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza:

“Enock Lihonzasia ni mbadala wa Diao ambaye tayari tumemalizana naye, hatakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao.”

Diao alijiunga na Azam Julai 4, 2023, wakati timu hiyo ikinolewa na kocha Youssouph Dabo.

Azam FC ambayo tayari imekata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara, imeripotiwa kufanya usajili wa wachezaji wawili hadi sasa.

Nyota waliosajiliwa ndani ya kikosi cha Azam FC ni kipa Aishi Manula ambaye amemaliza mkataba na Simba msimu huu. Mwingine ni mshambuliaji, Muhsini Malima akitokea Zed FC ya Misri ambaye pia amewahi kuitumikia Coastal Union na Dodoma jiji.