Zahera: Juma Abdul bado hayupo fiti kuanza Yanga

Muktasari:

Abdul anakazi kubwa ya kufanya kuhakikisha anamshawishi mwalimu kumpanga kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga Tanzania akichuana na Ally Ally na Paul Godfrey.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga Tanzania, Mwinyi Zahera ametoa sababu za kushindwa kumtumia katika kwanza beki Juma Abdul bado hajawatayari kutokana na kukosa nafasi ya kucheza muda mrefu.

Abdul ajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza tangu kutua kwa kocha huyo ambaye amekuwa akimtumia zaidi Paul Godfrey 'Boxer' ambaye sasa ni majeruhi na nafasi hiyo sasa imekuwa ikichezwa na Ally Ally.

Akizungumza na Mwanaspoti, Zahera akiri Abdul ni mchezaji mzuri, lakini hana kasi inayoendana na namna timu yake inavyotakiwa kucheza hivyo ameamua kumpa muda zaidi wa kujifua ili aanze kumtumia.

"Unajua mashabiki wao wanataka kuwa makocha wapange wao kikosi mimi ndiye ninayekaa na wachezaji muda mwingi hivyo nafahamu nani ni bora zaidi ya mwingine Juma msimu uliopita ajacheza michezo mingi wachezaji ninaowapa nafasi wamecheza wakiwa katika timu zao," alisema Zahera.

"Sina maana kwamba ni mchezaji mbaya hapana ni mzuri na amekuwa akipambana kusaka nafasi ya kucheza muda ukifika atapana nafasi hiyo kwasasa naomba majukumu yangu niachiwe mwenyewe nisiingiliwe," alisema na kuongeza kuwa.

"Mpira wa Tanzania unaendeshwa na ushabiki wao wakipata matokeo wanasahau kabisa kuwa waliocheza ni wachezaji wasiowapenda wakikosa matokeo pia hawakosi kitu cha kuzungumza," alisema Zahera.