Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zubimendi, Norgaard kuwahi pre-season Arsenal

Muktasari:

  • Usajili wa Arsenal ambao imefanya hadi sasa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ni kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga, ambaye imekubali kulipa Pauni 5 milioni ili kununua mkataba wake, akienda kuwa msaidizi wa namba moja, David Raya.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL ina matumaini makubwa kwamba itakamilisha dili la usajili wa Martin Zubimendi na  Christian Norgaard kwa wakati kabla ya kuanza kambi ya pre-season huko Hispania, wiki ijayo.

Usajili wa Arsenal ambao imefanya hadi sasa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ni kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga, ambaye imekubali kulipa Pauni 5 milioni ili kununua mkataba wake, akienda kuwa msaidizi wa namba moja, David Raya.

Lakini, Zubimendi uhamisho wake wa Pauni 51 milioni kutoka Real Sociedad upo kwenye hatua za mwisho kabla ya kutangazwa.

Na wa staa wa Brentford, Norgaard nao haupo mbali baada ya vipimo vya afya vya kiungo huyo kufanyika na atagharimu Pauni 10 milioni na nyongeza nyingine.

Kama mambo yatakwenda vizuri, viungo hao wawili wote watajumuishwa kwenye ndege ya pamoja ya mastaa wa Arsenal ambao watakwenda kwenye hali ya hewa ya joto huko Hispania kwa ajili ya kufanya mazoezi kabla ya kuanza kwa ziara yao ya mazoezi huko Singapore na Hong Kong kuanzia Julai 19.

Beki Takehiro Tomiyasu amesitisha mkataba wake kwenye timu hiyo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi mfululizo, huku akiondoka mkataba wake ukiwa umebakiza mwaka mmoja. Mjapani huyo alisema dakika sita tu msimu uliopita, huku maumivu ya goti yalimweka nje ya uwanja muda mrefu.

Wakati huo huo, straika Viktor Gyokeres amegomea ofa za kubaki Sporting CP akitaka kwenda kujiunga na Arsenal kwenye dirisha hili. Juventus nayo ilimtaka straika huyo, ambaye amegoma ili tu akajiunge na Arsenal na hivyo kuifanya miamba hiyo ya Turin kumsajili Jonathan David.

Kwenye ishu ya straika, Arsenal pia inamfukuzia mkali wa RB Leipzig, Benjamin Sesko - ambapo itaamua kupambana kupata saini yake kama watakwama kwa Gyokeres, ambaye alifunga mabao 54 katika mechi 52 alizochezea Sporting msimu uliopita.

Arsenal ipo sokoni pia kusaka mawinga na kwenye hilo mkali wa Crystal Palace, Eberechi Eze jina lake limewekwa ubaoni huku bei yake ikitajwa kuanzia Pauni 68 milioni na kama kocha Mikel Arteta atakwamba huko atahamia kwa winga wa Chelsea, Noni Madueke.