Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sporting, Gyokeres mambo yazidi kuwa mabaya

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo anaweza kujaribu kulazimisha uhamisho kwenda Ligi Kuu England kwa kutofika katika kikao cha kwanza kuelekea mazoezi ya msimu mpya kwenye makao makuu ya timu hiyo ya zamani ya Cristiano Ronaldo.

LISBON, URENO: MABOSI wa Sporting Lisbon wana hofu kuwa staa wao anayewindwa na  Arsenal, Viktor Gyokeres, ataendelea kushikilia msimamo wake wa kutojiunga na timu na hatohudhuria mazoezi leo, Jumatatu ikiwa ni sehemu ya kushinikiza aruhusiwe kuondoka.

Mshambuliaji huyo anaweza kujaribu kulazimisha uhamisho kwenda Ligi Kuu England kwa kutofika katika kikao cha kwanza kuelekea mazoezi ya msimu mpya kwenye makao makuu ya timu hiyo ya zamani ya Cristiano Ronaldo.

Gyokeres ambaye ni raia wa Sweden anayewindwa pia na Manchester United na Juventus, anataka sana kujiunga na Arsenal na anadai kuwa Sporting imevunja makubaliano waliyoweka Januari mwaka huu ya kumruhusu aondoke kwa pauni 60 milioni.

Sporting inafahamu kwamba timu nyingi zina uhitaji mkubwa wa huduma ya nyota huyo na inataka angalau pauni 68.5  milioni ili kumuuza.

Awali, Rais wa Sporting, Frederico Varandas  ambaye amekuwa na mvutano wa wazi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Coventry  alihisi kuwa tishio la Gyokeres kutohudhuria mazoezi ni la muda mfupi tu na sio kama amedhamiria sana na alitarajia atarudi jijini Lisbon Jumapili ili kujiunga na kikosi Jumatatu lakini hadi kufikia jana mchana bado hakuwa amerudi.

Gyokeres alipatiwa muda wa ziada wa mapumziko baada ya majukumu ya kimataifa na timu ya taifa ya Sweden mwezi uliopita wakati wenzake wakiwa wameshaanza mazoezi wiki moja kabla.

Vyanzo vya Ureno vimeiambia tovuti ya The Sun kuwa Gyokeres, ambaye alifunga mabao 54 katika mechi 52 msimu uliopita, huenda akakosa kabisa kuripoti kambini.

Inaelezwa fundi huyu amechukizwa na jinsi viongozi wa timu wanamfanyia.

Gyokeres amekataa ofa za pesa nyingi kutoka kwa timu za Saudi Pro League kama Al-Qadsiah na Al-Hilal, waliokuwa tayari kumlipa mamilioni ili ajiunge nao katika dirisha hili.

Fundi huyu amekataa ofa hizo kwa sabau bado anataka kucheza kwenye Ligi Kuu England.

Rais wa Sporting, Varandas amesema hawawezi kupokea ofa ya pauni 60 milioni ahata ikiwaje na watazingatia ofa zitakazoanzia walau pauni 68 milioni.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anahitaji mshambuliaji mpya na katika orodha yake ana wawili ambao ni Gyokeres na Benjamin Sesko wa RB Leipzig na anataka mchezaji mmoja kati yao asafiri naye kwenda Singapore kwa ajili ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya Julai 19.

Nyota wa Frankfurt Hugo Ekitike na aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City, Julian Alvarez (ambaye kwa sasa yuko Atletico Madrid), pia wanaangaliwa.