Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Mzambia atoka hospitali baada ya kuzirai uwanjani

Muktasari:

  • Banda alianguka ghafla dakika tano kabla ya mchezo kumalizika baada ya kupigwa kwa nguvu kifuani na mpira na alibaki bila kusogea wakati mchezo uliposimama, hali iliyosababisha madaktari kuingia uwanjani haraka kutoa huduma ya kwanza.

NAPOLI, ITALIA: Winga wa Zambia, Lameck Banda, amerejea nyumbani salama baada ya kupata tatizo la moyo wakati wa mechi ya Serie A kati ya Lecce na Napoli.

Banda alianguka ghafla dakika tano kabla ya mchezo kumalizika baada ya kupigwa kwa nguvu kifuani na mpira na alibaki bila kusogea wakati mchezo uliposimama, hali iliyosababisha madaktari kuingia uwanjani haraka kutoa huduma ya kwanza.

Kocha wa Napoli, Antonio Conte, aliwatahadharisha haraka madaktari wa Lecce, huku wachezaji wa timu zote mbili pia wakitoa ishara ya kuomba msaada wa haraka.

Banda alitolewa uwanjani kwa machela na mchezo kusimamishwa kwa muda. Mashabiki waliokuwapo uwanjani walipiga makofi wakati akipelekwa kwa wahudumu wa afya kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Lameck Banda ameondoka katika Hospitali ya Cardarelli asubuhi ya leo baada ya kufanyiwa vipimo kadhaa na majibu yote kuonyesha hana tatizo kubwa,” ilisema taarifa rasmi ya Lecce.

Klabu hiyo ilithibitisha Banda amerejewa na fahamu na ataendelea kufanyiwa vipimo zaidi ili kutathmini kikamilifu hali yake ya kiafya.

Tukio hilo limekuwa la kutisha katika msimu huu wa Serie A na limeonyesha hatari ambazo wachezaji hukumbana nazo wanapocheza mechi zenye ushindani mkubwa.

Kupona kwa Banda kumewapa faraja mashabiki, wachezaji wenzake na wadau wa soka kwa jumla.

Msimu huu, Banda amekuwa mchezaji muhimu kwa Lecce, akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao katika mechi 23 za Serie A, akionyesha kiwango bora katika timu na kuwa na mchango mkubwa katika kushambulia.

Mashabiki na wachezaji wenzake pia wametuma salamu za kumuunga mkono katika mitandao ya kijamii, wakifurahia kusikia ameruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea kuimarika.