Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye Rumble in the Jungle wametuacha

Muktasari:

  • Bondia huyo mashuhuri, bingwa mara mbili wa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu, amefariki dunia akiwa mwenye amani akizungukwa na familia yake, Ijumaa iliyopita.

LAS VEGAS, MAREKANI: GWIJI wa masumbwi, George Foreman amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76, familia yake imethibitisha.

Bondia huyo mashuhuri, bingwa mara mbili wa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu, amefariki dunia akiwa mwenye amani akizungukwa na familia yake, Ijumaa iliyopita.

Moja ya mapambano yake maarufu aliyopigana Foreman ni lile la Rumble in the Jungle alilopigana na bondia mashuhuri zaidi, Muhammad Ali huku ikielezwa hilo ni pambano la kihistoria lililowahi kutokea kwenye mchezo wa masumbwi. Pambano hilo la masumbwi linaelezwa kama tukio bora kabisa la kukumbukwa la michezo lililowahi kutokea kwenye karne ya 20.

Bondia Ali, naye alifariki dunia 2016, hivyo mabondia wote hao wawili waliotengeneza historia hiyo ya kukumbukwa kwenye mchezo wa masumbwi wahapo tena duniani.

Ripota mmoja wa masumbwi, ambaye bado yupo hai na aliripoti pambano hilo lililopigwa Kinshasa, Colin Hart anasimulia: “Pambano limefanyika nusu karne iliyopita, lakini hadi sasa ukisema tu Rumble in the Jungle kuanzia Angola hadi Zanzibar, watu wengi watakuwa wanafahamu unazungumzia kitu gani.

“Hakuna ubishi ni pambano lililoandikwa na kuzungumza mara nyingi zaidi, kwa sababu lilianza kuzungumzwa miezi tisa kabla. Rais wa Zaire, Mobutu Sese Seko aliweka pesa yake na kila bondia alilipwa Dola 5 milioni.”

Taarifa kutoka kwa familia ya bondia George kupitia ukurasa wa Instagram ilieleza: “Mioyo yetu imevunjika. Kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha kipenzi chetu George Edward Foreman Sr. aliyefariki kwa amani kabisa Machi 21, 2025 akizungukwa na wapenzi wake.”

Bondia Mike Tyson alituma salamu za pole baada ya kifo hicho, akiposti picha yake aliyopiga akiwa pamoja na Foreman na kuandika hivi: “Pole zangu kwa familia ya George Foreman. Mchango wake kwenye masumbwi umepitiliza na hautasahaulika.”

Foreman ambaye ni gwiji wa muda wote wa masumbwi Hall of Fame, alikuwa mmoja wa mabondia waliokuwa wakipiga ngumi hatari sana waliowahi kutokea duniani. Alishinda ubingwa wa dunia mara mbili katika kipindi cha miaka 30 ya ubondia.

Bado anashikilia rekodi ya kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu aliyekuwa na umri mkubwa. Foreman alimchapa Michael Moorer kwa KO, Novemba 1994 kushinda ubingwa wa WBA na IBF akiwa na umri wa miaka 45 na siku 299. Hiyo ilikuwa miaka 20 tangu aliposhinda ubingwa wa dunia wa uzito wa juu mwaka 1974.

Foreman mapambano yake 81 aliyopigana, amepoteza mara tano tu. Moja ya mapambano hayo machache aliyopita, moja ni la Muhammad Ali, ambalo linafahamika na wengi kama moja ya mapambano bora kabisa ya masumbwi yaliyowahi kutokea, Rumble in the Jungle.

Foreman, alikuwa na umri wa miaka 25 wakati huo na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda baada ya kuwa na rekodi ya kushinda mapambano 40 na 37 ilikuwa kwa KO. Mabondia hao wawili walipigana mbele ya mashabiki 60,000 huko Zaire, sasa DR Congo, Ali alitumia ubunifu wake uliofahamika kama ‘rope-a-dope’  na kushinda kwenye raundi ya nane.

Kadirio la watu bilioni moja walitazama pambano hilo kupitia televisheni. Ali alifariki dunia mwaka 2016, akiwa na umri wa miaka 74,  lakini wawili hao walimaliza tofauti zao na kuwa marafiki.

Pambano la mwisho la Foreman lilikuwa Novemba 1997 - wakati huo akiwa na umri wa miaka 48 na siku 316 - alipopigana na Shannon Briggs.